RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NENO LA MUNGU LA JUMAPILI 29.01.2013 KUTOKA KWA MUNGU KWA KUPITIA MTUMISHI WAKE NABII FLORA NI SIZE YAKO NA LINAKUFAA WEWE..SOMA SASA.

MAHUBIRI YA TAREHE 29 12 2013
Nakusalimu Mtanzania mwenzangu unayenitazama popote pale ulipo, na unayenitazama kwenye youtube na kunisoma kwenye blogu na facebook, najua kuna watu wananitazama live, tunawakaribisha sana katika kipindi cha neno la Mungu.  Katika siku ya leo tarehe 29 mwezi Adari, yaani mwezi wa 12 mwaka 2013. NITAKUWA NA UJUMBE KATIKA  WAFALME WA PILI 4:8-17
UJUMBE UNATOKA KATIKA KITABU CHA 2WAFALME 4:8-17
Hata siku moja Elisha alikwenda shuleni, na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo, naye akamshurtisha aje kwake apate chakula. Ikawa kila alipopita njia ile; leo nataka kibali kwa wenye vyeo, jaribu kumshurikisha mtumishi wa Mungu apite kwako apate kula chakula.

Nataka leo kabla hujamaliza mwaka, mshurtishe Nabii aingie kwako ili uweze kubarikiwa, alikuwa akifanya hivyo yule mwanamke mshimemo, kila ikifika mwisho wa mwezi anamshurikisha Nabii ili aweze kula chakula. Nataka leo kabla hujamaliza mwaka, mshurutishe Nabii aingie kwako apate kula chakula.
Ikawa alipokuwa kila akipita katika njia ile kula chakula, yule mwananmke akamwambia mumewe, kwamba mimi ninaona mtu huyu akipita kwetu mara kwa mara ni mtakatfu wa Mungu.  Nakuomba tumfanyie chumba kidogo ukutani; yaani huyu mtu ambaye anapita kwetu mara kwa mara, nimegundua mimi kama mama wa familia, mwanamke muombaji kwamba huyu mtu ni mtakatifu wa Mungu.
Mama akiisimamia vizuri nyumba yake, itakuwa nyumba yenye amani. Baba ni kichwa cha nyumba na mama naye ni msimamizi wa nyumba. Na akina mama ndio wa kwanza kuona kasoro katika familia, kwa sababu ndio wanaolinda familia. Na ndio maana huyu mwanamke mshimemo aligundua akamwambia baba, huyu mtu anayepita kwetu mara kwa mara nimeona ni mtakatifu.
Na ndani yake tumuwekee kitanda, na meza na kiti; maana ya chumba ni moyo wako, leo nataka uandae moyo wako, meza na kiti, uweke na taa ndani ya nyumba yako ili mfalme wa utukufu apate kuweka makao. Maana ya kitanda ni imani, nataka imani ikae ndani ya nyumba yetu, ukisikia godoro ni mafundisho. Mwekee Yesu kiti ndani ya nyumba yako, hebu washa taa ndani ya nyumba yako ili mafanikio yako yasikome katika nyumba yako. Na ili nyumba yako iwe na mawasiliano lazima uwe na dishi, ili uweze kukamata vitu mbali mbali.
Ikawa siku moja akafika huko, akaingia katika chumba kile akalala, akamwambia Jehazi mtumishi wake, akamwambia akamwite yule mshimemo. Naye alipokuwa amekwisha kuitwa, akasimama mbele yake, akamwambia “sema naye sasa” tazama wewe umetutunza namna hii, utendewe nini basi?
Wewe mama, baba mkazi wa Dar es salaam, na mtu unayeabudu katika Kanisa la Yesu Kristo, umejifunza mambo mengi sana mwaka huu, umepanda miguuni kwangu, umechangia ujenzi wa Kanisa, umetuvisha mavazi mazuri, umetununulia soda, maji tumekunywa, umetufanyia mengi sana mwana wa Mungu, umetenda kwa mwaka huu vitu vingi. Umechangia bili ya maji, ninatoa bahasha kila siku unakuwa mwaminifu, sasa leo unataka nikufanyie nini? Nami nakuuliza msikilizaji wangu, wewe uliyejitoa kwa mwaka mzima, unataka leo Mungu wangu akutendee nini basi. Umetoa michango, fungu la kumi umekuwa mwaminifu.
Je uombewe kibali kwa Mfalme, yule mwanamke akamjibu “mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe; sasa mimi nina ujumbe kwako wewe unayenisikiliza hapa Kanisani, mwana wa Mungu, wachungaji kwa wazee wa Kanisa, mme kuwa ni mimi kwa mwaka mzima, sasa mnataka Mungu wangu awatendee nini? Unataka nikutendee nini Rulea Sanga, umekuwa ukinirusha kwenye blogu na facebook, watu wengi wamepona, Bwana anasema akutendee nini. Kabla ya jua kuzama Bwana akutendee nini maana umekuwa mwaminifu mbele zangu.
Elisha akasema basi atendewe nini? Jehazi akajibu “hakika mtu huyu hana Bwana na mumewe ni mzee”, akamwambia kamuite. Naye alipokwisha kuitwa; ikiwa mwaka mzima umefanya kazi ya Bwana, Mungu wangu anauliza akutendee nini leo, huu ni mwezi wa kutendewa, leo ni siku ya mwanamke mshimemo kutendewa. Umekuwa na mimi bega kwa bega hukukosa Kanisani hata siku moja, Bwana akutendee nini kwako?
Kama ni baraka zitakufuata, kama ni mume atakuja, useme chochote Bwana wangu yupo tayari kukutendea leo. Kama ni maisha marefu utayapata leo, maana umekuwa ukipanda miguuni kwa Nabii, mmetubariki kwa mwaka mzima, leo tuwatendee kitu gani? Naachilia wingi wa miaka juu yenu, naachilia wingi wa majibu, pesa, ulinzi juu yenu, maisha marefu yashuke ndani ya watu hawa, unastahili kutendewa. 
Hata kama mchungaji alikukwaza achilia hilo jiwe, nikufanyie nini Mtanzania, maana umejitoa kumwabudu Mungu mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka. Pokea kutendewa, maisha yako yawe mazuri, nakutamkia baraka, amani na upendo, mshikamano na umoja. Haijalishi mumeo ni mzee, maisha yako yamechoka, Bwana anakwenda kuyachipua upya, yatakuwa kama kijana. Haijalishi hujapata mtoto, unakwenda kupata mtoto asema Bwana wa majeshi, haijalishi ni mzee na mbegu zimezeeka Bwana ataachilia uzao, katika kiuno cha mume wako, na wewe utapokea mtoto. Nakutamkia baraka, mafanikio.
Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni, Elisha akasema “panapo majira kama haya mwakani utamkumbatia mwana” nami nasema panapo mwakani majira kama haya utaamia kwenye nyumba yako, utakuwa na maduka ya jumla, utaitwa mbarikiwa, pokea ulinzi katika maisha yako. Panapo majira kama haya nakutamkia utahesabu faida juu ya maisha yako, watakuuliza mbona unazidi kuwa kijana, Yesu anakutendea leo.
Panapo majira kama haya utakuwa na mume wako kibindono, upako wako utaonezeka, nyumba yako itakuwa na baraka, watoto wako wataoa, mabinti wataolewa wote. Panapo majira kama haya binti utakuwa na kazi nzuri, haijalishi hujulikani utaitwa jina lako ikulu, nasema panapo majira kama haya Yesu anakwenda kubadilisha maisha yako, kuanzia leo maisha yako yanakwenda kubadilika.
Yule mwanamke akasema la! Bwana wangu, wewe ni mtu wa Mungu; kumbuka wewe ni mtu wa Mungu usiseme uongo, hata leo nikiwatamkia baraka hapa wanasema Nabii  amenitamkia mtoto mbona sijampata,  Nabii amesema nitaolewa leo tarehe 29 mbona hakuna cha mwanaume wala kinachoendelea. Wewe amini ondoa mashaka kama mwanamke mshimemo, neno lim eshuka litakuwa, kamata neno tembea katika mtandao wa neno la Mungu. Tembea na tamko la Nabii, Nabii akitamka lazima uinuliwe, kwa sababu ametamka wewe yakamate maneno, yafunge alafu yaweke moyoni mwako, alafu uandike terehe
Ukiamka asubuhi sema Mungu asante kwa sababu umenipa mume, unamwambia Bwana nimekwisha kutabiriwa sasa nafanya mazoezi ya kufunga ndoa. Kuwa na imani kama mwanamke mshimemo, alikuwa na mashaka lakini Elisha alimwambia panapo majira kama haya utakuwa na mtoto.

