RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NIGHT OF WORSHIP NDANI YA KANISA LA CCC HAISIMULIKI. PONGEZI KWA NEXT LEVEL. KAZI YA BWANA HAIKUABISHWA NA SHETANI

Hii ni nzuri machoni pa Bwana na machoni pa Mungu tunapoona watu wa Mungu wanajitoa na kuwa wabunifu kwa kazi ya Mungu. Inaleta raha ndani ya mtima. Tunawapongeza sana watumishi wa Mungu hawa walioandaa kitu hiki kizuri kinachoenda kwa jina la NIGHT OF WORSHIP kilichofanyika katika kanisa bora na zuri Tanzania la City Christian Centre (CCC) Upanga. Night of Worshipa ambayo iliandaliwa na kundi zima na machari nchini Tanzania la NEXT LEVEL ilifanyika baraka sana katika usiku wa tarehe 30/08/2014. Watu waliweza kukesha kwa kusifu na kuabudu wakiwa na kauli mbiu ya EXPLAINABLE GOD. Mungu azidi kuwalinda hawa waandaji na ili wazidi kufanya kazi ya Mungu kwa viwango vikubwa ili mataifa wajue yupo Mungu muweza wa yote.

Rumafrica inawapongeza sana watumishi hawa wa Mungu na pia media kwa kutuwezesha kupata hizi picha. Tunawapongeza bloggers wote walioweza kupiga picha hizi na kuturushia katika Facebook nasi tukazipata.








Comments