John Lissu na mke wake
Hongera John Lisu kwa kuwalea watoto wako hawa mapacha. Mungu kakukumbuka na kukupa zawadi ya watoto mapacha watatu. Kwa kupitia kwako tunaamini ya kwamba Mungu wetu humkumbuka mtu na kumtimizia haja ya moyo wake. Katika ndoa yako ulifikiria kupata mtoto lakini Mungu kafanya zaidi ya hapo. Umekuwa mwaminifu kwa kazi yako ya uimbaji, umemuimbia Mungu wetu wa mbingu kwa moyo wako wote, na leo Mungu kakuzawadia watoto wazuri.

Ninampongeza pia mke wako kwa kuwatunza watoto hawa wenye afya njema tangia walipokuwa tumboni mwake. Amekuwa mvumilivu mpaka sasa ameshuhudia kwa macho yake kile alichokuwa akikilea katika tumbo lake.

Ushauri wangu, zidi kumtumikia huyu Mungu kwa uaminifu naye atazidi kufungua milango mingine zaidi ya hapo. Ninaishi kwa imani ndio maana nasema Mungu Baba atafanya makubwa na wewe utashangaa upendo wake wa AGAPE.

Mungu alivyo wa ajabu akakupa mke ambaye anaendana na wewe . Mungu amekupa mke anayepiga gitaa kama wewe...kweli umependelewa mtumishi wa Mungu.

Comments