RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA



Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo Gospel Kitaa imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Katikati ni Askofu Moses Kulola

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

Askofu Moses Kulola akiwa Israel

Tutaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.Kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola ingia hapa.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.

Kipindi Askofu Moses Kulola anaumwa. Hapa akiwa na mjukuu wake



Enzi za uhai wake
Akiwa mkutanoni


Akiwa katika gari lake alilozawadiwa na kanisa la E.A.G.T

Gari alilokuwa akitumia enzi za uhai wake
Source: GK

Comments