UJUMBE HUU UNAKUHUSU KABISA..NI IBADA ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FORA PETER SIKU YA JUMAPILI 22.12.2013
Nakusalimu kwa jina la Bwana, nakukaribisha katika wakati
mzuri wa neno la Mungu, nakukaribisha katika ibada hii iliyojaa upako na
utukufu. Katika wakati huu wa Bwana kukutendea, katika mwezi huu Adari, ambao
Bwana alifanya mapinduzi, akapindua mawazo ya Hamani akajitwalia ushindi
Modekai, na akawa na sifa na sifa zake zikavuma sana.
Akawa na ukuu tena ule ukuu sana, nataka upate ukuu juu ya
mali zako, nataka sifa zako zivume zidi yao, waambie Bwana amekwisha
kunitangulia Galilaya. Bwana amekwisha kuvuka amewatangulia tayari, yaani
maadui zako umekwisha kuwatangulia mbele. Nakutakia baraka lazima uongozwe na
mtumishi aliyevuka.
NENO LA MUNGU LINATOKA
KATIKA KITABU CHA NABII ISAYA 45:1-7
Haya ndiyo Bwana amwambayo Koreshi masihi wake, ambaye nimeushika mkono
wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake; tunakwenda kutiisha
mwaka 2014, tunakwenda kuyatiisha mataifa yote, yatatiishwa chini ya miguu yetu,
maadui zako watainama chini yako, wewe utawekwa juu asema Bwana wa majeshi.
Nami nitalegeza viuno vya wafalme; Bwana anakwenda kulegeza
vile viuno vya matajiri, ile baraka itaamriwa ije kwako, zitatoka baraka kule
zitakufuata mwana wa Mungu, anasema anakwenda kulegeza vile viuno vya wafalme
ili wewe upate baraka za fedha. Tarajia akaunti zako kwenda kujazwa, huu ni
mwezi Adari, mwezi wa kwenda kupigwa maadui zetu, wanaozuia riziki zetu.
Ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa, nitakwenda
mbele yako, na kupasawazisha mahali malipoparuza; Bwana anakwenda
kulegeza vile viuno vya wafalme atayafungua malango mbele yako, sasa baraka
zinakwenda kufunguliwa, unakwenda kuvuka ukiwa na baraka. Yamkini watu
wamekwaruza maisha yako, wamekuchafua jina lako, lazima utakasike.
Nitavunja vipande vipande; anasema Bwana asubuhi ya leo,
anakwenda kuvunja vipande vipande, yamkini milango ya shaba inakuzuia,
umemaliza mwaka hujapata ajira, leo mimi nakwenda kuvunja vipande vipande
malango ya chuma. Yamkini mama mwaka unakwisha hujapokea mimba yapo malango ya
chuma yamezuia, leo mimi kwa jina la Bwana, ninavunja vipande vipande hayo
malango ya chuma, tena nakwenda kulegeza vile viuno vya wafalme wataleta baraka
kwako.
Watakupandisha cheo, viuno vyao vitalegezwa, bosi wako
utashangaa anakuita vizuri, yamkini wamesema maneno mengi juu yako, ya
kukugombanisha na bosi wako ili ufukuzwe kazi, watakuona unatangazwa kuwa
Mkurugenzi kwao. Wakakuwa chini yako, wewe ndio utapewa safari za kwenda
mikoani, waliochonga juu yako Bwana atafanya mapinduzi, pokea baraka.
Na kukatakata mapingo ya chuma; nami nakwenda kukatakata
mapingo ya chuma, yamkini kuna mapingo ya chuma, yanayozuia muujiza wako,
yamezuia biashara zako, yamezuia amani ya ndoa yako, yamezuia mahusiano yako na
mume wako, hayo mapingo ya chuma leo ninakwenda kuyakata. Nimepewa msimeno,
mkasi wa moto ninakwenda kukata hayo mapingo ya chuma, yanayozuia muujiza wako,
usipate safari za kwenda Ulaya, usifanikiwe, usipate amani, usipate kazi,
biashara zako zisiende. Kabla hatujamaliza mwaka ninayakata hayo mapingo ya
chuma, nataka uvuke ukiwa mwepesi kwa jina la Yesu, pokea baraka Bwana akuvushe
ukiwa na baraka.
Nami nitakupa hazina za gizani; nataka nikupe hazina za gizani
Mtanzania, na zile mali zilizofichwa mahalia pa siri, umaskini sio mpango wa
Mungu, kukosa pesa sio mpango wa Mungu, kuwa omba omba sio mpango wa Mungu.
Sasa Bwana anakwenda kuziinamisha hizi mbingu, anakwenda kutikisa, nataka Bwana
akutendee, mapingo ya chuma yanakwenda kukatwa. Anasema mimi Bwana nitakupa
zile hazina za gizani, ili upate kujua mimi ni Bwana niliye kuita kwa jina lako.
Watu wanasema wametendewa, kwa nini wewe haujatendewa? Kama
hujatendewa labda ulisema vibaya juu ya mtumishi wa Mungu, unaambiwa hiogope
Roho ya agano na huieshimu. Nilisha samehewa dhambi zote na Bwana, leo asubuhi
nilikuwa nawaambia watumishi usicheze na mwenye agano, na wala usijilinganishe
naye. Hata wewe unasesikia maneno, maneno hufuata sehemu palipo na kidonda,
kunakuwa na connection ya mashetani kwako, ndio maana maneno yanapitia kwako,
yanakuja Kanisani.
Hebu funga kata hizo nyaya, funga milango na madirisha, zuia
maneno mabaya, kwanini wakuletee wewe maneno mabaya, kataa. Ukiona watu
wanakuletea umbeya ujue na wewe unahasili ya umbea, kataa tena kata zile kamba,
mwambie mimi siitaji niambie ya Yesu. Maneno yanavunja moyo ukiwa huna imani
unavunjika, kuna watu hawana misingi ya imani, akisikia neno anavunjika. Kaa
tayari masaa yote ukimtazama Yesu aliye juu, ukimuangalia Mungu aliye mwema,
tazama matendo makuu, Mungu atembei na wenye dhambi.
MWISHO
Tupo Mbezi Salasala shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na Uliza kanisa la Nabii Flora
MWISHO
Tupo Mbezi Salasala shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na Uliza kanisa la Nabii Flora
www.nabiiflora.blogspot.com
Picha na RUMAFRICA
Picha na RUMAFRICA
Comments