RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIKU YA KWANZA YA KONGAMANO LA WANAWAKE KANISA LA ELIM PENTEKOSTE JIMBO LA MASHARIKI NA PWANI (27 - 29/08/2014). KONGAMANO LINAFANYIKA CHALINZE.



Inapendeza sana unapoona watu wa Mungu wanaamua kukaa pamoja na kufanya maamuzi ya msingi kwa lengo la kumtumikia Mungu. Ukiona mtu anaacha kazi zake na kuamua kumtumikia Mungu kwa kufanya kazi yake ujue sio kitu kidogo. Tumekuwa na changamoto kubwa sana kipindi hiki kuanzia watoto hadi wazee katika suala zima la kupata fedha. Kila mtu akiamka anafikiri sana ni jinsi gani atapata fedha kwaajili ya kuendesha maisha yake, kuna wengi wanaamua kuingia hata katika vitendo mbaya vya kutafutia fedha ili mradi maisha yasonge mbele

Wanawake wa kanisa la ELIM Pentekoste kwa msaada wa Mungu walweza kuona jambo la msingi ambalo linaweza kubadilisha maisha yao ni kumtumikia Mungu wa mbinguni na ndio maana wakaja na wazo la kuanda kongamano la wanawake ambalo lilifanyika Chalinze. Tunaamini katika kongamano hilo kuna watu waliweza kutoka na kitu kipya ambacho hawajawahi kupata popote na kama wameshawahi kupata basi hakikuleta matunda kama walichokipata katika kongamano hilo.

Ndugu msomaji kuna faida nyingi za makonagamo au mikutano inayoandaliwa na watumishi wa Mungu. Mungu huzungumza na wabeba maono wa mikutano hii na kuwapa ujumbe kwaajili yako, kwahiyo unapokosa kufika ujue unakosa Neno la Mungu, na mwisho wa siku unaishia kusema mimi Mungu hanikumbuki. Kuanzia sasa unaposikia makongamano unatakiwa kuhudhuria na kumuomba Mungu akupe kibali cha kupata hata ruhusa kutoka kazini kwako ili upate kitu kipya kutoka kwa Mungu kwa njia ya watumishi  wake.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 851 523


















Comments