RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MESS JACOB CHENGULA AMPONGEZA ROSE MUHANDO KWA TAMASHA LA UPENDO

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Mess Jacob Chengula anayejulikana kwa albamu yake ya MUNGU HABADILIKI amempongeza sana malkia wa nyimbo za Injili Tanzania Rose Muhando mkazi wa Dodoma kwa uamuzi alioufanya wa kusaidia watoto yatima wa kituo cha HOCET kilichopo Kimara. Alisema huu ni moyo wa Agape na unahitajika sana kuigwa na kila mtu.

Mungu anavyokubariki kwa kidogo yakupasa kula na yule ambaye ohajabahatika kwa wakati huo kubarikiwa kama yeye. Sio muda kuwa mchoyo na baraka za Mungu. Kumbuka Mungu mara nyingi humbariki mtu kwa kupitia wanadamu, hata kama kuna njia nyingi Mungu anaweza kumbariki mtu, lakini hii ya kupiti mwanadamu ni mojawapo. Unapompatia yatima kile ulichonacho basi yatima huyu hukushukuru na akisha kukushukuru, milango ya mafanikio inakujia.

Mess aaliwaomba Watanzania kuungana na Rose Muhando katika tamasha hili la UPENDO. Aliwaomba Watanzania wakapokuja katika tamasha hili la kipekee wajaribu kuja na zawadi kwa Yatima.

Comments