Kwaya ya Uinjilisti Sayuni yenye makao makuu yake kanisa la Kilutheri Kinondoni jijini Dar es salaam, siku ya jumapili iliyopita waliendeleza wimbi lao la Uinjilisti kwakuwatembelea watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa katika hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na watoto yatima wa kituo cha Malaika kilichopo Kinondoni jijini hapo.
Akizungumza na GK mwenyekiti wa kwaya hiyo bwana James Makatta amesema
kwaya hiyo imekuwa ikifanya huduma kama hizo kwa muda mrefu ingawa si
kwa mfululizo na wamekuwa wakimuona Mungu akiipigania kwaya hiyo
kwakufanya ibada kama hizo na kutoa wito kwa vikundi vingine na jamii
kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuwatembelea watu wasiojiweza na wenye
uhitaji ili kutimiza wajibu wa Mkristo kwa vitendo na si maneno pekee.
Ambapo kwaniaba ya hospitali hiyo mmoja wa wauguzi aliishukuru kwaya
hiyo, na kutoa wito pia kwa watu wengine kufika hospitalini hapo
kusaidia watu kwakuwa kuna wazazi wapo zaidi ya miezi sita wakiwa tunza
watoto wao ambao wanapata matibabu wengine wakiwa wametelekezwa bila
msaada. Baadhi ya vitu ambavyo kwaya hiyo imetoa ni pamoja na dawa za
meno, sabuni, biscuits, juisi huku katika katika kituo cha watoto yatima
walitoa vitu kama hivyo pamoja na mbuzi mmoja na pesa taslimu 30,000.
Kwaya ya Sayuni ni moja kati ya kwaya kongwe nchini ambayo uimbaji wao
ni wakipekee na wakitambulishwa sana na vazi la kimasai ambalo ni moja
kati ya sare ya kwaya hiyo tangu miaka ya 90, kwasasa wameachia album
mpya ya sauti iitwayo "Dua na Maombezi" ambayo wanaisambaza wenyewe huku
wakiwa njiani kuachia video yao ambayo picha na mandhari ya maeneo
yaliyotumika katika kurekodi video hiyo pamoja na ujumbe uliomo ndani ya
nyimbo hizo utafanyika baraka zaidi kwa watu watakaobahatika kuipata.
GK imeishuhudia video hiyo ikiwa katika hatua za mwisho za kuhaririwa.
Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Sayuni wakiwa nje ya wodi ya watoto kabla ya kuanza uinjilisti. |
Muuguzi wa wodi hiyo akitoa shukrani kwa kwaya ya Sayuni kwa kutembelea wagonjwa hospitalini hapo |
Comments