Hapa duniani Mungu amegawa karama na majukumu ya kumtumikia kwa kila
mtu, hakuna mtu atakayesema yeye hana jambo la kufanya kwaajili ya
Mungu. Madam Ruti ametambua wajibu wake hapa duniani na kutambua kile
Mungu ameweka ndani yake. Baada ya kutambua aliamua kukifanyia kazi,
Mungu alimuwezesha kufanya albamu yake ya JANA IMEPITA. Siku ya Jumapili
25.05.2014 katika uzinduzi wa albamu ya Mercy Kitundu aliweza kumtukuza
Mungu na kumwimbia kwa furaha na shangwe, na hii ilisababisha watu
wengi kumuunga mkono kwa kumshangilia kutokana na uimbaji wake na ujumbe
aliobeba kwa kupitia wimbo wake wa JANA IMEPITA. Madam Ruti ambaye
aliweza kuhudhuria ibada ya asubuhi ya Jumapili katika kanisa la KKKT
Mbagala Zakiem kwa lengo zima la kumuunga mkono mwimbaji mwenzake.
Madam Ruti
Huu ni upendo wa ajabu sana amabao Madam Ruti anaonyesha kwa waimbaji
wenzake kuiga. Kazi ya Mungu inahitaji ushirikiano na sio kuwa mwimbaji
ambaye unatamani sana pesa na ukasahau uko katika kazi ya kumtumikia
Mungu. Tuache wazo la kutamani fedha bali tumtangulize Mungu kwanza na
Mungu atatubariki kwa njia nyingine na sio kwa kutegemea muziki kuwa
chanzo cjha mapato yako. Kazi ya MUNGU sio biashara. Tunatambua ya
kwamba unatumia pesa nyingi kurekodi studio, lakini muombe Mungu afungue
milango katika kazi zako zingine ili yubarikiwe na uzidi kufanya kazi
ya Mungu.
Rumafrica inalkupongeza sana Madam Ruti kwa moyo wako huo na endelea
kufanya kazi ya Mungu na Mungu atazidi kukubariki na kukufikisha pale
unapotamani kufika.

Kulia ni Madam Ruti na Bahati Bukuku
Madam Ruti akifanya yake kumtukuza Mungu wetu







Comments