Paulo alimwandikia hivi Timoteo:
Cha pili – awe makini sana kuhusu mafundisho yake, kwa sababu wokovu wake wa milele na wa wanaomsikiliza unategemea anachofundisha, kama Paulo alivyoandika katika mstari huo hapo juu. Mtumishi akifuata mafundisho ya uongo, au akipuuza kuwaambia watu ukweli, matokeo ni hasara ya milele kwake na kwa wengine.
Ila – hakuna kujitetea kwa mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi, kama atafundisha uongo, maana Mungu amempa yeye Roho Mtakatifu na Neno Lake ili kumwongoza katika kweli. Watumishi wenye makusudi mabaya mara nyingi hurudia kama kasuku mafundisho yanayopendwa na watu, yenye kutolewa na waalimu wengine. Wao hawajifunzi Neno ili wapate kitu cha kutoa, na inakuwa rahisi kwao kupotoka katika mafundisho yao na imani zao. Ulinzi kinyume cha hayo ni mtumishi kusafisha moyo wake, akihakikisha kwamba kusudi lake moyoni ni (1) kumpendeza Mungu, na (2) kuwasaidia watu wawe tayari kusimama mbele za Yesu, badala ya kutaka kutajirika kibinafsi, au kuwa na uwezo au kuwa maarufu. Tena, lazima ajifunze kwa bidii sana Neno la Mungu ili awe na ufahamu kamili na wenye usahihi. Paulo alimwandikia Timoteo tena, akasema hivi:
Kufasiri sawasawa Neno la Mungu hufanywa sawa tu na kufasiri sawasawa maneno ya mtu. Tukitaka kuelewa vizuri maana iliyokusudiwa ya mwandishi yeyote au msemaji tunayemsikiliza, inabidi tufuate sheria fulani za ufasiri, ambazo msingi wake ni akili tu ya kawaida. Katika sura hii, tutatazama kanuni tatu muhimu za kufasiri Biblia ipasavyo. Ni hizi zifuatazo: (1) Soma na akili timamu, (2) Soma ukizingatia mantiki, na (3) Soma na moyo ulio wazi.
Mlinganisho huonyesha jinsi vitu viwili ambavyo ni tofauti kabisa, vinavyofanana. Katika Maandiko utakutana na hili mara nyingi sana. Mfano mmoja ni maneno ya Kristo wakati wa Chakula cha Mwisho na wanafunzi Wake.
Kuna wanaotoa hoja hivi: “Lakini, Yesu alisema kwamba mkate na divai ni mwili Wake na damu Yake. Mimi nitaamini alichosema Yesu!”
Sawa. Kuna wakati ambapo Yesu pia alisema ni mlango (Yohana 10:9). Je, alifanyika mlango halisi, wenye komeo na bawabu na kitasa? Wakati mwingine Yesu alisema Yeye ni mzabibu, na sisi ni matawi (Yohana 15:5). Je, Yesu alifanyika mzabibu halisi? Je, sisi tumefanyika matawi halisi ya mzabibu? Wakati mwingine Yesu akasema ni nuru ya ulimwengu na chakula kilichoshuka kutoka mbinguni (ona Yohana 9:5; 6:41). Je, Yesu ndiye mwangaza wa jua siku hizi na boflo ya mkate?
Basi – hizo zote ni lugha za mfano ambazo ni mlinganisho wa vitu viwili ambavyo ni tofauti kabisa, vyenye kufanana kwa kiasi fulani. Kwa namna fulani, Yesu ni kama mlango na mzabibu. Maneno ya Yesu wakati wa Chakula cha Mwisho ni mifano pia. Divai ilikuwa kama damu Yake (kwa kiasi fulani). Mkate ulikuwa kama mwili Wake (kwa kiasi fulani).
Hebu tutazame mifano mitatu ya Yesu, tukianza na Mfano wa Juya.
Mfano huu ni mzuri wa kuonyesha jinsi ambavyo kila mlinganisho usivyofaa kabisa kueleza kitu kwa sababu hatimaye vitu vile vinavyolinganishwa hufikia mahali pa kutofautiana. Hatupaswi kwenda zaidi ya kusudi la msemaji, yaani kudhani kwamba tofauti zote ndiyo kufanana. Kwa mfano: Wote tunajua kwamba “samaki wazuri” huishia kupikwa kwa moto, na “samaki wabaya” hurudi majini. Yesu hakutaja hayo, maana yangekuwa kinyume cha kusudi Lake.
Mfano huu haufundishi mkakati wa “uinjilisti kwa juya” – kwamba tujaribu kumkokota kila mmoja kanisani – mwema na mbaya – akitaka asitake! Mfano huu haufundishi kwamba ufuoni mwa bahari ndipo mahali panapofaa kufanyia uinjilisti. Mfano huu hauthibitishi kwamba Unyakuo wa kanisa utatokea mwisho wa kipindi cha dhiki kuu. Wala mfano huu haufundishi kwamba wokovu wetu ni chaguo la Mungu kwa kuwa samaki waliochaguliwa katika mfano hawakuhusika kwa njia yoyote na kuchaguliwa kwao. Usilazimishe maana isiyostahili katika mifano ya Yesu!
