RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DR. FADHILI EMILY AMSHUKURU MUNGUKUKUTANA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TIBA (UNIVERSITY OF TEACHING HOSPITAL) LUSAKA NCHINI ZAMBI

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic iliyopo nchini Tanzania aliweza kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Tiba kinachotambulika kwa jina la THE UNIVERSITY TEACHING HOSPITAL (U.T.C).


Dr. Fadhili Emily aliweza kumshukuru Mungu kwa kile alichompa katika maisha yake, hasa ule uwezo wa kuweza kutambua na kujua ni dawa gani zinaweza kumsaidia mwanadamu ambaye amekuwa akiteseka sana na magonjwa sugu ambayo yamemsababishia kuonekana kama amekataliwa na dunia.

Pia aliongeza kusema kuwa anapenda sana kuisaidia jamii inayosumbuka na magonjwa sugu yayosababishwa taifa kushuka nyuma kimaendeleo kutokana na nguvu kazi kupungua. Wagonjwa wamekuwa ni watu wa kukaa nyumbani na kuwa tegemezi, hawawezi kufanya kazi kutokana na magonjwa yao kutoruhusu kufanya kazi. Badala ya watu kwenga kufanya kazi wamebaki nyumbani wakiuguzwa na wengine wamesababisha na watu wengine ambao ni wazima kushindwa kwenda  kazini na badala yake wamebaki nyumbani kuwasaidia hawa wagonjwa.
 Akiongea na Rumafrica, Dr. Fadhili Emily alisema anapenda sana kuwasaidia madaktari wenzake ambao bado hawajapata maarifa kama aliyojaliwa na mwenyezi Mungu ya kutambua na kugundua dawa za mimea na matunda ambazonni tiba nzuri kwa binadamu. Kumbuka Mungu huyu ndiye aliyeumba hii mimea na alituachia agizo la kutawala kila kitu kilichopo duniani na sio vilivyomo duniani kututawala.

Hali ya kuonekana watu wanataabika na magonjwa na kuona hakuna wataalamu wa kutosha kutokomeza maradhi yanayowasumbua wagonjwa, Dr. Fadhili Emily aliweza kutuma ujumbe kwa njia ya watsap kwa mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga ukisema, ":Kwa kweli napenda sana kujua na ninatamani sana kusaidia madaktari wenzangu duniani kuhakikisha tunatokomeza maradhi yasiyo ya lazima katika dunia hii, ninawaomba Watanzania wenzangu mnisaidie kwa maombi ili Mungu anyooshe mkono wake niwaletee Chuo Kikuu Afrika cha Tiba zitokanazo na sayansi ya mimea Asili ambacho kitaitwa UNIVERSITY OF MEDICINAL PLANTS IN TANZANIA"

 Kutoka na wazo la kuanzisha Chuo cha tiba za mimea asili, Dr. Fadhili Emily alitoa hoja yake ya msingi na kusema anaona itakuwa vema sana kutoa elimu  ya kutosha juu ya afya ya miili yetu na njisi namna tuwezavyo kutuma lasilimali za kutumia mime na kujitibu wenyewe. Alimaliza kwa kumshukuru Mungu na kumuomba mwenyezi Mungu aibariki nchi ya Tanzania kuwa na amani na utulivu na kuondoa haya mateso ambayo wanapata kutokana na magonjwa.


Dr. Fadhili Emily ambaye amekuwa akisafiri nchi tofauti kujifunza na pengine kuwasaidia watu walioko katika nchi hizo ili waweze kuwa na maarifa kama aliyonayo. Safiri zake zimekuwa na matunda makubwa kwani kila anapokuja nchini anakuwa na kitu cha tofauti sana na nguvu za ajabu za kupambana na magonjwa na maradhi yanayowasumbua watu.

Tunakukaribisha sana katika ofisini zetu zilizopo Afrikana, Mbezi Beach.
 MATUKIO KATIKA PICHA












Comments