RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAMILIONI WAJITOKEZA HITIMISHO LA SIKU YA VIJANA DUNIANI RIO

Watumishi wakihudhuria ibada ambayo imefanyika Jumapili kwenye fukwe za Copacabana jijini Rio de Janeiro, Brazil. ©AP
Papa akiwapungia mkono maelfu ya vijana ambao wengi wao walilala ufukweni katika kusubiri hitimisho la siku ya vijana duniani inayoandaliwa kila mwaka na kanisa katoliki. ©AP
Makumi kwa makumi elfu ya watu wakiwa kwenye ufukwe wa Copacabana jijini Rio kwenyw maadhimisho ya siku ya vijana duniani. Takriban watu milioni 3 walijitokeza kwenye hitimisho ya siku hiyo, tarehe 28 Julai. ©AP
Baraka zikitolewa kwa mtoto mmojawapo aliyekuwepo kwenye hadhira ya hitimisho la siku ya vijana duniani. Papa akiwa ndani ya kigari chake. ©AP

Masista wakiserebuka wakati wakisubiria ratiba kuanza kwenye fukwe za bahari ya Copacabana jijini Rio de Janeiro, Brazil. ©AP
Masista raia wa Poland wakiwa kwenye ufukwe wa Copacabana jijini Rion de Janeiro nchini Brazil wakati wa maadhimimisho ya siku ya vijana duniani ya kanisa katoliki. ©Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images
Masista wakifurahia pamoja na vijana kutoka mataifa mbalimbali kwenye ufukwe wa Copacabana jijini Rio, Brazil. ©AP
Mwanamama akisali siku ya Jumapili wakati siku ya vijana duniani ilipokuwa ikihitimishwa jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. ©AP
Papa Francis akifunga jumuiko la vijana kwenye maadhismisho ya siku ya vijana duniani jijini Rio de Janeiro nchini Brazil, ambapo aliwataka vijana kueneza Neno hata kwa wale wasiofikiwa. ©AP
Papa Francis akizungumza na vijana wa nyumbani kwake (Argentina), kwenye kanisa la Rio de Janeiro. ©Nelson Almeida/AFP

Comments