RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CLAUDY P. MWAKALASYA ANAYEFUATA NYAYO ZA BONY MWAITEGE AACHIA VIDEO YAKE.

Hakika kila jambo na wakati wake. Leo hii Claudy P. Mwakalasya kutoka katika hali ya kuwa dancer wa mwimbaji maarufu sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Bony Mwaitege ameweza kusimama peke yake na kutoa albamu yake ya UPENDO WA MASIKINI. Jamani mimi sifanyi kazi ya kumpromoti huu mwaimbaji ila nyimbo zake na ujumbe wake katika video hii unajipromoti wenyewe. Mungu ni mwema sana kwa walio wake na wenye nia ya kutimiza ndoto zao kwa kijibidiisha kama huyu mtumishi wa Mungu Claudy P. Mwakalasya

Claudy P. Mwakalasya

Nimeamini lile Neno linalosemwa na walio wengi kutoka katika kitabu kitakatifu ya kwamba, wewe hata usipomsifu Mungu wako, basi Mungu anweza kutumia hata mawe kumsifu. Sana naomba tuone kazi ya Claudy P. Mwakalasya katika clip hii,

Unaweza kuwasilina naye kwa simu +255 756 573 788 au +255 712 616 112

Comments