Bwana Yesu asifiwe! Ujumbe huu umekufikia kwa kusudi kabisa na ninaamini Mungu atakusaidia na utatoka hatua moja kwenda nyingine. Hebu chukua nafasi twende tujifunze pamoja na ni maombi yangu kwamba Mungu akufunulie akili zako ili uelewe kile ambacho anakwenda kutufundisha!
Kabla ya yote ni muhimu ufahamu kwanza juu ya imani maana tunachojifunza hapa ni jinsi ya kuitumia imani kama ngao wakati shetani atakapokutupia mishale yake yenye moto.
Biblia inasema,”1 Basi imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (ebr.11:1)
Sikiliza tafsiri nyingine kutoka katika Kiswahili cha kisasa biblia inasema hivi,“kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayoyatumainia Kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona”

Kwa hiyo kuwa na IMANI ni kuwa na HAKIKA ya mambo uanayoyatarajia au unayoyatumainia. Kwa maana hiyo imani ni sasa hata kama kitu unachotarajia hakipo imani inabaki kuwa sasa, imani inaleta mambo unayoyatarajia kuwa halisi hata kama hujakiona kile kitu! Kitu kingine unachopaswa kujua ni chanzo cha imani na unisikilize hapa nikwambie kitu, kila imani chanzo chake ni kusikia haijalishi ni imani ya kimungu au la zote chanzo chake ni kusikia! Angalia Biblia yako katika kitabu cha warumi 10:17, “17 Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia Huja kwa neno la Kristo”
Kwa nini nataka uelewe chanzo cha imani? Ni kwa sababu watu wengi sana wamekuwa wakiomba kwa Mungu ili waweze kuwa na imani na wengine wamejaribu hata kufunga wakiomba imani, sikiliza ndugu yangu! Imani chanzo chake ni kusikia na si kusikia tu bali kusikia kunakotokana na neno la Kristo, kwa hiyo kama imani chanzo chake ni kusikia kunakotokana na neno la Kristo basi huwezi kuwa na imani kama huna neno la Kristo! Nimesema hivi huwezi kuwa na imani kama hauna neno la kristo! Ndiyo, ni lazima uwe na neno la Kristo ambalo kwa hilo utaamini kile unachoamini! Imani lazima iwe na kitu cha kushikilia huwezi ukaamini kitu from no where lazima uwe na kitu kinachokufanya ushikilie hicho unachoamini na hicho kitu kinaitwa neno la kristo au neno la Mungu (haleluya!) Ngoja twende kwa mifano utanielewa tu,angalia rumi 4:17-21 inasema hivi,
“17 Kama ilivyoandikwa,nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi;mbele zake yeye aliyemwamini, Yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu,ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa,ili apate kuwa baba wa mataifa mengi,kama ilivyonenwa,ndivyo utakavyokuwa uzao wako.19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani,alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwishakufa,(akiwa amekwishakupata umri wa miaka mia),na hali ya kufaya tumbo lake sara. 20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwaimani,akimtukuza Mungu;21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi”.
Nitafafanua vizuri hii habari huko mbele lakini nachotaka uone hapo ni hiki chanzo cha imani ni kusikia neno na kama ni hivyo chanzo cha imani ni neno la Mungu na utaona kwenye habari hiyo hapo juu ibrahimu alikuwa na miaka mia na mpaka anafikisha miaka mia hakuwa na mtoto lakini kama ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kuna maneno aliyatamka Mungu kwa ibrahimu huko nyuma kuhusu mtoto na biblia inasema Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kuwa ni haki kwake. Ilipita miaka mingi na ibrahimu hakuwa na mtoto kwa hiyo kama mwanadamu alianza kufikiri hali ya mwili wake(uzee alionao maana alishafikisha miaka mia) akafikiria na hali ya kufa kwa tumbo la mkewe sara maana kibinadamu sara hakuwa na uwezo wa kubeba mimba tena, lakini akiiona AHADI ya MUNGU, hakusita kwa kutokuamini bali ALITIWA NGUVU kwa imani……….. sikiliza! hapo anaposema akiiona ahadi ya Mungu umeshawahi kujiuliza ni ahadi gani hiyo? Na anaposema alitiwa nguvu umeshajiuliza alitiwa nguvu na kitu gani? Sikia ahadi aliyokuwa akiiona Ibrahim ilikuwa ni NENO ambalo Mungu alimuahidi huko nyuma na kwa neno hilo imani ya Ibrahim ilijengwa hapo,(kumbuka nataka uelewe chanzo cha imani ili uache kufunga na kuomba imani)! Na kwasababu neno hilo ambalo imani ya Ibrahim ilijengwa hapo ndilo lilikuwa likimpa Ibrahim nguvu ya kuendelea kuamini japokuwa uzee ulikuwa umemlemea na hali ya kufa kwa tumbo la mkewe Sara ilikuwa inamzonga lakini akiiona ahadi ya Mungu (neno) hakusita kwa kutokuamini bali alitiwa nguvu! (haleluya!)
Biblia inasema imani huja kwa kusikia wala haijasema imani huja kwa kufunga na kuomba na hata ukiomba upewe imani Mungu atakupeleka kwenye neno lake tu ambalo ndiyo chanzo cha imani. Angalia mfano huu labda tutamalizia hapa kwa habari ya chanzo cha imani, luka 17:5,6 inasema hivi,
“5 mitume wakamwambia Bwana, tuongezee imani. 6 Bwana akasema,kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali,mngeuambia mkuyu huu,ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii”.
Unaona kitu ambacho mitume walikuwa wanaomba! Walikuwa wanaomba waongezewe imani lakini kumbe hata hiyo imani yenyewe amabayo wao walitaka waongezewe hawakuwa nayo hata kidogo! Ndo maana unaona Bwana anawaambia kama wangekuwa hata na hiyo imani ya kiasi cha chembe ya haradali wangeuambia mkuyu ng’oka ukapandwe baharini nao ungewatii, mi sijui kama unaelewa alichokuwa anamaanisha Bwana lakini kama unaisoma Biblia kwa kuitafakari mistari yake utagundua alichomaanisha Bwana ni kwamba imani ina chanzo chake ni kama mwanzo wa mti ambapo kwanza huanza mbegu ndogo sana lakini unapoipanda inakua na kuwa mti mkubwa sana. Kitu ni kilekile ukirudi kwenye somo tunalojifunza ni kwamba kama unataka kuwa na imani ni lazima uwe na mbegu ambayo ukiipanda itaota na kukua nakukufaya uwe na imani kubwa sana na hiyo mbegu ni neno la Mungu! Angalia kitabu cha luka 8:11 inasema, “11 Na huo mfano,maana yake ni hii
MBEGU ni NENO la MUNGU”

Comments