RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SANAMU YA BIKIRA MARIA INAYOTOKWA MAFUTA YAVUTA MAMIA NCHINI ISRAELI

  Sanamu ya bikira Maria ikiwa inatoa machozi ya mafuta nyumbani kwa Osama na Amira nchini Israel ©visionofjesuschrist.

Mamia ya waumini kutoka viunga mbalimbali vya nchi ya Israel wanamiminika katika mji mdogo wa Tarshiha wa nchi hiyo ambao upo kwenye mpaka na Lebanon ili kujionea sanamu ya bikira Mariam ambayo inadaiwa ilizungumza huku pia ikitokwa na machozi ya mafuta ambayo licha ya kufutwa bado sehemu ya sanamu hiyo zilionyesha mng'ao.

Sanamu hiyo inayomilikiwa na wanandoa Osama na Amira Khoury. Ambapo kwa mujibu wa Amira amesema aligundua sanamu hiyo ndogo kugubikwa na mafuta na kumwambia mwanamke huyo asiogope "don't be afraid". Jirani ya wanandoa hao alikuwa wa kwanza kugundua machozi ya mafuta machoni mwa sanamu hiyo ya bikira Mariam, inadaiwa watu 2000 wamesafiri kwenda kuiona sanamu hiyo ambayo imezungushiwa rozali mwili mzima, wanandoa hao wameruhusu watu kuitazama.

Kwa mujibu wa mume wa Amira bwana Osama ameiambia Sky News kwamba mke wake aliisogelea karibu sanamu hiyo na kugundua ilikuwa imefunikwa kwa mafuta na kuamua kuyafuta mafuta hayo akiwa anaogopa, anasema aliamua kumwita jirani yao ambaye alifika na kugundua yalikuwa mafuta kweli mwilini mwa sanamu huyo na kumshika mikono Amira na kumtaka kutoogopa kwakuwa hizo ni baraka zimeingia nyumbani kwake. Kwa upande wake Amira amesema kitendo cha kuona sanamu hiyo inatokwa mafuta kimemfanya awe mtu wa maombi kwakuwa ni kitu cha ajabu

Source: Gospel Kitaa
Link:

Comments