RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA ZA IBADA YA JUMAPILI 01.06.2014 KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM

Jumapili hii Mtume na Nabii Josephate Mwingira alikuwa safarini Mwanza, aliweza kuongea na waumini kwa njia ya simu mabpo simu iliwekwa Loud Speaker na kuunganishwa katika spika kubwa. Nabii aliongea kwa furaha sana na alionyesha ku-miss ibada hii ya Jumapili. Alitumia muda wa dakika kama 20 akiongea na waumini kanisani huku akimpongeza mke wake kwa kazi ya Mungu.

Ibada iliongozwa na mke wake mpendwa Eliyapunda. Ibada ilifanyika baraka sana kwa waliofika na waliokuwa wakifuatilia katika luninga.
Mbali na kula chakula cha Bwana pia kulikuwa na nusu tamasha kutoka na uimbaji ambao ulikuwa ukiendelea katika kanisa hili. Hakika kanisa hili limejaliwa kwa uimbaji. Nyimbo zao hazifananishwi na makanisa mengine kwa style zao na sauti zao. Mungu amewweka kitu katika maisha ya hawa waimbaji. Mungu azidi kuwatunza waimbaji hawa.

Tuone baadhi ya picha.

Mke wa Nabii na Mtume Josephate Mwingira akihubiri

Kwaya za Mass Choir pamoja na Chipukizi, zikimwinua BWANA MUNGU wetu MKUU
Pichani: Ukombozi na Uponyaji Ibadani leo


POKEA BARAKA ZA LEO
Photo: Naibariki Jumatano yangu...

Comments