RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UTABIRI MZITO WA T.B JOSHUA, KIONGOZI WA NCHI MOJAWAPO AFRIKA MASHARIKI KUTEKWA



Hali ya tahadhari imetolewa na watu kuingia katika maombi kutokana na utabiri mzito uliotolewa na mtume maarufu barani Afrika T.B Joshua kutoka kanisa la Scoan Nigeria ambaye katika ibada ya jana ametangaza kuna moja ya nchi Afrika mashariki lakini sio Kenya, kiongozi wake atatekwa na watu ambao yeye hawajui wala sababu za kiongozi huyo kutekwa hazijui.

Akizungumza katika ibada ya jana kanisani kwake mtume huyo amesema nchi ambayo iko hataraini kukutwa na tukio hilo ambalo iliwahi kupatwa na matatizo watu wake wakiwa wanakunywa na kucheza na kwamba tukio hilo linatokea tena.

T.B Joshua hakutaka kutaja jina la kiongozi huyo wala nchi anayotokea ingawa ameshaambiwa na Mungu na kusema kwamba endapo Mungu atamtaka kutaja jina la kiongozi na nchi atokayo atafanya hivyo. Ila kwasasa amewataka wana Afrika mashariki kumuomba sana Mungu ili jambo hilo lisitokee. kwa maelezo zaidi. Tazama na kusikiliza katika video hapo chini.



Source: Gospel Kitaa

Comments