Baada ya kuachia nyimbo yao ya MY SAVIOUR GOD Grace na Joshua wameachia ngoma nyingine ya kumtukuza Mungu ya TUMTANGAZE YESU. Nyimbo hii imeimbwa kwa lugha ya Kiswahili wakati nyimbo yao iliyobeba jina la albamu imeimbwa kwa lugha ya Kiingereza. Watumishi wa Mungu wanafanya vizuri sana katika huduma yao ya kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji. Kumbuka hawa ni ndugu na wameamua kutotengana kufanya kazi ya Mungu.
Uimbaji wao ni wa kipekee sana kama umebahatika kuwasikia wakiimba. Ujumbe wao kwa kweli unajenga, unaelimisha na kuadibu ukiusikiliza kwa makini. Mpaka sasa wameachia nyimbo mbili kwa mfumo wa Audio na wanajipanga kisawasawa kwaajili ya video.
Sasa mdau wangu tega sikio kuwasikiliza watumishi wa Mungu wakikuletea ujumbe kutoka kwa Mungu kupitia uimbaji wao. Utabarikiwa sana na utaamini maneno yangu.
Comments