NILICHOJIFUNZA NA KUONA KATIKA MKESHA WA KUAGA MWAKA 2013 KATIKA KANISA LA WORDALIVE SINZA MORI SIKU YA JANA--RULEA SANGA
Kuna mengi nimejifunza katika mkesha wa kumaliza mwaka katika kanisa la WordAlive Sinza Mori kwa siku ya jana.
Rulea Sanga wa RUMAFRICA aliyevalia shati lenye weusi na weupe katika tamasha la mkesha WordAlive Sinza Mori
1. Watumishi wa Mungu wanakwenda na wakati kuanzia mavazi yao na mazingira wanayoabudia. Hii ni tofauti sana na makanisa yetu ya awali huko vijijini kwetu. Sehemu za ibada zilionekana choka mbaya.
2. Vijana wanakuja mbio na wanaleta mapinduzi katika kumtangaza Yesu Kristo. Kunaekuwa na ubunifu mkubwa sana katika kazi ya Mungu. Kila kijana anataka kuja na kitu fulani cha pekee chenye mguso wa pekee ili apate kumuinua Yesu Kristo na mwisho wa siku apokee baraka kutoka kwa Mungu. Watu watakapoona kitu ulichonacho ni cha kipekee watakutafuta na kutaka kuwekeza kwako, na hii ni moja ya wewe kutoka katika hatua moja na kwenda katika hatua nyingine. Kuna watu Mungu amewapa fedha nyingi na hawaoni wapi wazipeleke ili zizalishe zaidi, na wengine wana vipaji lakini wanashindwa kuendeleza kwasababu hakuna support. Kwahiyo wewe mwenye talent unapaswa kuonyesha talent yako hata katika mazingira magumu na baadae watu watakujua. Mfano mzuri ni MC Pilipili...
3. Vijana wanajituma katika kutumia vipawa walivyopewa na Mungu.
4. Kuna ubunifu mkubwa sana katika uimbaji ukifafanisha na hapo mwanzo. Watu walio wengi wanatumia akili zao za kuzaliwa kufanya mambo makubwa wawapo majukwani kwaajili ya utukufu wa Mungu. wengine hawajasoma kabisa ila Mungu amewapa kitu fulani na hicho ndicho wanachokitumia kufanikisha kazi ya Mungu. Watu hawa wakiingia darasani kidogo tu watafanya mambo makubwa sana na utakuwa mtaji mkubwa sana na msaada mkubwa katika jamii yetu.
5. Watu wana hamu ya kufanya kazi ya Mungu hasa vijana ukifananisha na hapo mwanzo ambapo vijana walikuwa hawataki kabisa kuokoka, laikini sasa wao wenyewe wanatamani kuingia katika wokovu.
6. Vijana wanapendeza kimavazi na usafi kwa ujumla, tofauti na zamani ambapo walokole walionekana wamechoka sana na hawajipendi nikimaanisha ya kwamba, walikuwa hawapendi kupendeza.
7. Kuna changamoto kubwa sana kati ya wachungaji na waimbaji hasa vijana. Vijana wanamsimamo na hawaoni woga kumtania hata mchungaji wao. Zamani ilikuwa ngumu sana kumtania mchungaji wako.
8. Maeneo ya kufanyia ibada yamebadilika sana na kuwa bora sana ukifananisha na zamani ambapo nyumba za kuabudiwa zilikuwa mbaya sana na hazina mvuto.
9. Vijana wamekuwa wanajikita sana kuimba nyimbo kwa kufuata tamaduni za ulaya na kusahau kuwa kuna watanzania ambao utamaduni huo kwao ni mgeni na hauleti uwepo wa Mungu kwa maana hawaelewi lugha za wazungu. Kungekuwa na mchanganyiko fualni wa mambo ya Ulaya na huku Uswahili kwetu.
10. Komedi zamani ilionekana ni kituko sana na sio moja ya injili ya kumtangaza Yesu Kristo, lakini kwa sasa imekuja kwa kasi kubwa sana na watu wanapenda.
11. Sijajua suala zima la sarakasi katika madhabahu ya Mungu, lakini tutaona hapo baadae kwa maana hata komedi hatukuielewa inavyoingia lakini sasa tumeipata barabara...
Ni mimi Rulea Sanga
NI MAMBO MENGI NILIJIFUNZA LAKINI HAYO HAPO JUU NI BAADHI
ANGALIA MKESHA ULIVYOKUWA KATIKA POST YA HAPO CHINI

Comments