RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO CHOIR ST. JAMES ARUSHA YATIMIZA MIAKA 46 KWA KISHINDO

kwaya na vikundi vingi vimeanzishwa na kuvunjika katika hali isiyotarajiwa ama katika ya mafarakano. Lakini mfano wa kikundi cha kwaya ambacho kimedumu katika huduma ni kwaya ya Upendo ya Mtakatifu James jijini Arusha. Wiki hii ambayo imeaisha, wametimiza rasmi miaka 46 ya kuanzishwa kwake.
28 July 1967, ndio kundi la watu 12 walianza na kwaya hii, lakini sasa kwaya ina jumla ya wahudumu 68. Wkongwe wachache wapo, akiwemo mmojawapo wa watu walioanza nayo tokea mwaka 68, Mama Chausa. Zifuatazo ni baadhi ya picha kama ambavyo zimeifikia Gospel Kitaa.

Upendo Kwaya wakiwa stejini tayari kuimba wimbo"Kama siyo yale mateso" katika kusheherekea miaka 46 ya uimbaji.


Ibada ya kusifu na kuabudu ikiendelea.




ANGALIA MATUKIO MENGINE

Bonyeza "Read More" HAPO CHINI





Worship team wakishambulia jukwaa.
Mtumishi Christian Mwabukusi akifundisha maana ya namba Saba
Mchungaji Kajembe(Aliyepiga magoti mbele) akiombewa juu ya Kuvikwa vazi la utumishi na aliyesimama nyuma yake ni Mtumishi Christian Mwabukusi akiongoza sala

Mtumishi wa Mungu Mwabukusi akichovya vitambaa kuwakilisha damu na MAJI vilivyomwagika pale msalabani na kufanyika ukombozi kamili wa Mwanadamu



Mtumishi Mwabukusi akiombea watu utakaso.
Watu wakiwa wamezama Kwenye Maombi, tazama picha ya mbele binti kava skafu inayowakilisha Bangi,Injili inahitajika zaidi kwa watu Kama hawa!
Kwaya ya KKKT Usharika wa Ngateu Arusha nao walikuwepo kusheherekea miaka 46 ya uimbaji tangu Kwaya ya Upendo kuanzishwa.
Mchungaji kiongozi Rev.Kajembe,Mwinjilisti Aminiel Nnko wa Safina Radio na Mchungaji Alice wa Mount Meru University wakiombea watu Kwenye Semina iliyoandaliwa na Upendo  kwaya katika kuadhimisha miaka 46 ya Uimbaji.
Picha zote kwa hisani ya Samuel Kusamba

Comments