RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NGUO ZANGU NI CHUKIZO MBELE ZA MUNGU? NISAIDIENI

Rumafrica leo inataka kukaa chemba na wewe mdau ili tutete kuhusiana na mavazi sahihi ya mkristo kuvaa kanisani na mahali popote. Katika picha zangu hapo chini nimeona tujadili na wewe unayependa kupendeza, Je, hayo mavazi ni sahihi kuvaliwa kwa Mkristo? Nimejaribu kuchungulia baadhi ya haya mavazi nikagundua jambo, nimeona mavazi mengine yako poa sana hata ibadani ila mengine ni balaa. Kuna mavazi yanayoonysha mwili wako yaani mavazi yanayobana.

Mavazi kama haya ya kubana yamekuwa yakivaliwa sana na watu wengi (waliokoka na wasio okoka). Wengine ni watumishi wa Mungu wanavaa hata madhabahuni bial hata hofu ya Mungu. Waumini wenye imani haba wamekuwa wakitokwa na udenda wa mate wakitamani kuona mwili wa mtumishi ulivyobanwa na mavazi yake, na hii imesababisha waumini wengine kutoka ibadani wakiwa hawaja "gain" chochote madhabahini, mawazo yao yamejaa fikra potovu na hata lkusababisha wengine kuwachokoza watumishi kwa kuwatamani na kuwalaghai kwa mali zao.


Wanaume nao wamebadilika siku hizi, nao wanatamani sana kuonysha mapaja yao kwa kuvaa visuali vilivyobana sana na wanaonekana kama vikatuni. Na cha kushangaza ni pale wanaume wanavyoweza kulegeza suruali zao na kuvalia makalioni bila ya haya.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrHVyXKWeUZkAwQpNYWQPHlvEQwpUI33shjKWNA0AUGXwZi1rMzC4a4jYBz7WN7FnCQO4BpfLxA8jSPzoC9HWekOgmJlScx35mJogKuXey_qc_a3TFtSryxLO5W_-4gOa-NRCUpXSgRVBg/s1600/JBC+Campaign+20.jpg
Jamani hii ni tabia mbaya sana na haipendezi kabisa kwa watu wa Mungu. Wadada wengine wanavaa nguo ndevu sana lakini utashangaa kuna bonge la mpasuo pajani au makalioni, ukimuangali mbele unasema hakika leo nimeonana na dada anajitambua, ngoja sasa uone nyuma...utakimbia!!!

Umarekani na Uulaya unatuweka pabaya sana Waafrika, tunaharibu utamaduni wetu na tunakuwa kelo kwa Mungu wetu. Nguo zetu zisitusababishie tukakosa mbingu.

nguo fupi kwa wadada na wamama zimeonekana ni fashion, utamkutana mmama wa heshima ukimuangalia kwa sura lakini mavazi yake ni ovyo yaani uchuroooo...Unaweza kuona unapendeza na unavutia kwa miguu yako mizuri unayoonyesha kwa watu, kiroho chako kinafurahi sana unapoona wanaume wanaumia shingo kukuangalia ukipita na kinguo chako kifupi na ukasahu kuwa unamkosea Mungu wako.
Unapoona huyu jamaa anageuza shingo na kukuchungulia wewe mdada ujue unamsababishia kutenda dhambi ya tamaa na baadae kumuingiza katika fikra potovu za kutafuta wanawake walio na mguu kama wako ili alale nao..dhambi ya zinaa inamvaa huyu mkaka...
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdGGMvY-lG3fv-mxZizlQVnNTsYEldC6tZHB2MRjSCQXF0oIUjmjdMowKOV_CBiNLh_HUEWarRvQauMsHTjNOTiRbSZ7BSdmXHRYfV0jwSrHFB37ytWrsRnRizQdgTnGvIjcGoXrKz9CAe/s1600/JBC+Campaign+31.jpg

Sina uhakika na uvaaji wa suruali kwa mtu aliyeokoka kama ni sahihi...Kwani ninasema hivi..? kwasababu suali kwa mwanamke ni chanzo kikubwa sana kwa mwanaume kumfikiria vibaya huyu mwanamke. Kuna suruali zingine zinakuwa zimebana sana mwili na zinaonyesha maumbile yako. Mguo hizi kwa sasa zinavaliwa hata na wachungaji au watumishi wa Mungu kama vile waimbaji wamekuwa wakitupia sana mapigo haya bila hata aibu. Tukemee hali hii watu wa Mungu. Tuamuudhi Mungu wetu.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga


Comments