Zifuatazo ni nukuu za baadhi ya viongozi mbalimbali ambao wako kwenye msiba wa Askofu Mkuu Dkt Moses Kulola ambaye amepumzika siku ya Alhamisi. Gospel Kitaa imekukusanyia sehemu ya kwanza ya nukuu hizi kutoka kwa viongozi hawa, fuatana nasi.
Baadhi ya viongozi wakiwa viti vya mbele, Askofu Kakobe akiwa amefika muda si mrefu kutokea uwanja wa ndege. |
Mh. Mbunge, Dr Getrude Rwakatare.
1976, alipohubiri nilikuwa na matatizo ya ndoa, nilipookoka bado nilikuwa
na mateso ya ndoa, nikamuuliza mbona hivi? Akachukua jukumu la kuniandikia
barua moja kila mwezi, na kuniambia hakupigi wewe anampiga Yesu, hakutesi wewe,
anamtesa Yesu. Alinitia moyo hadi nilipokuwa mchungaji.
Alipokuwa anapelekwa India kwa ajili ya matatizo, nilipata nafasi ya kwenda
kumuona Chanika, akaniombea na kunitamkia maneno kwa dakika 15, nikaona kama
nimependelewa, na maneno ya mwisho na usia ili niweza kuendelea kumtendea kazi
Mungu.
Baba amefanya kazi nzuri sasa ni sisi kuweza kufanya kazi ya BWANA bila
kujihurumia.
Bishop Dr Methud Lyamungu, Methodist Church
NImekuwa nikimfahamu Kulola, juzi tu nilipofika uwanja wa ndege nikapokea
msg kuwa hatunaye, amepumzishwa, ilikuwa shock, lakini namshukuru Mungu.
Nakumbuka miaka ya late 80's kulikuwa na mkutano kwenye kanisa la udugu,
nikamwalika kwa chakula cha jioni, alikuja, nikashangazwa na unyenyekevu wake,
ni rafiki wa wote, hana adui.
Askofu Esambu Mitachi Polo;
Bila Kulola sijui ningekuwa wapi, huduma yangu imeinuliwa na makanisa ya
Ask. Moses Kulola. Lakini mkumbukkue hivi ndugu zangu, msafara wa mamba, kenge
wapo. Yesu ndie muweza yote na yeye ndiye aliyezungumza haya.
Tunaweza kuzungumza maneno mazuri, lakini matendo hatuna. Tumtazame Yesu,
maana hata huyu aliyetuacha, alikuwa anatuasa tumtazame Yesu, huwezi kuingia
mbinguni bila mamlaka ya Bwana Yesu, usiwe kenge.
Tanzania tumtazame Yesu. Moses amekwenda, lakini Yesu yupo, amefanya kazi
zake atalipwa na Bwana Yesu, na wewe ufanye kazi zako utalipwa na Bwana Yesu.
Kiburi kitu kibaya, unafiki kitu kibaya, haya ndio maneno nayosema kwa Watz.
Phillip Mangula (makamu m/kiti wa CCM bara)
Moses nimeanza kumfahamu 8 /8/1083 nikiwa mkuu wa wilaya ya Kwimba, kipindi
kile mtakumbuka kulikuwa n tofauti kidogo ndani ya kanisa, barua iliandikwa
nchi nzima ya kuzuia Moses Kulola asihubiri kwa jina la kanisa, na mi niliipata
kwangu.
Nikamweleza Moses Kulola, akaniambia, kijana wangu, mimi sitahubiri kwa
jina la kanisa lolote, nitahubiri kwa jina la Yesu.
Nikawaita OCD, kwamba bwana, Moses Kulola hatahubiri kwa dhehebu lolote, atahubiri
kwa jina la Yesu.
Tareje 9, tumemaliza mkutano, alihubiri mkutano mkubwa sana, mke wangu
akajifungua mtoto wa kiume, nikamwita Moses, kwahiyo mtoto wangu anaitwa Moses
Malumbo Kulola.
Dakika 20 baada ya kifo cha Dr Moses Kulola, nilipata msg, wakati huo
nilikuwa nimetoka Njombe kumzika binti yangu wa mwisho, kipindi ambacho Moses,
mtoto wangu alikuwa anaoa, Moses anao, dada yake mdogo anafariki, kwahiyo
nilichelewa kidogo, lakini nimefika kushuhudia.
Alipotoka India alikuja na mwanae huyu hapa, tulizungumza mengi sana,
lakini haoa si mahala pake, itoshe tu kusema, Moses alikuwa mtu wa watu. Aliendeleza
injili, nasi tuiendeleze.
Theresia Uvinza
Nimemfahamu 1985, baada ya kumaliza chuo kikuu nilienda kufundisha Songea Girls,
na hapo kulikuwa na rafiki yangu, Mama Hyela, walokole wa kwanza Songea. Siku
moja aliomba nimshikie wanafunzi kwa kuwa mchungaji alikuwa anafikia kwake.
Nikamuuliza huyu mchungaji anafanana na Yesu?Akasema pengine, ila ukitaka
kumuona, unaweza maana amefikia kwangu. Tukawaacha wanafunzi wote, tulifanya
hilo kosa…
Tukasubiri na kusubiri na mida ya saa tisa, alipotoka nikajisikia kupiga
magoti, nikamwambia baba naomba uniombee – na kweli akaniombea, nilikuwa na
shilingi elfu moja tu, nikampa. Naamini mafanikio niliyo nayo ni kutokana na
maombi niliyofanyiwa mwaka 1985.