Kama nilivyokwisha sema huko nyuma, Yesu aliwaambia wanafunzi Wake wa karibu sana mfano huu (ona Mathayo 24:3; Marko 13:3), waliokuwa wanamfuata kwa uaminifu sana wakati huo. Basi – kinachosemwa wazi kabisa katika mfano huu ni kwamba iliwezekana kwa Petro, Yakobo, Yohana na Andrea kutokuwa tayari wakati Yesu atakaporudi. Hii ndiyo sababu alikuwa anawaonya. Basi, mfano huu unafundisha kwamba upo uwezekano kwa wale walio tayari sasa kwa ajili ya kurudi kwa Kristo kutokuwa tayari wakati atakaporudi. Wanawali wote kumi walikuwa tayari kimsingi, lakini watano wakawa hawako tayari. Kama bwana arusi angefika mapema zaidi, wote kumi wangeingia katika karamu ya arusi.
Lakini, nini maana ya kuwepo kwa wanawali watano wapumbavu na watano wenye busara? Je, maana yake ni kwamba katika waamini wote, nusu tu ndiyo watakuwa tayari wakati Kristo atakaporudi? Hapana.
Nini maana ya mafuta? Je, ni mfano wa Roho Mtakatifu? Hapana. Je, ni udhihirisho kwetu kwamba wale tu waliobatizwa na Roho Mtakatifu ndiyo watakaoingia mbinguni? Hapana.
Je, kurudi kwa bwana arusi usiku wa manane kunaonyesha kwamba Yesu atarudi usiku wa manane? Hapana.
Mbona bwana arusi hakuwaita wale wanawali wenye busara ili wawatambue wenzao wapumbavu? Kama angefanya hivyo, ingeharibu hoja nzima ya mfano, maana wale wapumbavu hatimaye wangeingia arusini.
Labda tunaweza kusema kwamba, sawa na jinsi wale wanawali wapumbavu waliyvokosa taa na wakalala, ndivyo na waamini wapumbavu wanavyoanza kutembea katika giza la kiroho na kujikuta wamelala kiroho pia. Mwishowe, wanajifikisha mahali pa kuhukumiwa. Pengine arusi katika mfano huu inaweza kufananishwa na karamu ya arusi ya Mwanakondoo hapo baadaye – ila, hapo ndipo tunapoweza kufika bila ya kuanza kulazimisha maana nyingine katika mfano huu.
Hoja kuu za mfano huu ni dhahiri kabisa: Waliookoka kweli huzaa matunda; wasiookoka hawazai matunda. Japo Mungu hawahukumu waovu sasa hivi wanapoishi miongoni mwa waliookoka, siku moja atawatenganisha kutoka kwa wenye haki na kuwatupa jehanamu.
Halafu – Yesu Mwenyewe alitoa maana ya mfano huu, hivyo hakuna haja ya mtu kutafuta maana nyingine kuliko aliyotoa.
Wataalamu wengi wa Biblia wanahesabu kila tamko lenye kueleza viungo vya mwili wa Mungu kama vile mikono Yake, pua, macho na nywele kuwa ni lugha ya mfano. Wanasema haiwezekani Mungu Mwenyezi kuwa na viungo kama wanadamu.
Mimi sikubaliani nao kwa sababu kadhaa. Kwanza: Kwa sababu Maandiko yanasema wazi kabisa kwamba sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na sura Yake.
Tena, tuna maelezo fulani kuhusu Mungu yatolewayo na waandishi wa Biblia waliomwona. Kwa mfano: Musa na wazee sabini na tatu wa Israeli walimwona Mungu!
Nabii Danieli pia alipata maono ya Mungu Baba pamoja na Mungu Mwana.
Basi, mimi ninaamini kwamba Mungu Baba ana umbo lenye utukufu sana linalofanana na umbo la mwanadamu, japo Yeye hana mwili wa nyama na damu – ni roho (ona Yohana 4:24).
Sasa – Utajuaje mafungu ya Maandiko yanayotakiwa kufasiriwa kama yalivyo, na yapi yafasiriwe kwamba ni mifano? Hilo ni rahisi tu kwa yeyote anayeweza kufikiri vizuri. Wewe tafsiri kila kitu kama kilivyo, isipokuwa kama kinaeleweka vingine. Kwa mfano: Vitabu vya manabii katika Agano la Kale pamoja na kitabu cha Ufunuo cha Agano Jipya vimejaa lugha ya mifano. Kuna ambayo imefafanuliwa, na mingine haijafafanuliwa. Lakini lugha za mifano zinazohusika si ngumu kutambua.
Inawezekana kuifanya Biblia iseme chochote unachotaka iseme kwa kutenganisha maandiko na mantiki yake. Kwa mfano: Una habari kwamba Biblia inasema Mungu hayupo? Tunasoma hivi katika Zaburi ya 14, “Hakuna Mungu” (ms. 1). Lakini sasa, tukitaka kutafsiri maneno hayo kwa usahihi, lazima tuyasome katika mantiki yake. Ni hivi: “Mpumbavu amesema moyoni mwake, ‘Hakuna Mungu’.” (Zaburi 14:1. Maneno mepesi kukazia). Unaona? Mstari umekuwa na maana tofauti kabisa!
