RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

USIKOSE MKUTANO MKUBWA WA TAI "CHUMA KUNOA CHUMA"

Malengo ni nini?
Binafsi nimekuwa na changamoto kubwa sana kutafuta maana rahisi na ya kueleweka juu ya neno “malengo.” Huwa ninawaambia watu wengi ya kwamba inawezekana kwamba usiwe na maana (definition) ya malengo, lakini ukiyaona ni lazima utayafahamu. Lakini, huwa ninaamini ya kwamba huwezi kuanza kutenda/kushughulika na kitu, jambo au hali usiyoijua. Na kwa misingi hiyo basi, ninawiwa kujenga ufahamu ndani yako juu ya malengo. Katika mzunguko niliouonyesha hapa awali kwenye taswira, malengo huzaliwa kutoka kwenye dhamira (utume). Lazima dhamira ikusukume kuumba malengo! Sasa, malengo ni nini basi? Malengo ni ajenda au mahitaji husika/mahususi ambayo mtu fulani hujiwekea kwa kipindi cha muda fulani ili kumzalishia matokeo yanayoonekana, matunda na/au mabadiliko yaliyokusudiwa… hupimika, huweza kufanyiwa tathmini!


Weka malengo kwa vigezo hivi:

Malengo mazuri huwa na sifa ya “SMART”, neno la kiingereza linalomaanisha nadhifu, -enye uelewa mzuri. Kwahiyo malengo yako yanapaswa kuwa nadhifu, sasa neno smart linabeba maana kubwa sana kwa kila herufi yake:
S -(Specific), kwanza lazima lengo liwe ni maalum au hususani juu ya jambo, mtu au hali fulani. Kwa mfano mtu anaposema, “Mimi ninataka kupambana na umaskini.”. Ni sawa hilo ni lengo lakini si hususani, yaani halina mwelekeo… Je, mtu huyo anataka kupambana na umaskini wa aina gani (umaskini wa kifikra, kifedha…), Je, anapambana nao katika ngazi ipi? (mtu binafsi, kijiji, familia, nchi…) lazima uainishe. Na ndivyo ilivyo katika huduma, unaweza kusema nina wito wa kuhubiri injili, ni sawa lakini ni katika ngazi gani? Ni wazi kwamba kuizungukia dunia yote ni jambo ambalo si rahisi (nchi zote, mikoa yote, majimbo yote, wilaya zote, vijiji vyote na kaya zote za dunia.) Si jambo rahisi, ukijaribu utaumia tu na matunda hayatakaa.

Mfano: Lengo langu ni kuihubiri injili nchini Tanzania.
Kumbuka kuwa Tanzania ni nchi kubwa, ina mikoa zaidi ya ishirini na wilaya zake na tarafa, kata, mitaa/vijiji na kaya (familia) kwahiyo unatakiwa kuwa specific zaidi. Kwahiyo waweza kusema, kuhubiri injili nchini Tanzania katika ngazi ya wilaya.
M -(Measurable), Pili lengo lolote linatakiwa kupimika, Je unaweza kuuona ufanisi, matokeo au matunda ya lengo hilo? Kwa mfano lengo la kuihubiri injili nchini Tanzania katika ngazi ya wilaya…Baada ya muda je unaweza kupima matokeo ya lengo hilo. Sasa kuna njia mbalimbali za kuyapima malengo yetu, baadhi ya njia ni kuangalia mabadiliko katika maisha ya watu, je, kuna mabadiliko yoyote,njia nyingine ni kuangalia je, idadi iliyokusudiwa imefikiwa? Tukiendelea kuutumia mfano wetu wa kuihubiri injili nchini Tanzania katika ngazi ya wilaya ili tuufanye kuwa SMART; Ili kuweza kupima lengo hilo waweza kusema:
Kuihubiri injili kwa watu 1000 nchini Tanzania katika wilaya 4 (unapaswa kuzitaja wilaya ulizokusudia kuzifikia) kuanzia Januari mpaka Juni.

Comments