Kiongozi mmoja wa madhehebu ya wanaokula nyama za watu akijiita Yesu Mweusi, ambaye aliwachinja wafuasi wake wa kike wanaojulikana kama 'Flower Girl' na kunywa damu yao, amejiua mwenyewe kwenye misitu minene ya Papua New Guinea.
Akiwa kavalia majoho, Stephen Tari, mwenye umri wa miaka 40, mwanafunzi aliyeshindwa masomo ya Biblia, aliwahi wakati fulani kuongoza 'wafuasi' 6,000 kwenye mikoa ya milimani nchini humo, lakini alituhumiwa kwa kuua wasichana wasiopungua watatu na, huku mama zao wakilazimishwa kutazama, akinywa damu zao.
Akijiita mwenyewe 'Yesu wa ukweli', alitiwa hatiani kwa ubakaji miaka mitatu iliyopita - kabla ya nchi hiyo kutunga sheria mpya zinazosema wauaji wanaotiwa hatiani na wabakaji wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo - na alikuwa miongoni mwa wafungwa 48 ambao walitoroka gerezani miezi sita iliyopita.
Tangu wakati huo amekuwa mafichoni akiwa na wafuasi wake wa kutosha waaminifu, lakini maisha yake ya vioja yalifikia mwisho pale aliposemekana kumuua mwanakijiji wa kike wiki hii na kujaribu kukatisha maisha ya mwingine.
Akiwa amezingirwa na wanakijiji wenye hasira kali Alhamisi, anaaminika kupigwa na kukatwakatwa hadi kufa, sambamba na kibaraka wake kwenye kijiji kinachofikika kwa tabu cha Gal kilichoko katika jimbo la kaskazini la Madang.
Uchunguzi rasmi uliofanywa na Daily Mail miaka sita iliyopita uliwahoji wanawake watatu ambao walisema walishuhudia Tari akinywa damu ya binti zao waliouawa kwenye sherehe za kafara ya ajabu katika vibanda vya kijiji huku akiongoza wafuasi wake kukatisha kwenye msitu huo mnene.
Sababu ya eneo hilo ambako aliuawa kutofikika kwa urahisi, polisi hawakuwa na uwezo wa kusema kama alituhumiwa kumuua mwanamke sababu alianzisha upya dhehebu lake la zamani na alihitaji kafara zaidi za binadamu.
Mkuu wa polisi wa jimbo la Madang, Sylvester Kalaut alieleza kwamba kijiji hicho ambacho Tari alikumbwa na mauti yake kiko maili kadhaa kwa miguu kando ya njia za msitu mnene kutoka mji huo mdogo wa karibu.
"Tunapeleka polisi na daktari kwenye kijiji hicho kuchunguza chanzo cha kifo hicho.
"Kijiji hicho ambacho alikuwa akiishi ni masaa manne kutembea kwa miguu na kutokana na ushauri na ripoti zilizopatikana za hali ya mwili wake, atalazimika kuzikwa haraka iwezekanavyo baada ya uchunguzi kufanyika," alisema Kalaut.
Ofisa huyo wa polisi alionya kwamba wafungwa wengine ambao bado wamejificha na ambao wamekuwa wakijihusisha na Tari wajisalimishe wenyewe.
"Kwa sasa amekufa na hii inaweza kuwa maajaliwa ya wengine ambao pia wamezitoroka mamlaka husika. Ninaonya na kuwatahadharisha wote waliotoroka kujisalimisha wenyewe kwa mamlaka husika."
Katika kilele cha uovu wake, Yesu Mweusi alikuwa akivaa majoho meupe huku akisimama juu ya mwamba kwenye msitu mnene akitakasa na kuhubiri aina yake ya injili kwa wafuasi wake. Aliueleza umati huo kwamba watapokea zawadi kutoka mbinguni kama wakimfuata yeye.
Lakini nyuma ya mahubiri yake alikuwa na dhamira ya kishetani. Akiwashawishi wasichana wadogo aliowaita 'Flower Girls' kuingia ndani ya vibanda, aliwachinja shingoni na kunywa damu zao, kinamama walithibitisha baadaye.
Mwanamke mmoja alisema aliamriwa kunywa damu ya binti yake mwenyewe katika moja ya matukio hayo.
Polisi hawakuwa na uwezo wa kumkamata, licha ya kufahamu alikokuwa sababu ya uwepo wa 'kundi' lake kubwa - alikuwa akilindwa na kibaraka aliyekuwa akibeba bunduki kubwa, mikuki na pinde na mishale.
Lakini wanakijiji hatimaye walifanya 'nguvu ya umma' mwaka 2007 na hatimaye Tari akahukumiwa kifungo jela.
Sasa, ni nguvu ya kijiji kwa mara nyingine tena ambayo imehitimisha mafundisho yake haramu. Inatarajiwa atazikwa karibu na jamii ndogo ya msituni ambako aliuawa.
Comments