MWINJILISTI DANIEL SAFARI AELEZEA MAISHA YAKE JINSI ALIVYOKUWA AKIISHI KAMA CHOKORAA HAPA BONGO BAADA YA KUSUSIWA NA WACHUNGAJI WAKE MBEYA NA PIA UJIO WA ALBAMU YAKE YA TATU
Mwinjilisti Daniel Safari ni mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye aliweza kufanikiwa kutoa moja ya albamu yake iliyompa na jina la SAFARI ambaye ilikuwa ikienda kwa jina la SAFARI. Daniel Safari aliweza kutembelea ofisi ya Rumafrica kufanya mahojiano katika kipindi cha RUMAFRICA Online TV kuhusina na ujio wa albamu yake ya tatu ya MWANADAMU NI MWANADAMU. Alisema, albamu yake ni tofauti kabisa na albamu zake zote kutokana na ujumbe aliyoambiwa na Mungu aulete kwako wewe. Pia kuna baadhi ya nyimbo ameweza kuelezea maisha yake na mapito aliyopitia
BAADHI YA MAPITO ALIYOPITIA MWIMBAJI DANIEL SAFARI
ONE: Kuishi maisha ya uchokora hapa jijini Dar es Salaama baada ya kushindwa kupata nauli ya kurudi kwao Mbeya
TWO: Ndoa yake kuteteleka kutokana na maneno ya adui zake kwamba sasa amekuwa chokoraa
THREE: Kushindia uji wa chumvi yeye na mke wake baada ya kumleta Dar es Salaam na kulala katika kitanda cha miti chenye miguu ya matofali
FOUR: Kutembea kwa mguu kutoka Gongo la Mboto mpaka Kariakoo kutafuta riziki
FIVE: Wachungaji wake kumtangazia kuwa maisha yake ni ya taabu na ni chokoraa mjini
SIX: Jinsi Mungu alivyomuinua kwa kupitia Mchungaji Mwasasu na mpaka sasa anaitwa Daniel Safari na ni mjasiliamali. Famili yake iko salama mikononi mwa Yesu Kristo
SEVEN: Sababu ya kuiita jina lake DANIEL SFARI, Kwanini aliita jina la SARAFI
EIGHT: Ujio wa albamu yake mpya MWANADAMU NI MWANADAMU
KUNA MAMBO MENGI KAZUNGUMZIA. KARIBU SANA NAMSIKILIZE
Comments