RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PASTOR RYOBA AFUNGISHA NDOA YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MUSHI NA NIKODEMUS SHABOKA JR NDANI YA BOTANIC GARDEN DAR EW SALAAM

Duniani wawili wawili, hili limetimia kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Mushi na Nikodemus Shaboka Jr. baada ya kiu yao ya muda mrefu ya kuitwa mume na mke kutimia siku ya leo. Inapendeza kuona watu wanaacha na ukapera wa kushindia chips na sasa kuingia katika ndoa wakiwa na uhakika jioni kuna msosi kamili nyumbani. Ukapera unaumiza sana kwani unakuwa huna ratiba maalumu ya misosi, unaweza ukagonga chips au soda na biskuti ikawa imetoka.
Rose Mushi

Tunamshukuru Mungu kwa kuwasaidia watumishi wa Mungu hawa kwa kuwaunganisha kuwa kitu kimoja. Tunawaombea maisha mema yenye baraka katika ndoa yao hii ambayo imefanyika baraka kwa walio wengi na wanaowajua wanandoa hawa.
Maids

Sasa tunaamini kazi yao ya kumtumikia Mungu itakuwa haina maswali mengi kama ilivykuwa zamani. Rose Mushi mbali na uimbaji pia ni mwandishi wa vitabu na ni mwalimu wa kufundisha mambo mbalimbali. Amekuwa akifundisha hata maswala ya ndoa hata kama yeye alikuwa hajaolewa, Mungu alikuwa akimtumia na kumpa ujasiri wa kujibu hata maswali ambayo pengine yalikuwa yakimhusu kutokana na ukapera wake.
Rose Mushi

Wanandoa hawa wameleata heshima katika kanisa na familia yao. Inapendeza kwa wazazi wanapoona watoto wao wanaolewa na kuoa. Tumekuwa na vijana wengi sana ambao bado hawajaolewa na kuoa, na wanatamani kuoa na kuolewa lakini kuna vitu ambavyo vinawazuia, inawezekana ikawa kifedha, dini, nguvu za giza, woga wa maisha na vitu vingine kama hivyo.
Ewe mwanandoa unapaswa kuwaombea watu kama hawa ili waweze kuishi maisha kama haya ambayo Rose na Nikodemus wanaenda kuishi sasa.

 Rose Mushi na mume wake Nikodemus Shaboka Jr
  Rose Mushi na mume wake Nikodemus Shaboka Jr
 Jenifer Mgendi na Jasmine Harry wakiwa ndani ya tukio


 Watumishi wa Mungu ndani ya Botanic Garden.
 Myboss Original na mamaye wakiwa ndani ya tukio
 Nickodemus Shaboka Jr. Akiwa na Norman Massawe best man.

Pastor Ryoba akiwa tayari kufungisha ndoa ndani ya Botanic Garden.
 Nikodemus akimfunua mke wake Rose







Ze bloga Samasasali akiwa amepiga vitu simpo..hakuna matata


ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBOFYA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO








.












Wakisani vyeti vya ndoa









Comments