Mfano mwingine: Nilisikia mhubiri mmoja akihubiri juu ya Hitaji la Wakristo kubatizwa ‘katika moto’. Alianza ujumbe wake kwa kusoma maneno ya Yohana Mbatizaji katika Mathayo 3:11, kama ifuatavyo: “Kweli, mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba, lakini yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi. Sistahili hata kuvua viatu vyake. Huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (TLR).
Kutokana na mstari huo mmoja tu, alitengeneza ujumbe. Ninakumbuka akisema hivi: “Haitoshi kwamba umebatizwa na Roho Mtakatifu! Yesu anataka akubatize kwa moto pia, sawa na jinsi Yohana Mbatizaji alivyotamka!” Basi akaendela kueleza kwamba tukiisha “kubatizwa kwa moto” tutajaa shauku na ari ya kumtumikia Mungu. Hatimaye akaita watu wafike mbele, wale waliotaka “kubatizwa kwa moto”.
Kibaya ni hiki: Mhubiri huyo alifanya kosa la kawaida kabisa – la kuondoa mstari katika mantiki yake.
Kwani Yohana Mbatizaji alimaanisha nini aliposema Yesu angewabatiza watu kwa moto? Ili tupate jibu, tunachohitaji ni kusoma mistari miwili kabla ya mstari huo, na mstari mmoja baada ya mstari huo. Hebu tuanze na mistari miwili kabla. Yohana alisema hivi:
walikuwa Wayahudi, waliodhani kwamba wokovu wao ulitokana na ukoo wao. Hivyo, mahubiri ya Yohana yalikuwa uinjilisti.
Pili: Tunajifunza kwamba Yohana alikuwa anaonya kwamba watu wasio-okoka wako katika hatari ya kutupwa katika moto. Ni sahihi kufikiri kwamba “moto” anaosema Yohana katika mstari wa 10 ndiyo huo huo aliosema habari zake katika mstari wa 11.
Hayo yanakuwa wazi zaidi tukisoma mstari wa 12.
Kutokana na mistari inayotangulia, bila shaka Yohana katika mstari wa 11 alimaanisha kwamba Yesu angewabatiza watu na Roho Mtakatifu kama ni waamini, au kwa moto, kama si waamini. Kwa kuwa ni hivyo, haipaswi mtu awahubirie Wakristo kwamba wanahitaji kubatizwa kwa moto!
Tukiachana na mantiki hiyo ya mistari husika, tutazame pia Agano Jipya lote. Je, kuna mfano wowote katika Matendo ya Mitume, mahali ambapo Wakristo wanatajwa kwamba walibatizwa “kwa moto”? Hapana. Kinachokaribia ni maelezo ya Luka kuhusu siku ya Pentekoste, wakati wanafunzi walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu na ndimi za moto zikaonekana kwa muda juu ya vichwa vyao. Lakini Luka hakusema kwamba huo ulikuwa ni “ubatizo kwa moto”. Zaidi ya hayo – je, tunaweza kupata fundisho au ushauri wowote katika nyaraka za mitume kwamba Wakristo wabatizwe “kwa moto”? Hapana. Basi, ni salama kabisa kusema kwamba hakuna Mkristo anayetakiwa kutafuta ubatizo wa moto.
Kwa mfano: Maneno ya Paulo kuhusu wokovu kupatikana kwa neema na si matendo, yapatikanayo katika Waefeso 2:8 yametumiwa vibaya kukuza injili ya uongo, na ni kwa sababu mantiki imepuuzwa. Paulo aliandika hivi:
Kwanza: Hebu tufikiri fungu lenyewe zima linasema nini. Paulo hasemi kwamba tumeokolewa kwa neema. Anasema tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani. Imani ni sehemu muhimu sana ya wokovu kama neema. Maandiko yanasema kwamba imani pasipo matendo haifai – imekufa – na haiwezi kuokoa (angalia Yakobo 2:14-26). Kwa hiyo, Paulo hafundishi kwamba utakatifu hauna maana kwa wokovu. Anachosema ni kwamba, juhudi zetu hazituokoi – msingi wa wokovu wetu ni neema ya Mungu. Yaani – tusingeweza kuokoka bila neema ya Mungu, lakini pia, ni wakati tunapoitikia neema ya Mungu kwa imani ndipo wokovu unapotokea katika maisha yetu. Matokeo ya wokovu kila mara ni utii, ambalo ni tunda la imani halisi. Tukitazama mantiki – mstari unaofuata tu – jambo hilo linathibitishwa. Paulo anasema hivi:
Lakini, wale waliopasua maneno ya Paulo kutoka mantiki yake, wameunda kitu chao, kinachofanana hivi:
Tukisoma kidogo tu mantiki ya maneno ya Paulo, tutagundua pia kwamba hali halisi huko Efeso ilikuwa sawa na sehemu zingine alizohubiri Paulo. Yaani: Wayahudi walikuwa wanawafundisha waongofu wapya wa Paulo wasiokuwa Wayahudi kwamba iliwabidi kutahiriwa na kushika baadhi ya sheria za kidini za Torati ya Musa kama walitaka kuokoka. Basi, kutokana na mantiki hiyo ya tohara na matendo ya kidini, Paulo aliandika juu ya “matendo” yasiyotuokoa (ona Waefeso 2:11-22).
