MSIKILIZE MWIMBAJI WA GOSPEL ANNA DAT ALIYEVUTA BANGI, ALIISHI KAMA MWANAUME, ALIKUWA AKIPIGA WATU MITAANI, ALIYETENGWA NA JAMII, ALIYEKUWA MUHUDUMU WA BAR AOKOKA NA SASA ANATAKA KUJENGA KANISA
Kama kawaida yake, Rumafrica ilikuahidi kuwa itakuletea story kuhusiana na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Anna Dat mkazi wa Kilimanajoro huko Moshi. Mwimbaji huyu ambaye kwa sasa ana ndoto za kujenga kanisa na kuwa mchungaji mbali na uimbaji aliweza kufika katika ofisi za RUMAFRICA Sinza Africa Sanga na kuweza kufunguka kuhusiana na maisha yake kabla hajamjua huyu Bwana Yesu Kristo.
Anna Dat
Anna Dat alisema, ameishi maisha machafu sana, ametengwa na jamii, mama yake alimkata, alikataliwa na kila mtu kutokana na uhuni na tabia mbaya aliyokuwa nayo, amevuta bangi sana, haitoshi alikuwa muuza bar baada ya maisha kumpiga chenga, aliishi maisha ya kiuanaume yaaani alikuwa na tabia ya uanaume, aechezea elimu na mambo mengi ambayo utasikia katika video hapo chini.
Mwimbaji huyu ambaye alisema anampenda sana Rose Muhando kiumbaji na ndio maana na na yeye anajaribu kuimba kama Rose Muhando hata kama anakipaji chake ambacho Mungu amempa. 
DVD Cover la albamu ya Anna Dat

DVD Cover la albamu ya Anna Dat
Nisikumalizie uhondo, nakuomba sasa usikilize kwanini aliamua kuokoka na sasa ni mwimbaji mwenye ndoto ya kujenga kanisa
Comments