RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MKESHA WA KRISMASI KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA-DSM TANZANIA KWA NABII FLORA PETER

MAMBO YOTE YATAKUWA MAPYA
Mungu anakwenda kufanya mambo kuwa mapya mwaka 2014. Tugemea kupokea mambo mapya mwakani na hata kwani leo tunakumbuka siku ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kuzaliwa kwake kunafanya na mambo yetu kuwa mapya au kuzaliwa upya.


MIAKA SABA YA UREJESHO
Tunakwenda kurejeshewa vitu vilivyopotea kwa muda wa miaka saba. Bwana anakwenda kurejesha na kila kitu kitakuwa shwari. Hakuna mtu atakaye kufa kijinga kijinga
Yesu alipozaliwa katika Bethelemu, tazama mamajuzi wakaenda Yerusalemu na kuuliza yuko wapi aliyezaliwa kwa maana sisi tuliona nyota ya mashariki.


Maadui zako wataona nyota yako ikishamiri na watashangaa. Kuzaliwa kwa Yesu  uchumi wako unabadilika na utakuwa na mafanikio. Yesu ni nyota kuu inyong’ara na ndio maana maisha yetu yatang’ara.
Hutakiwi kufadhaika kwasababu iko nyota kutoka mashariki ambayo ni Yesu Kristo. Kama kuna rafiki au ndugu yako amefadhaika sema hakuna kufadhaika kwa maana iko nyota mashariki itakayobadilisha maisha yako.

Ninataka kukuambia kuwa huduma yetu ya maombezi inakwenda kuchipuka kwa maana Bwana wetu amezaliwa. Kama huna ajira utakwenda kupata tu kwa maana Yesu Kristo amezaliwa kwako.
Tumekuwa tukitangaza habari za Yesu Kristo na watu wanapona vipofu wanaona, wagonjwa wanafunguliwa, waliokufa wanafufuka. Ninasema hakuna jambo linalomshinda Mungu.

MAMBO MAPYA YANAKWENDA KUZALIWA
Bwana anakwenda kutupa mtawala katika maisha yetu na kutokana na yeye tutaona mafanikio, maisha ya ndoa yatakuwa mapya.Mungu nakwenda kufanya kila kitu kuwa kipya, kama ni nyumba utapata mpya, kama ni ajira utapata nzuri na mambo mengine mengi yatakuwa mapya.

Kama kuna mchumba wako amekuacha ninasema Yesu anakwenda kumpokonya na hatapata mchumba wako. Yesu amekuja kukomboa uchumba wako, uchumi wako, na kila kitu anakwenda kukomboa. Pokea Baraka sasa, pokea ushindi.

Historia ya maisha yako inakwenda kubadilika sasa kwa maana Yesu Kristo amezaliwa sasa. Utakapofika nyumbani au kazini kwako utaona connection ya kazi ikitokea. Utashangaa unafanikiwa na maisha yako yataanza kubadilika.

UTABIRI JUU YA NDOA
Kama Nabii Flora ninasema kwa jina la Yesu Kristo Yule mume wako au mke wako aliyekuacha anakwenda kurudi na atakukumbatia huku akitoa machozi. Hakuna kuoneana sasa kwani Yesu Kristo amezaliwa. Kwanini upate kushidwa katika ndoa yako wakati Yesu leo amezaliwa ndani yako?.


MABINTI KUPA WACHUMBA WAO SAS
Mabinti wote wa hapa kanisani mtakwenda kuolewa kwani uliumbwa ili uwe na mwenza wako, iweje leo ukose mchumba wako? Na kama ulikuwa na mchumba akakumbia ninasema anakwenda kukosa raha sasa na atatamani kurudi kwako kwa kukupigia magoti huku akilia machozi. Yesu hakuzaliwa ili wewe uteswe na mwanandamu kimapenzi...Kama Mungu aliruhusu ndoa basi na huyo aliyekupa uishi naye atakuwa wako na hatakwenda kwa kahaba tena.

KUZALIWA KWA YESU KRISTO KUNA MAANA NZITO KWETU
Ni ninakutabiria ya kuwa unakwenda kujenga nyumba yako mwaka 2014 na kama una nyumba unaenda kuongeza nyumba nyingine kwa jina la Yesu..
Kuzaliwa kwa Yesu kuna maana kubwa sana maisha mwetu. Tunatakiwa sasa kutafakari kwa kina na kujua dhumuni zima la Mungu kumtuma mwanae wa pekee kuja hapa duniani na alipofika wanadamu hawakumpokea katika mapokezi mazuri na hatimaye akaishia kuzaliwa katika zizi la ng’ombe. Lakini kwa sababu alitupenda  alivumilia mateso yote na hatimaye kutukomboa katika kifungo cha shetani.

Mimi na wewe tunatakiwa kuwa makini sana na siku ya leo kwani kuna mambo mengi yatajitokeza kutaka kukuvuruga kiimani. Kuna marafiki siku ya leo watatamani kukutoa katika uwepo wa Mungu na kukushirikisha kutenda dhambi.

Watakushauri mwende disko, na kama unamchumba atakushauri mfanye mapenzi, na kama una mpenda pombe atakushauri mnywe pombe na mambo mengine kama hayo.
Jitahidi siku ya leo kukaa katika uwepo wa Mungu ili asubuhi ya leo ukawe kiumbe kingine na kuzaliwa na Yesu Kristo.



















 Tembelea
Karibu kanisani, ukitaka kufika panda gari la Tegeta kama unatokea Mwenge na uliza kituo cha Mbezi Salasala na ukifika hapo uliza kanisa la Nabii Flora. 

Comments