MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA TANZANIA DAVID ROBERT ASUMBUA VICHWA VYA WATANZANIA AKIWA NJE YA NCHI
David Robert ambaye inasemekana yuko nje ya nchi ya Tanzania amekuwa
akisumbua vichwa vya watu kutokana na picha zake ambazo amekuwa
akiziposti katika facebook account yake zikionyesha mazingira ya Ulaya.
Picha zake zote anazoposti anaandika kuwa yuko Mbeya Tanzania, maeneo ya
Kiwira, Tukuyu mara Mwanjelwa na maeneo mbalimbali ya Mbeya.
David Robert
David Robert kwa kabila ni Mnyakyusa na mara nyingi hupenda sana kuongea
Kinyakyusa hasa anapokutana na Mnyakyusa mwenzake. Na amekuwa akipenda
sana kabila lake na mji aliotoka. Kutokana na hivyo, amekuwa akiendelea
kuipaisha Mbeya kwa kupiga picha akiwa nje ya Tanzania na kusema yuko
Mbeya.
Nasi tunamuombea Mungu azidi kufanya mema huko Mbeya Ulaya ili
atakapotua Dar basi watu wa Bongo tufaidike matoki (ndizi) za Mbeya.
David Robert kwa wanaomjua ni mtu wa utani sana, na ndiyo maana hata
aliko huko bado anafanya jox kuwafurahisha wadau wake. Ninaamini ipo
siku atafunguka na kusema siri aliyoificha.
BAADA YA MIZUNGUKO YA SIKU NZIMA, MTUMISHI WA MUNGU AKIWA ANAJIPUMZISHA
David Robert
Comments