Mchungaji Antony Lusekelo alimaarufu kama Mzee wa Upako, asema kuwa, CCM yashindwa kuenea kwenye viatu walivyo achiwa na muasisi wao Mwl. J.K. Nyerere na badala yake, vinawapwere pweta.
Maneno hayo aliyasema jana katika Ibada takatifu, aliyo iongoza katika kanisa lake lililopo Ubungo Kibangu, jijini Dar es salaam.
Aidha usemi huo uliogeuka kuwa kituko, uliibuka baada ya Mchungaji Lusekelo kutoa tathimini ya kile kinacho endelea ndani ya Taifa hili, ambapo chama tawala ni CCM, juu ya mchakato mzima wa kuitafuta Katiba ya Taifa hili, itakayo tumika kwa miaka 50 mbeleni.
Mabishano yasiyo na sababu, fujo pamoja na hoja dhaifu ndani ya Bunge maalumu la katiba ni kati ya vitu vinavyo mkera Mchungaji huyu, huku akisisitiza kuwa; Wabunge waliopo kwenye Bunge lile maalumu, hawapaswi kabisa kumsakama Jaji Warioba, kwani hoja zinazoendelea katika vikao vyao, nyingi ni dhaifu na abadani haziwezi fananishwa na hoja alizozitoa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya marekebisho ya Katiba alimaarufu kama 'Tume ya Warioba', hususani juu ya suala la Muungano.
Kwasasa Mchungaji huyu amezidi kufahamika sana ndani na nje ya Taifa letu, kutokana na kipaji na uwezo wa kutengeneza nguvu za kuwasaidia binadamu alizo nazo.
Source: Bongo Frag
Comments