SIKU hizi uovu hauchagui pa kutua, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejikuta katika hali mbaya baada ya kulishwa sumu na mtu mwenye nia mbaya, Akizungumza na mapaparazi wetu kanisani kwake, Kawe, Dar es Salaam hivi karibuni, Gwajima aliweka wazi kwamba, tukio hilo lilimtokea mwanzoni mwa mwezi huu.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. MCHEZO ULIVYOANZA
Mchungaji Gwajima ambaye anasifika kwa kuwarejesha katika hali ya ubinadamu watu waliodhaniwa wamekufa (misukule) alisema kuwa sumu hiyo aliwekewa kwenye soda aliyokaribishwa na askofu mmoja mkuu wa kanisa kubwa nchini Tanzania (jina kapuni).
“Siku hiyo, huyo askofu aliniita nyumbani kwake (hakupataja jina), nikaenda nikiongozana na askofu mwingine ambaye ni rafiki yangu.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. MCHEZO ULIVYOANZA
Mchungaji Gwajima ambaye anasifika kwa kuwarejesha katika hali ya ubinadamu watu waliodhaniwa wamekufa (misukule) alisema kuwa sumu hiyo aliwekewa kwenye soda aliyokaribishwa na askofu mmoja mkuu wa kanisa kubwa nchini Tanzania (jina kapuni).
“Siku hiyo, huyo askofu aliniita nyumbani kwake (hakupataja jina), nikaenda nikiongozana na askofu mwingine ambaye ni rafiki yangu.
MAONGEZI KUHUSU MUNGU NA SODA JUU
“Tulipofika, tuliongea mambo mengi ya kiroho. Baadaye akatupa soda lakini nilipoinywa nilihisi kuna kitu ndani yake. Roho wa Mungu pia akasema nami kuhusu hilo, palepale nilimwambia yule askofu kwamba amenipa soda yenye sumu ndani yake,” anafunguka Gwajima kwa mara ya kwanza.
“Yeye alikuwa akikataa kwamba hajaniwekea sumu kwenye kinywaji hicho lakini cha kushangaza alionekana kutetemeka sana.”
AISHIWA NGUVU, AAGA
Gwajina alisema filamu ya sumu hiyo haikuishia hapo kwani ghafla alianza kuhisi kuishiwa nguvu jambo ambalo lilimshtua na kuanza kubabaika.
Gwajima: “Niliondoka haraka sana huku nikimhakikishia yule askofu kwamba sitakufa bali nitaishi kama maandiko yanavyosema kwa kuwa naamini katika ufufuo na uzima.
MKEWE AMTAKA AENDE HOSPITALI
Akaongeza: “Wakati huo nilikuwa nikitakiwa kuja kwenye huduma hapa kanisani, nikaingia huku tumbo likiwa linakata sana. Cha kushangaza nikafanya maombi kama kawaida.
“Nilipomaliza huduma nilirudi nyumbani na kumwambia mke wangu. Yeye akanisihi niende hospitali lakini nilikataa.”
AENDA KUONANA NA DAKTARI WAKE
Gwajima anaendelea: “Katikati ya usiku mnene, nilisikia kitu kimelipuka tumboni na maumivu makali yakafuatia, nilimwomba Mungu anifikishe hadi asubuhi. Ilipofika nilikwenda kwa daktari wangu ambaye baada ya kunichunguza aliniambia nilipewa sumu ya kuniharibu akili na si ya kufa kama nilivyodhani.”
Mchungaji huyo aliendelea kusema kwamba, daktari wake huyo alimwambia kwa vile sumu hiyo aliinywa kidogo dawa yake ni kunywa maji mengi ili kuimaliza kabisa, akamtahadharisha kuwa angeinywa kwa kiwango kikubwa na kuchelewa tiba angechanganyikiwa akili kiasi cha kushindwa kuwa na mawasiliano mema na binadamu wenzake.
ASKOFU ALISHALIPWA FEDHA ILI AMDHURU GWAJIMA
Gwajina alisema katika utafiti wake, aligundua kuwa askofu huyo alilipwa shilingi milioni 300 na wabaya wake ili wamdhuru kwa sumu hiyo, lengo ni kumfanya ashindwe kutoa huduma ya kiroho katika kanisa lake ambalo linakua siku hadi siku.
AMPIGIA SIMU ASKOFU MBAYA WAKE
“Asubuhi ya siku iliyofuata nikiwa nimepata nafuu nilimpigia simu yule askofu nikamwambia kwa kumtania kwamba anigawie pesa kidogo katika hizo alizolipwa,” alisema Gwajima.
AMWACHIA MUNGU
Gwajima alisema alikuwa na uwezo wa kumpeleka mbele ya sheria askofu huyo lakini kwa vile yeye ni mtumishi wa Mungu alitakiwa aoneshe mfano wa kusamehe kama maandiko yanavyotaka.
Hata hivyo, alisema kama angeamua kumwanika askofu huyo ana uhakika waumini wake wangetimka kanisani kwake na kubaki yeye na familia yake tu.
SOURCE: http://www.vitukovyamtaanews.com/2013/11/mchungaji-gwajima-alishwa-sumu-na.html#axzz2m9mbNjEQ
Comments