Tukisoma zaidi kidogo na kupata mantiki ya barua ya Paulo nzima kwa Waefeso, tutaona waziwazi kabisa kwamba Paulo aliamini utakatifu ni lazima kwa wokovu.
Kiini cha barua nzima ya Paulo kwa Wagalatia ni: “Wokovu kwa imani, si kwa matendo ya Torati”. Lakini je, Paulo alikusudia kwamba wasomaji wake wafikie uamuzi kuwa utakatifu si kitu cha lazima ili mtu aingie katika ufalme wa Mungu? Hapana kamwe!
Kwanza: Tunaona kwamba kwa mara nyingine tena Paulo alikuwa anapambana na Wayahudi walikuja Galatia na kuwafundisha waongofu wapya kwamba wasingewokoka kama wasingetahiriwa na kuishika Torati ya Musa. Paulo anataja swala la tohara mara kadha katika barua yake, maana hilo linaonekana kuwa ndiyo mkazo mkuu kwa Wayahudi washika sheria (tazama 2:3, 7-9, 12; 5:2-3, 6, 11; 6:12-13, 15). Paulo hakusumbuliwa na waamini Wagalatia kuwa watii mno kwa amri za Kristo. Yeye alisumbuliwa na ukweli kwamba walikuwa hawamwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wao, badala yake, wanaweka imani yao kwenye tohara na juhudi zao dhaifu sana za kuishika Sheria ya Musa.
Tunapotafakari mantiki nzima ya barua ya Paulo kwa Wagalatia, tunaona akiandika hivi katika sura ya 5:
Kwa mfano: Niliwahi kumsikia mhubiri mmoja akitangaza kwamba hatupaswi kutaja ghadhabu ya Mungu tunapohubiri Injili kwa sababu Biblia inasema hivi: “…wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu” (Warumi 2:4b). Basi, kulingana na huyo ndugu, njia inayofaa ya kutangaza Injili ni kusema habari za upendo na wema wa Mungu tu. Hayo yangewavuta watu watubu.
Lakini, unaposoma mantiki ya mstari huo ambao mhubiri aliutaja – yaani sura ya pili ya kitabu cha Warumi – tunagundua kwamba unazungukwa na Maandiko kuhusu hukumu ya Mungu na hasira Yake takatifu! Mantiki yake inaonyesha kwamba hakuna uwezekano kuwa Paulo alikusudia kusema hayo aliyosema huyo mhubiri. Hebu ona.
Yesu alikuwa anazungumza na wanafunzi Wake (ona Mathayo 5:1-2), watu ambao walichojua kuhusu Neno la Mungu ni mambo waliyofundishwa na waandishi na Mafarisayo katika masinagogi yao. Huko walisikia sheria ya Mungu ikitajw akwamba, “Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.” Maana ya amri hiyo ilikuwa imegeuzwa sana na waandishi na Mafarisayo kwa sababu ya kupuuzia mantiki yake. Mungu hakutaka amri hiyo itafsiriwe kwamba ni sharti watu wajaribu kulipiza kisasi kila mara kwa makosa madogo. Katika Torati ya Musa Yeye alisema kisasi ni chake (ona Kumbu. 32:35), na kwamba watu Wake wawatendee mema adui zao (tazama Kutoka 23:4-5). Lakini waandishi na Mafarisayo walipuuza amri hizo na kutengeneza tafsiri yao wenyewe ya maneno ya Mungu ya “jicho kwa jicho”, iliyowapa wao haki inayofaa ya kujilipiza kisasi kibinafsi.[3] Walipuuza mantiki.
Agizo la Mungu kuhusu “jicho kwa jicho, na jino kwa jino” linapatikana katika mantiki ya amri Zake zenye kutoa haki inayostahili katika mahakama za Israeli (tazama Kutoka 21:22-24; Kumbu. 19:15-21). Kuwa na utaratibu wa mahakama ni ufunuo tosha wa jinsi Mungu asivyounga mkono kisasi cha mtu binafsi. Mahakimu wasio na upendeleo wanaotazama ushahidi husika wana uwezo zaidi wa kutoa haki kuliko watu binafsi ambao wamekosewa na wenye mtazamo wa kibinafsi. Mungua natazamia kwamba mahakama na mahakimu watatoa adhabu zinazostahili hatia, bila upendeleo. Ndiyo sababu ni “jicho kwa jicho, jino kwa jino”.