Kuna watu hawaamini mpaka leo, hamini neno hili sasa unakwenda kufunga ndoa, pokea kibali hicho, hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mwanadamu tunacheleweshaga majibu wenyewe, mashaka tu, ukiwa na mashaka jibu lako unalichelewesha, unatakiwa kuwa na imani, imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo tena bayana ya yale yasiyoonekana.
Yule mwanamke akachukuwa mimba akazaa mtoto mume, wakati huohuo mwakani; japokuwa alipata mashaka mwanamke mshimemo, akamwambia Nabii kumbuka wewe ni mtu wa Mungu, tena wewe ni mtakatifu Nabii wa Bwana, kwa nini unaongea uongo.

Kuna watu wanamashaka, wanasema Nabii Flora umetabiri mambo mengi juu yetu mbona hatujaona? Mama weka vizuri laini yako wacha kuichezesha, yaani maana yake joto la kiroho lisipungue ndani yako. Na uhakikishe simu yako inasalio, yaani maana yake maombi yawe ndani mwako, na imani ya kumwamini mtumishi wa Mungu.    

MWISHO

JINSI YA KUFIKA IBADANI
Panda magari ya Tegeta kama unatokea Mwenge, Shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora    

Tembelea
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
Facebook: Nabii Flora Peter

Picha na uandishi ni RUMAFRICA +255 715851523

Comments