Mchungaji Josephat Gwajima.
Biblia inasema, Wakorintho 6:16;
‘...Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye...’
Kuna watu wengi vibali vyao vimeondolewa kwasababu ya kuwa na waume au wake wa kiroho (majini mahaba). Unaweza kujiona unaota ndoto kuwa unafanya mapenzi na mtu mwingine unayemjua au usiyemjua kumbe ndio jini mahaba.
Ni muhimu kujua kuwa, hiyo si ndoto bali ni bayana, Ndoto ni yale mambo ambayo mtu (ambaye ni roho) huyaona wakati mwili ukiwa umelala, hivyo ni bayana kabisa (real). Huyo anayekujia ndotoni ni mume au mke wa kiroho yaani ‘spiritual husband/wife’. Anaweza kuwa jini, joka, mzimu au shetani.
Hivyo basi, unapokutana naye kimwili katika ulimwengu wa roho wewe na huyo jini au pepo, mnafanyika kuwa mwili mmoja kwa maana mmefungishwa ndoa katika ulimwengu wa roho. Hii ni moja ya sababu kubwa ya mtu kukosa kibali mbele za watu na hata mume au mke.
Watu wote walio kwenye ndoa halafu wana waume/wake wa kiroho ndio ambao utawakuta wenye matatizo ya kindoa yasiyoisha, hawawezi kufanikiwa katika maisha hata kama wana akili kiasi gani. Haya majini yanakuja yenyewe. Yanazuia kila maendeleo katika maisha yako, ni mawakala wa kumfanya mtu akose kibali.
Mapepo haya yana nguvu sana kwa sababu kuna agano la ndoa nyuma yake ambalo linawafanya wasumbue maisha ya watu wengi sana. Kwa asili yana wivu hivyo, huleta kutokufanikiwa ili mtu huyu asijekumpata mtu atakayempenda zaidi yao.
KUNA NJIA TATU AMBAZO MAPEPO HAWA HUTUMIA KUINGIA WATU.
1. Kuokota vitu mfano pete au cheni;
Ni muhimu kujua majini ni roho hivyo yana uwezo wa kujibadili maumbo yoyote, hivyo ili apate mtu wa kumwingia hujigeuza kuwa pete. Pete hiyo husimama kama agano la ndoa baina ya mtu na pepo mchafu. Sio lazima iwe pete inaweza ikawa cheni au kidani cha dhahabu, mara utakapovaa hiyo ndio tayari ndoa. Inaweza kuja kupotea au kuibiwa baadaye lakini agano lipo palepale, ndio unakuwa ushaolewa kiroho na jini huyo.
2. Kukutana kimwili na asiye mtu;
Sababu nyingine ni kukutana kimwili na mtu asiyemtu, ni muhimu kujua, majini yana uwezo wa kuvaa mwili na kuwa kama watu. Majini ni malaika (wachafu) (Ufunuo 12:7), kumbuka wale wageni aliowapokea Ibrahimu walikuwa kama watu kabisa lakini walikuwa malaika. Hivyo ukikutana kimwili na jini huyo, pepo wachafu huingia kwako na kuanza kufanya mapenzi nawewe, hali ambayo utakutokea zaidi ndotoni, na wakati mwingine hata ukiwa macho.
3. Uhusiano wa kimapenzi na mtu mwenye majini;
Siku moja nikiwa Japan nikihubiri, kuna binti mmoja anaitwa Masami, maombi yalipopamba moto alianza kuruka na kuparamia miti, tulivyomkamata akaanza kusema kuwa yeye ni mtumishi wa shetani. Anachofanya ni kuwa na mahusiano na watu wakubwa, akilala nao anaachilia vitu vya ajabu ndani yao na hao wanaume wanaenda kuviachilia kwa wake zao au kwa yeyote watakayelala nao, aliendelea kusema kuwa matokea yake watu hao huzaa watoto ambao ama ni walemavu au waliokufa.
KUVUNJA MIKATABA YA NDOA
Ili kuvunja mikataba ya ndoa za kichawi/kishetani ni lazima utamke maneno. Mungu aliumba dunia kwa neno lake hivyo, ili kusimama kinyume na majini au pepo hao unatakiwa utamke maneno katika jina la Yesu.
‘Ninavunja maagano ya ndoa za kishetani/kichawi katika jina la Yesu Kristo, nadhoofisha utawala wa majoka na mashetani katika maisha yako katika Jina la Yesu Kristo uwe huru kabisa!!!
UFUFUO NA UZIMA
Habari inatoka: Gospel Kitaa
Comments