Basi, tunaweza kulinganisha maneno hayo ambayo mwanzoni yalionekana yanapingana. Yesu alikuwa anawasaidia wasikilizaji Wake waliokuwa wamefundishwa uongo maisha yao yote waelewe mapenzi ya Mungu ya kweli kwa ajili yao kuhusu kisasi cha binafsi. Hayo yalikuwa yamefunuliwa tayari katika Torati ya Musa, lakini yalipotoshwa na Mafairsayo. Hakuwa anakwenda kinyume na Torati alyompa Musa. Alikuwa anadhihirisha maana yake halisi – ile iliyokusudiwa.
Sasa hilo linatusaidia na sisi kuelewa vizuri kile ambacho Yesu anatazamia kutoka kwetu kuhusu kutokuelewana kunakoweza kusababisha twende mahakamani. Mungu hakuwatazamia Waisraeli kupuuzia kila kosa walilotendewa na Waisraeli wenzao. Ingekuwa hivyo asingeweka utaratibu wa mahakama. Vivyo hivyo, Mungu hatazamii Wakristo kupuuzia kila kosa wanalotendewa na waamini wanzao (au wasioamini basi). Agano Jipya linapendekeza kwamba Wakristo wasioweza kuelewana wapate msaada wa kupatanishwa na waamini wenzao (ona 1Wakorintho 6:1-6). Wala hakuna kosa kwa Mkristo kumpeleka asiyeamini mahakamani, kwa habari ya kutokuelewana kwa hali ya juu. Mfano ni kama kutolewa jicho au jino! Makosa madogo ni kama vile kupigwa kofi shavuni, au kunyang’anywa kitu kidogo (kama vile shati lako), au kulazimishwa kwenda maili moja. Mungu anataka watu Wake wamwige Yeye na kuonyesha neema isiyo ya kawaida kwa wenye dhambi na waovu wasiofikiri.
Wamekuwepo waamini wenye nia njema tu ambao, kwa kudhani kwamba wanamtii Yesu, wanakataa kuwashtaki wale ambao wameshikwa wakiwaibia. Walifikiri kwamba wanageuza “shavu la pili – kumbe wanamwezesha mwizi kuiba tena, wakimfundisha kwamba hakuna adhabu kwa kosa kama hilo. Wakristo wa namna hiyo hawaenendi kwa kuwapenda wengine ambao wataibiwa mali na mwizi huyo huyo! Mungu anataka wezi wapate haki na kutubu. Lakini, mtu anapokukosea kwa njia ndogo kama kukupiga kofi, usimpeleke mahakamani au kumpiga kofi na wewe. Mwonyeshe rehema na upendo.
Ni wazi lakini kwamba Wakristo wa kwanza – ambao wote walikuwa Wayahudi walio-ongoka – waliendelea kufuata sheria za vyakula za agano la kale kwa sababu ya desturi zao (ona Matendo 10:9-14). Na watu wa Mataifa walipoanza kumwamini Yesu, wale Wayahudi Wakristo wa mwanzo waliwaambia wafuate sheria za vyakula za Musa kwa kiasi fulani kwa sababu tu ya kuwajali Wayahudi jirani ambao wangekwazwa (ona Matendo 15:1-21). Kwa hiyo, hakuna kosa lolote kwa Wakristo kufuata sheria za vyakula za Musa mradi tu wasizitumaini kwamba zitawaokoa au kuwapa haki fulani.
Baadhi ya Wakristo wa kwanza walishawishika pia kwamba ni kosa kula nyama au vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Paulo aliwashauri waamini waliokuwa na mawazo tofauti (kama yeye) wafuate kanuni ya upendo kwa ndugu zao wenye “imani dhaifu (tazama Warumi 14:1). Alishauri wasifanye chochote kitakachowakwaza dhamiri zao. Kama mtu ataacha kula vyakula kwa sababu ya kumwamini Mungu (hata kama imani yake haina msingi), anatakiwa kupongezwa kwa msimamo wake badala ya kulaumiwa kwa kutokuelewa kwake. Vivyo hivyo – wale wanaojiepusha na vyakula fulani kwa sababu ya imani zao binafsi wasiwahukumu wale wasiojiepusha. Wote wawili waenende kwa upendo, maana hilo linaagizwa na Mungu (tazama Warumi 14:1-23).
Vyovyote vile – Kwa sababu Biblia ni ufunuo unaoendelea, tunapaswa kutafsiri ufunuo wa zamani (yaani, Agano la Kale) kwa mwanga wa ufunuo mpya zaidi (yaani, Agano Jipya). Hakuna ufunuo wowote wa Mungu ambao unapingana – siku zote unasaidiana na kukubaliana.
Ifuatayo ni mfano michache kuhusu jinsi habari za kihistoria au utamaduni zinavyoweza kutusaidia tusichanganyikiwe tunaposoma Biblia.
1) Wakati mwingine katika Maandiko tunasoma kuhusu watu kupanda darini (au orofani) – tazama Matendo 10:9 – au kutoboa dari (tazama Marko 2:4). Itasaidia tukijua kwamba kwa kawaida huko Israeli nyumba zilikuwa na mapaa yaliyonyooka, na kwamba pembeni mwa kila nyumba kulikuwa na ngazi za kupandia huko darini. Tusipojua hilo tutafikiri juu ya mtu katika Biblia akihangaika kuparamia bati la msonge huku akipata shida mahali pa kujishikilia!
