REHEMA CHALAMILA (RAY C) ANAYESEMA ANAMWAMINI MUNGU KWANI AMEMUOKOA NA MADAWA YA KULEVYA. ANAZIDI KUWAOKOA WENZAKE MITAANI
Mwimbaji wa jimbo za kijamii ambaye alijiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya hivi karibuni na kuharibu future yake ya muziki na maisha yake kwa ujumla kutoka na matumiza ya madawa ya kulevya. Mwanamuziki huyu kwa msaada wa Rais JK Kikwete aliweza kuachana na madawa ya kulevya.
Ray C baada ya kuona madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya sasa ameamua kwenda mitaani na kuongea na watumiaji na kuwashauri waachane nayo, na baadhi yao wamekubali na wamesema wapo pamoja na Ray C na wako tayari kufika katika Tiba ya Methadone Mwananyamala kwa matibabu, wamesema wamechoka maisha ya utumwa.
Ray C ambaye kwa sasa ameonekana kuwa na hofu ya Mungu, kila jambo analosema kuhusiana na madhara aliyopata kutokana na madawa ya kulevya amekuwa akimshirikisha sana Mungu na kumtaja kuwa Mungu ni mwema.
Hii ni changamoto kwetu tulieokoka, kufanya vitu kwa vitendo, tuondokane na ile hali ya kuhubiri sana kwa maneno bali tuantakiwa kutoka sasa kwenda kuifikia jamii iliyoangamia na kuiokoa kwa mali zetu na pia kuwajenga KIROHO kwa kuwafundisha NENO la Mungu. Inapendeza sana kuona tunawaombea watu hawa kanisani, lakini tumekuwa wavivu wa kuifikia jamii hii inayoteseka kwa shida mbalimbali. Tuombe Mungu sana atufungue ili tujue haya mambo.
Yesu Kristo alikuwa ni mtu wa maombezi sana, lakini hakuishia kuomba tu bali alitoka ka kuifuata ile jamii yenye uhitaji. Yesu Kristo hakuwa mtu wa kukaa tu bali alikuwa mchapa kazi na akifanya kwa vitendo. Watumishi wa Mungu tuamke sasa na kufanya kazi ya Mungu kwa mifano, na hii itapendeza sana mbele za wanadamu na mbele za Mungu.
Tuzidi kumuombea mwimbaji huyu wa nyimbo za kidunia siku moja amwimbie huyu Mungu ambaye amekuwa masaada mkubwa sana katika maisha yake, na sasa anatumia mali zake na maarifa yake kuwaokoa watu wengine. Tuiombee Foundation yake ya RA C FOUNDATION PAMOJA ili ilizi kusonga mbele kuwaokoa watu na ikiwezekana iwe na sehemu ya watu waliookolewa wapate NENO LA MUNGU
Wenu katika Bwana
Rulea Sanga

Comments