HILI NDILO JIWE LA AJABU NCHINI TANZANIA NA HAIRUHUSIWI KULIPANDA WALA KULISOGELEA
Maana ya neno Mbuji ni "Kitu kikubwa"
1. Ni jiwe pekee kubwa Mkoani Ruvuma,
2. lina vyanzo vingi vya maji chini yake,
3. Ni ngumu kulipanda na ukithubutu yatakayokukuta ni juu yako na tayari Mzungu mmoja kapoteza maisha'
4. Ni ngumu kulizunguka,
5. Hutumika kwa matambiko kwa baadhi ya koo,
6. Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo kwa yeyote anayetaka kulifikia ama kupanda,
7. Ni kivutio kikubwa kwa wageni wachache ambao
hutembelea Litembo, Maguu, Hagati nk huko Mbinga,
8. Linaheshimika sana na wakazi wanaolizunguka jiwe hilo,
9. Sehemu kubwa ya watu wananchi wanaolizunguka hawajawahi kulipanda wala kulisogelea kwa hofu,
10. Jina la jiwe hilo ndilo jina la Tarafa ya Mbuji wilayani Mbinga.
Comments