RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ADELITA MSHUMBA ANOGESHA HARUSI YA BURTON ELENEST NA ELENEST JONATHAN USIKU WA LEO

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Morogoro, Adelita Mshumba siku ya leo amekuwa dhahabu kwa walio wengi hasa pale alipoonyesha kwa jamii kile ambacho Mungu amemzawadia kwa uimbaji wake.


Adelita Mshumba alionekana kukonga mioyo ya watu wengi hasa alipoimba wimbo wake wa amani mchana ya leo katika kanisa la Tabata Kuu Luthelani hapa jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Prince Kristo Mfalme.

Watu walionekana wakiwa katika ulimwengu mwingine wa kiroho kutoka na ujumbe aliokuwa akiuachia mahali hapo. Hakika watu walibarikiwa sana na uimbaji wake na wengine kutamani azidi kuimba. Hii ina maanisha ya kwamba Mungu ni Mungu wa kusifiwa na kuimbiwa nyimbo zenye utukufu kwa Mungu na zenye kuwaleta watu kwa Bwana wetu Yesu Kristo


Mwimbaji huyu akiongea na Rumafrica amesema yuko tayari kufanya kazi ya Bwana mahali popote na wakati wowote. Kwahiyo kama wewe ungetamani kuwasiliana naye basi unaweza kumpigia kwa simu hii +255 715  540 283
Pia Mungu amemuinua huyu muuimbaji ambaye hapo mwanzo alikuwa akiimba nyimbo za kidunia na alikuwa mlevi sana kama alivyoongea na Rumafrica siku ya jana. Amesema sasa ameamua kumtumikia Mungu kwani amemuokoa na mengi sana na amebadilisha maisha yake. Hivi sasa amefanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza inayoenda kwa jima la KILICHOBAKI NI MAOMBI yenye nyimbo nane.


Comments