RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA ZA KUJENGA IMANI YAKO KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER


 ENOCK NA MKE WAKE WAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MTOTO NA MALEZI MEMA KUTOKA KWA NABII FLORA. USHUHUDA WA 20.01.2014

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Enock; mimi Nabii Flora aliniokota kama chokoraa, nilifukuzwa katika
Makanisa mengi, lakini baada ya kufika kwa Nabii Flora akanipokea, sina mengi ya kuongea zaidi ya kumshukuru sana Nabii Flora. Mungu amemjaza sana Nabii Flora upendo wa dhati, kama sio yeye hata nisingekuwa nimesimama hapa. Nabii Flora; kweli kabisa mtu ni mtu mpende kama alivyo, mbegu ya Mungu ni ya Mungu tu, hata ingekuwaje ikimwagiliwa maji lazima itachipuka tu.
Unajua wanadamu wengi wanatazama hapa, hawaangalii mbele, lakini uzuri wa Mungu huwa anaangalia mbele. Hawawezi kujua maisha ya kesho kutwa ya mtu yule yatakuwaje, mimi namshukuru Mungu kwa hilo sijisifu, Mungu amenipa upendo.

JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kama unatokewa Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na uliza kanisa la Nabii Flora Peter
Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

Comments