2) Tunasoma katika Marko 11:12-14 kwamba Yesu aliulaani mtini kwa sababu haukuwa na tini, japo “hakikuwa kipindi cha tini”. Inasaidia tukijua kwamba kwa kawaida miti ya mtini huwa na tini chache hata kama si wakati wake. Basi, Yesu hakukosea kuwa na matazamio aliyokuwa nayo.
3) Tunasoma katika Luka 7:37-48 kuhusu mwanamke aliyeingia nyumbani mwa Farisayo, mahali Yesu alipokuwa akila chakula. Maandiko yanasema alisimama nyuma ya Yesu akilia, kisha akaanza kulowesha miguu ya Yesu kwa machozi yake, kuipangusa na nywele zake, na kuibusu na kuipaka marhamu. Itatushangaza kwamba iliwezekanaje hayo yote kufanikiwa huku Yesu ameketi mezani anakula chakula. Je, aliingia chini ya meza? Alifanikiwaje kuiepuka miguu ya wale walaji wengine wote?
Jibu ni kwamba katika siku zile, kawaida ilikuwa kula chakula ukiwa umejilaza chini kwa ubavu mmoja karibu na meza fupi. Mkono mmoja ulitumiwa kujitegemeza na mwingine kujilisha. Yesu akiwa hivyo, aliweza kuabudiwa na kutendewa yote hayo na yule mwanamke.
Hii pia inatusaidia kuelewa jinsi Yohana alivyoweza kuegama kifuani pa Yesu wakati wa Chakula cha Mwisho, na kumwuliza swali. Yohana alikuwa amejilaza kwa ubavu, mgongo wake ukimkabili Yesu. Basi ilikuwa rahisi tu kwake kuegama kifuani pa Yesu na kumwuliza swali bila kumsumbua mtu mwingine (ona Yohana 13:23-25). Ile picha maarufu ya Chakula cha Mwisho iliyochorwa na Da Vinci, ambapo Yesu na wanafunzi wake wameketi mezani – sita upande huu na sita upande huu – inaonyesha kutoelewa Biblia kwa mchoraji huyo. Hapo alihitaji kuelezwa kidogo mantiki ya kihistoria!
Hili ni swali zuri tunaloweza kujibu tukitumia kanuni nzuri tu za kutafsiri, pamoja na kutazama mantiki ya kitamaduni.
Hebu kwanza tutazame zuio la Biblia juu ya wanawake kuvaa mavazi ya wanaume (na kinyume chake pia).
Hapana – hilo haliwezi kuwa kusudi Lake kwa sababu wakati huo wanaume wa Israeli hawakuwa wanavaa suruali. Suruali hazikuhesabiwa kuwa mavazi ya kiume au ya kike, wala ya mtu yeyote. Ukweli ni kwamba, mavazi yaliyovaliwa siku za Biblia yalifanana sana na mavazi ya kike ya siku hizi! Hiyo ni habari kidogo tu ya kihistoria na kitamaduni, inayotusaidia kutafsiri vizuri kile ambacho Mungu anasema.
Sasa – kusudi la Mungu lilikuwa nini?
Tunasoma kwamba yeyote aliyevaa mavazi yasiyo ya jinsia yake alikuwa chukizo kwa BWANA. Hilo ni jambo zito. Je, kama mwanamume akichukua kitambaa cha mwanamke akakivaa kichwani kwa nukta tatu anakuwa chukizo kwa Mungu? Hapana, si hivyo.
Inaonekana kwamba, kitu alichokuwa anapinga Mungu ni watu kuvaa makusudi ili waonekane kuwa ni wa jinsia nyingine na huku si hivyo. Mbona mtu atake kufanya hivyo? Pengine ni kwa sababu alitazamia kumshawishi mwingine wa jinsia ile kimapenzi – ufuska. Kama ni hivyo, bila shaka tunaanza kuelewa jinsi tendo hilo linavyoweza kuwa chukizo kwa Mungu.
Basi, haiwezekani mtu kuamua kwamba ni makosa kwa wanawake kuvaa suruali kutokana na maneno ya Kumbukumbu 22:5, isipokuwa kama atavaa ili kujifanya mwanamume, kwa lengo la kuwashawishi wanaume kimapenzi. Akivaa na aendelee kuonekana kama mwnaamke, hafanyi dhambi kwa kuvaa suruali.
Ila, Maandiko yanafundisha kwamba wanawake wavae mavazi ya staha (ona 1Timo. 2:9). Basi, suruali zenye kubana sana kiasi cha kuonyesha umbo hazifai. Hata magauni na sketi na blauzi za namna hiyo hazifai, kwa sababu zinaweza kusababisha wanaume kutamani. Mavazi mengi yanayovaliwa na wanawake hadharani katika nchi za Magharibi (na hata Afrika!) hayafai kabisa, na ni yale yanayovaliwa na makahaba katika nchi zingine. Hakuna mwanamke Mkristo anayetakiwa kuvaa mavazi hadharani yenye kuonyesha mwili, au kwa lengo la “kuvutia”.
