RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BAMBOO KUVUNJA MBAVU KATIKA FINALI ZA MESS CUP NA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA MKOANI IRINGA

Baada ya kuvunja mbavu watu wengi kwa kuchekesha katika luninga, sasa Bambo atahakikisha wakazi wa Iringa wanavunjika mbavu katika finali za MESS CUP zitakazoamabata na uzinduzi wa Albamu kali ya Mess Jacob Chengula inayoenda kwa jina la MUNGU HABADILIKI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNQAy7PVsn6Wvs_qtGhj0KMSRCkSsuL7hS9s-keIJjb6dziFO0w0TqxNBPXnaVzaKdk5SvxjNSmASjXH5BJcshPIkKbR-_w3a6oq7v8vtiU1enup4IZA2XlQAP3DwopfYu2_5pYzzL_Nlo/s320/Bambo+ajali.jpeg
Wakazi wa Iringa umefika wakati wa kufanya kazi ya Bwana na kuwaonyesha watu wa mataifa kuwa sisi ni vichwa na sio mikia. Tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kila jambo kwa kuwaunga mkono watumishi wa Mungu wanapokuwa wamepewa maono na Mungu kuwakusanya watu wakifurahi pamoja na kumtukuza Mungu wetu wa mbinguni. Leo hii mtumisjhi wa Mungu Mess Jacob Chengula amepata maono na Mungu ya kufurahi pamoja na wakazi wa Iringa na ndio maana akapata wazo la kuandaa finali za mpira zinazoenda kwa jina lake la MESS CUP ili wewe unayependa soka uweze kufika na ukishafika basi Neno la Mungu na upako wa ajabu utakuujia kwa njia ya uimbaji wa Mtumishi wa Mungu Mess Jacob Chengula.

Katika zoezi hilo la kugawa kombe kwa wshindi na kuzindua albamu hiyo pendwa sana, kutakuwa na waimbaji zaidi ya kumi na tano (15) watakaovamia jukwaa moja wakitumia mic moja huku wakumsindikiza mwimbaji mmoja ambaye ni Mess Jacob Chengula. Kama uanvyojua watumishi hawa wanamzuka wa kufanya kazi ya Mungu na wanapopata tu muda wa kufanya kazi ya Mungu, huwa hawakosei kabisa jukwaani, uimbaji wao ni wa kuotea mbali. Kutakuwa na fleva tofauti za uimbaji kama Hip Hop, sebene, zuku, byimbo za kuabudu na fleva mbalimbali.

RATIBA YA FINALI ZA MESS CUP NA UTAMBULISHO WA NYIMBO
MPYA YA “NANI MSHINDI KAMA YESU” YA MESS JACOB CHENGULA
4:00 Asubuhi - 6:00 Mchana - Kutafuta Mshindi wa tatu na wa pili
6:00 Mchana - 8:00 Mchana - Finali za MESS CUP
9:00 Alasiri - Zawadi za washindi
9:30 Alasiri - 12: 00 jioni - Uzinduzi na kutambulisha Nyimbo mpya za Mess Chengula
Mawasiliano yetu ni +255 715 880 584: Blogu: www.messchengula.blogspot.com

Comments