Kwa hiyo kila wakati ambapo nilikuwa nikisikia Moses Kulola amekuja DSM,
kwenye viwanja vya Jangwani , huwa sikusita kuhudhuria, labda tu niwe nje ya
Dar. Nakumbuka aliwahi kusema nywele zake zilikuwa zinampotezea muda, hivyo
akamuomba Mungu zibaki hivyo hivyo, na kweli zikabaki. Huu ni ushahidi kwamba
kuna alikuwa anazungumza na Mungu.
Advera Senso (Msemaji wa Jeshi la Polisi)
Hata kama leo tungeamua takamate watenda dhambi wote, si kwamba wangebadilisha
matendo yao kiroho na kimwili.
Amekuwa pia akimbwambia IGP Said Mwema, kuwa unpoona makosa ya jinai
yanaongezeka hizo sisi watumishi wa Mungu tunaita dhambi, amwambie ili atume
watu ama aende mwenyewe kuhubiri.
Hivyo tumekuwa tukiona makosa yakizidi sehemu, tunawasiliana na yeye
anaenda kuhubiri injili eneo hilo.
IGP anasema chipukizi waendelee kuhubiri injili, hadi kweny ngazi ya
familia, kwasababu wahalifu wako kwenye familia, wako kwenye mitaa…
Na watu wa Mungu niwawambie kuwa tushirikiane na serikali kuhakikisha kuwa
wahuni wachache hawabadilishi amani iliyopo. Tuendelee kuhubiri na watu
waokoke.
Paulo
Nashangaa kwa nini nimekuuja hapa, nitazungumza kidogo tofauti na m/kiti
wangu.
Nilianza kumfahamu kaka yangu mwaka 67, akiwa ndio ameanza kazi kipindi
hicho, nikawa namshangaa sana, nasema huyu mbona anapoteza muda, anazunguka na
baiskeli huku na huko nikasema hapa tuna kazi kilichonipa faraja ni pale
nilipoanza kuanza kazi yake.
Faraja niyoipata ni pale alipokuja Kilimanjaro, kipindi ambacho alinyimwa
kuhubiri. Akaja kunionmba msaada ofisini, nikamwambia nani amekwambia akasema,
aah aah, ni hilo ni nimekufikishia.
Nikamwambia kwa jina la Yesu utahubiri. Tukasimamia akafnya mkutano mkubwa
sana, na lipomalia akaja ofisini kwanguna kuniambia sina cha kukulipa, piga
magoti.
Akaniambia nitakuwakiongozi mzuri, baada ya hapo haikuchukua muda nikapelkwa
Mbeya kama mkuu wa mkoa. Baraka zikaendelea, nikapata na uwairi, na tena
uwaziri mwingine… nikakoswakoswa kidogo niwe waziri mkuu.
Assumpta Mshama (Mh Mbunge Nkenge/Mchungaji
Msaidizi, Mito ya Baraka)
Watz, hatuna haja ya kuendelea kulia, sanasana ni kumshukuru Mungu… Hata
ubunge huu nilipoupata, ni kipande kidogo cha Mzee huyu…
Wakati naokoka, 1989 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, nilipoongozwa na mtu
ambaye hata pia hajaokoa.
Nilipookoka kazi yangu ilikuwa ni kupika chakula na kumpelekea mahali
popote. Na pia baadae nikaanza kurekodi video za mikutano yake.
Nilipotaka kuwa Mbunge, akaniambia utakuwa mbunge – na nilifanikiwa.
Mary Alice Chipungahelo (former RC, DSM)
Nilipoteuliwa kuwa RC, wakaniambia utaweza, nikasema zaidi ya hilo,
nitapambana usiku na mchana…
Baba, sasa ni hayati Moses Kulola, alikuwa karibu na mimi sana, na kila anapokuja
DSM, lazima anitembelee, Baba huyu, nilikuwa na matatizo, “mwanamke naye nini,
mwanamke naye nini”
.
Alikuja nyumbani, nikamkaribisha nikapiga magoti, akauliza una nini,
nikamwambia nataka natakasika. Mungu alizidi kuniunganisha naye, nikiwa Mwanza,
aliwekwa ndani, nilipopata taarifa, tukapelekeana simu – lakini kama unavyojua
kila mka na taratibu zake. Tulikubaliana mzee akatolewa, na akaja kunitafuta
ili anie shukurani, nikamwambia hapana shukurani mpe Mungu, maana ndio
ametuwezesha.
“Piga magoti” akaniambia, “unataka nini”, nikamwambia nataka niwe na afya
nifanye kazi bila upendeleo wala rushwa.
Na ikawa hiyvo, nikapaishwa hadi Canada nikawa
msaidizi wa Balozi, kazi ya heshima sana. Nimekuja kw moyo mweupe kabisa
moyo mkunjufu, mama nikwambie kuwa wajane tuko wengi, wewe umebahatika
kuwa na mzee anayeikjua dini, sisi wengine tumeolewa olewa tu…
Tunakutakia kila kheri, afya njema, ulee watoto, na watoto nao wana watoto wao…
Nukuu zaidi za viongozi mbalimbali zitaendelea kuwajia kupitia Gospel Kitaa.
Inatoka GK
Comments