RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ANGALIA PICHA ZA SHANGILIENI KWAYA WAKIWA AFRIKA YA KUSINI KIHUDUMA

Kwaya ya Tumaini Shangilieni toka St.James Kaloleni Arusha inatarajiwa kuwasili siku ya leo ikitokea nchini Afrika ya kusini ambako ilikwenda katika kanisa la Anglican kitongoji cha Tembisa jijini Johannesburg kihuduma. Kwaya hiyo ambayo iliondoka na ndege ya Fastjet siku ya ijumaa, imefanikiwa kufikia lengo lililowapeleka nchini Afrika ya kusini kumuhubiri Kristo.

Wakati huohuo taarifa ambazo blogu ya GK imezipata ni kwamba kwaya hii inatarajiwa kuwepo usharika wa Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam siku ya tarehe 8 mwezi ujao katika kuwasindikiza kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ambayo itakuwa ikisherehekea miaka 25 ya kwaya yao tangu ilipoanzishwa.

Taarifa kamili na picha nyingine zitawajia kupitia katika blog ya GK. Kwa leo pata japo kwa kifupi

KAZI NZURI GOSPEK KITAA..BIG UP..!!

Mawinguni mwe!

Muonekano wa jiji la Johannesburg kutokea juu karibu na uwanja wa ndege wa OR Tambo.

Mwenyekiti wa Tumaini Dkt. Emanuel Mtangoo na wanakwaya wengine wakizungumza na mwenyeji wao mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa OR Tambo.

Safari ya kuelekea kanisani.

Usharikani Tembisa.

Waimbaji wa Tumaini wakiwa kanisani siku ya jumapili.



Mmoja wa waimbaji wa Tumaini Angel Minja alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, wenyeji walimuandalia keki.

Mwenyekiti wa Kwaya Dkt. Emanuel Mtangoo akimkabithi Dkt. Emmanuel Mbennah zawadi ya kitabu kutoka kwa Askofu Stanley Hotay wa Dayosisi ya Mt.Kilimanjaro Tanzania.

Waimbaji wa Tumaini wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa Dkt. Emmanuel Mbennah.

Waimbaji wa Tumaini walitembelea kituo cha radio cha Trans Wordl, hapa wakipewa maelezo.

Mwenyekiti wa kwaya Dkt. Emmanuel Mtangoo akiwa studio kwa mahojiano.

Waimbaji wakiwa wameandaliwa mema ya nchi mbele yao mara baada ya maelezo ndani ya kituo hicho.



Tumaini wakiwa mbele ya lango la kuingilia kituoni hapo.

Mdau wa GK, bwana Kusamba akiwa ameweka pozi jijini Johannesburg.



Tumaini Choir wakiwa mitaa ya Soweto nchini Afrika ya kusini.

SOURCE: gospelkitaa.blogspot.com/2013/11/angalia-picha-za-shangilieni-kwaya.html



Comments