RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUNGU IBARIKI JUMATATU YANGU

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuamsha tena na kuiona Jumatatu hii. Mungu ametutetea na mengi usiku wa kuamkia leo. Wengi wamekufa na wengine usiku huo walipelekwa hospitalini, polisi, wengine wamepata ajali. Mungu amekuwa mwema kwangu na kwako na ndio maana tumeiona siku ya leo. Hii tunasema ni kwa neema tu na sio kwa ujanja wetu.



Mungu wetu atabaki kuitwa Mungu kwa wema wake na upendo wake kwetu. Ibada ya Jumapili ilikuwa ni ibada ya sifa, maana Nabii na Mtume Josepahate Mwingira na waumini waliweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji ibada nzima, na baadae aliweza kuombea watu wenye shida mbalimbali na wale walioamua kumpokea Yesu Kristo. Ibada hii ilionekana kuwabariki walio wengi.

Mimi nikutakie Jumatatu njema na yenye mafanikio. Niombee nitimize ndoto zangu.
Wenu katika Bwana
Rulea Sanga

Comments