RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHETANI AKISHAKUTUMIA BAADAE ANAKUABISHA MBELE ZA WATU KAMA HUYU BIBI ANAYESADIKIKA KUWA NI MCHAWI AMEKUTWA CHUMBANI KWA MTU MJINI BUKOBA


Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya leo Ijumaa Januari 31,2014
  Bi. Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba. Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni mchawi wakati wengine wakisema wasubili taarifa ya Polisi.



Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.

Wakielekea kituo cha cha polisi cha Bukoba Mjini leo asubuhi.

Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba

PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG

Comments