RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BREAKING NEWS: MWIGIZAJI WA FILAMU RACHEL HAULE AFARIKI DUNIA NA MWANAE




Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia. Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae

RACHEL HAULE AKIWA MJAMZITO HIVI KARIBUNI

Rumafrica itazidi kuwapa taarifa hizi
Marehemu Rachel Haule


FILAMU ALIZOSHIRIKINA NA ODAMA KWA MARA YA MWISHO
Hizi ni filamu alizocheza kwa mara ya mwisho na rafiki akishirikiana na ODAMA. Rumafrica ilihusika sana katika upigaji wa picha wakati wa maandalizi ya filamu hizi. Rumafrica imepigwa sana na kifo chake kwani ilikuwa karibu sana na Rachel Haule, mbali na uigizaji pia alikuwa mshauri mzuri Rumafrica.



HII NI MOJA YA PICHA AMBAYO RUMAFRICA ILIMPIGA MAREHEMU RACHEL WAKATI WA UZINDUZI WA FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU MAENEO YA MLIMAN CITY
nakumbuka Rachel aliniomba sana nimpige picha, na mimi nikaamua kumpiga na baada ya kumpiga nakumbuka alinishukuru sana huku akionyesha ku-appreciate kazi yangu ya upigaji picha. Rachel Haule alikuwa ni mcheshi sana na mwenye kupenda watu hasa pale unapoomba ushauri. Nakumbuaka siku nampiga picha hii alisema, "Rulea natamani siku moja unipeleke kanisani kwako" alivyoniambia hivyo nilidhani ananitania tu kutokana na utani wake.
MUNGU AMULAZE MAHALI PEMA PEPONI

Comments