WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA MIZENGO PINDA KUNGURUMA MADHABAHU YA RGC TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA WIKI HII
·
Ni katika
sherehe ya kihistoria kutimiza miaka saba ya Urejesho
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Jumamosi ya wiki hii, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika sherehe maalum ya kutimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwa kanisa la RGC
Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti
hili ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Kiongozi wa RGC Tabata Chang’ombe Mtume Peter
Nyaga, alisema wanajisikia faraja kubwa kama kanisa kutokana na uamuzi wa Waziri
Mkuu Pinda, kukubali kufika katika sherehe hiyo ya kihistoria katika kanisa
lao.
“Sisi
kama kanisa tumefurahishwa sana na uamuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
kukubali kushiriki katika sherehe yetu hii, tunajivunia kuwa naye katika siku
hii ambayo inaakisi harakati zetu za kumtumikia Mungu ambazo zimekuwa na
mafanikio makubwa tangu siku niliyoitwa kwa ajili ya kumtumikia Bwana katika
nchi hii” alisema Mtume Nyaga.
Alisema
pamoja na kupitia changamoto nyingi ikiwemo kufungwa jela kwa sababu ya
kumtumikia Mungu, lakini wanashukuru kwa sababu Mungu amekuwa pamoja nao na
kuwafanikisha kwa kiasi kikubwa katika kipindi chote cha miaka saba ambacho
kimeshuhudia maelfu ya watu wakikombolewa kutoka katika utumwa wa shetani na
kurejeshwa katika ufalme wa Mungu.
Tangazo limetengenezwa na Rumafrica +255 715851523
Kwa
mujibu wa Mtume Nyaga, sherehe hiyo ya kihistoria itatanguliwa na semina maalum
ya uumbaji na maajabu, itakayofanyika Jumapili
ya leo ni kuanzia saa 3 asubuhi hadi 6 mchana na kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa
semina itafanyika kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni. Alisema Semina
hiyo itahitimishwa kwa sherehe kubwa ya kanisa itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 7/12/13 kuanzia saa 5
asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo Mgeni
rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza
Peter Pinda (MB).
Akiingumzia
siku hiyo, Mtume Nyaga alisema, itahusisha mambo kadhaa ikiwemo Kutimiza miaka
saba (7) ya Kanisa, kufanya tendo la huruma la kula chakula cha mchana na
watoto yatima, walemavu na wajane, kuzindua Vitabu 7 vya Urejesho
vilivyoandikwa na Mtume na Mchungaji Peter Njue Nyaga kwa neema ya Mungu ili
viwe Ukombozi kwa jamii ya Watanzania na kuwagawia chakula, walemavu, watoto
yatima na wajane.
Alivitaja
vitabu vitakavyozinduliwa siku hiyo kuwa ni pamoja na Nguvu ya Kibali, nguvu ya
uponyaji, Nguvu ya Imani, Nguvu ya Urejesho, Nguvu ya Roho Mtakatifu, Nguvu ya
Fedha na Nguvu ya Ujasiriamali ambavyo anaamini kwa neema ya Mungu
endapo vitatumika vizuri vitaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanadamu.
Mtume
Nyaga, alisema lengo la uzinduzi huo utakaohudhuriwa pia na Askofu Mkuu wa RGC
Duniani Dokta Arthur Kitonga, ni kwa ajili ya kutoa sadaka maalum ya ununuzi wa
lori la kuhubiria injili vijijini ili
kuwafikia ambao bado hawajafikiwa na Injili ili wengi wapate kuona matendo
makuu ya Mungu ya kuokolewa, kuponywa na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo
mbalimbali vya shetani.
Alisema baada ya kuhubiri injili kikamilifu
katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kuokoa watu wengi, sasa ni zamu ya
mikoani na hasa vijijini kwenye uhitaji mkubwa wa injili, hivyo alitoa wito kwa
wote wanaopenda kushiriki Baraka hizo kwa kuchangia kupatikana kwa lori hilo kutuma
sadaka zao kupitia Mpesa 0756-863528/
Tigo pesa 0716147361 au wafike siku ya tukio na Mungu wa mbinguni
atawabariki.
Comments