Pia inanishangaza kwamba sijawahi kuulizwa swali kama hilo na watumishi wanawake katika nchi ya Myanmar, ambako kimila wanaume huvaa vazi linalofanana na sketi liitwalo longgi. Ni kwamba mavazi ya kike na ya kiume hutofautiana kutoka mila hadi nyingine, hivyo tunapaswa kuwa waangalifu tusilazimishe utamaduni wetu kuingia katika Biblia.
Mwisho: Nashangaa ni kwa nini wanaume wengi wasiotaka wanawake wavae suruali kwa sababu ya Kumbukumbu 22:5 hawaoni sababu ya kujipima wenyewe na Walawi 19:27. Tunasoma hivi:
Labda maelezo kidogo ya kihistoria yatasaidia kuelewa kusudi la Mungu katika Walawi 19:27. Kuharibu pembe za ndevu ulikuwa utaratibu wa kidini wa kipagani katika kuabudu sanamu. Mungu hakutaka watu wake waonekane kuwa wamejitoa kwa miungu ya kipagani.
Katika mafungu mengi ya Maandiko, maneno ya watu ambayo hayajavuviwa yameandikwa. Kwa hiyo, hatupaswi kufikiri kwamba kila kitu kilichosemwa na watu kilichoandikwa katika Biblia kimevuviwa na Mungu.
Kwa mfano: Watu wengi hukosea kwa kutumia maneno ya Ayubu na rafiki zake kana kwamba ni maneno yaliyovuviwa ya Mungu. Kuna sababu mbili kubwa zenye kuonyesha kwamba ni kosa. Kwanza: Ayubu na rafiki zake walibishana kwa sura thelathini na nne. Hawakukubaliana. Basi, si kila walichosema kinachoweza kuhesabiwa kuwa Neno la Mungu lililovuviwa kwa sababu Mungu hajipingi Mwenyewe.
Pili: Mwishoni mwa kitabu cha Ayubu, Mungu mwenyewe anazungumza, naye anamkemea Ayubu na rafiki zake kwa kusema mambo ambayo hayakuwa sahihi (ona Ayubu 38 hadi 42).
Tunapaswa kuwa makini tunaposoma Agano Jipya pia. Mara kadhaa Paulo anasema wazi kwamba baadhi ya mafungu aliyoandika ni mawazo yake au maoni yake binafsi (ona 1Wakorintho 7:12, 25-26, 40).
Mfano: Wengi hudai hii ahadi ipatikanayo katika Zaburi mojawapo, wakiamini ni yao.
Cha kushangaza ni kwamba, wale wenye kuhubiri juu ya kurudishiwa mara mia hukazia sana nyumba na mashamba. Hawataji sana kuhusu watoto na udhia, ambavyo pia vimetajwa! Yesu hakumaanisha kwamba watakaoacha nyumba zao watapata nyumba mia moja badala yake. Aliahidi tu kwamba watu wakiacha familia zao na nyumba zao, wanafamilia wao wapya kiroho watawakaribisha majumbani mwao kukaa. Wanafunzi wa kweli hawajali sana kuhusu kumiliki vitu maana hawana chochote chao – wao ni mawakili tu wa vitu vya Mungu.
Angalia mfano huu niliokutana nao hivi karibuni, wenye kuonyesha jinsi unavyoweza kulazimisha itikadi yako iingie kwenye mstari. Mwalimu mmoja alianza kwa kusoma maneno maarufu sana ya Yesu – Mathayo 11:28-29.
Lakini – hiyo ndiyo maana aliyokusudia Yesu? Hapana. Huko ni kulazimisha maana kwenye andiko ambayo haipo wala haidhaniwi. Yesu hakusema anatoa mapumziko aina mbili. Alikuwa anatoa pumziko moja kwa wale waliochoka na wenye kulemewa, na njia pekee ya kupata pumziko hilo ni kwa kuvaa nira ya Yesu – yaani, kujinyenyekeza Kwake. Hiyo ndiyo maana ya Yesu.
Mbona huyo mwalimu akatoa tafsiri hiyo? Kwa sababu maana halisi ya fungu hilo haikulingana na imani aliyo nayo yeye – kwamba kuna aina mbili za Wakristo waendao mbinguni – waamini, na wanafunzi. Hivyo hakutafsiri fungu hilo kwa moyo ulio wazi na ukweli.
Kama ambavyo tumeona huko nyuma katika mafungu mengi tu ya Maandiko tulipochambua itikadi hiyo, tafsiri ya mwalimu hiyo hailingani na mantiki ya mafundisho mengine ya Yesu. Hakuna popote katika Agano Jipya tunapojifunza kwamba kuna aina mbili za Wakristo wanaokwenda mbinguni – waamini na wanafunzi. Waamini wote wa kweli ni wanafunzi. Wasiokuwa wanafunzi si waamini. Uanafunzi ni tunda la imani ya kweli.
Basi, tujitahidi kusoma Biblia kwa mioyo iliyo wazi, iliyo safi. Tukifanya hivyo, tutampenda Kristo zaidi, na kumtii.
Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia (1Timo. 4:16. Maneno mepesi kukazia).Kila mtumishi anatakiwa kutilia maanani ushauri huu, akiwa makini sana kuhusu yeye mwenyewe kwanza – yaani, kuhakikisha kwamba yeye ni mfano wa utauwa kwa wengine.
Cha pili – awe makini sana kuhusu mafundisho yake, kwa sababu wokovu wake wa milele na wa wanaomsikiliza unategemea anachofundisha, kama Paulo alivyoandika katika mstari huo hapo juu. Mtumishi akifuata mafundisho ya uongo, au akipuuza kuwaambia watu ukweli, matokeo ni hasara ya milele kwake na kwa wengine.
Ila – hakuna kujitetea kwa mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi, kama atafundisha uongo, maana Mungu amempa yeye Roho Mtakatifu na Neno Lake ili kumwongoza katika kweli. Watumishi wenye makusudi mabaya mara nyingi hurudia kama kasuku mafundisho yanayopendwa na watu, yenye kutolewa na waalimu wengine. Wao hawajifunzi Neno ili wapate kitu cha kutoa, na inakuwa rahisi kwao kupotoka katika mafundisho yao na imani zao. Ulinzi kinyume cha hayo ni mtumishi kusafisha moyo wake, akihakikisha kwamba kusudi lake moyoni ni (1) kumpendeza Mungu, na (2) kuwasaidia watu wawe tayari kusimama mbele za Yesu, badala ya kutaka kutajirika kibinafsi, au kuwa na uwezo au kuwa maarufu. Tena, lazima ajifunze kwa bidii sana Neno la Mungu ili awe na ufahamu kamili na wenye usahihi. Paulo alimwandikia Timoteo tena, akasema hivi:
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli (2Timo. 2:15).Kusoma, kujifunza na kutafakari Neno la Mungu iwe ni kawaida kwa mtumishi kufanya kila wakati. Roho Mtakatifu atamsaidia kuelewa vizuri zaidi Neno la Mungu atakapojifunza kwa bidii. Hiyo itahakikisha kulitumia “kwa halali neno la kweli”. Tatizo moja kubwa katika kanisa siku hizi ni kwamba watumishi wanafasiri vibaya Neno la Mungu, na wanapotosha watu wanaowafundisha. Hii ni hatari sana. Yakobo alionya hivi:
Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi (Yakobo 3:1).Basi, ni muhimu kwamba mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi ajue jinsi ya kufasiri sawasawa Neno la Mungu, huku lengo lake likiwa kuelewa ipasavyo maandiko yoyote na kuyafafanua ili watu wapate maana yake halisi.
Kufasiri sawasawa Neno la Mungu hufanywa sawa tu na kufasiri sawasawa maneno ya mtu. Tukitaka kuelewa vizuri maana iliyokusudiwa ya mwandishi yeyote au msemaji tunayemsikiliza, inabidi tufuate sheria fulani za ufasiri, ambazo msingi wake ni akili tu ya kawaida. Katika sura hii, tutatazama kanuni tatu muhimu za kufasiri Biblia ipasavyo. Ni hizi zifuatazo: (1) Soma na akili timamu, (2) Soma ukizingatia mantiki, na (3) Soma na moyo ulio wazi.
Kanuni ya kwanza: Soma na akili timamu. Elewa uliyosoma kama yalivyoandikwa isipokuwa kama ni dhahiri kwamba yalikusudiwa kueleweka kama mfano.
Biblia ni kama maandiko mengine. Imejaa lugha za mifano. Ukisoma sehemu kama hizo, zielewe hivyo hivyo.Mlinganisho huonyesha jinsi vitu viwili ambavyo ni tofauti kabisa, vinavyofanana. Katika Maandiko utakutana na hili mara nyingi sana. Mfano mmoja ni maneno ya Kristo wakati wa Chakula cha Mwisho na wanafunzi Wake.
Nao walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake akasema, ‘Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu’. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa akisema, ‘Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi’ (Mathayo 26:26-28).Je, Yesu kweli alimaanisha kwamba mkate aliowapa wanafunzi Wake ulikuwa mwili Wake halisi na kwamba ile divai waliyokunywa ilikuwa damu Yake halisi? Kufikiri kidogo tu kutaonyesha kwamba Sivyo. Maandiko yanasema wazi kwamba Yesu aliwapa mkate na divai, na hayasemi kwamba vitu hivyo vilibadilika wakati wowote na kuwa nyama na damu halisi. Hata Petro na Yohana hawasemi hivyo katika nyaraka zao wakati wowote, na wao walikuwepo kwenye Chakula hicho. Tena, haiwezekani kwamba wanafunzi wangekubali kujihusisha na ulaji wa nyama na damu ya mwanadamu!
Kuna wanaotoa hoja hivi: “Lakini, Yesu alisema kwamba mkate na divai ni mwili Wake na damu Yake. Mimi nitaamini alichosema Yesu!”
Sawa. Kuna wakati ambapo Yesu pia alisema ni mlango (Yohana 10:9). Je, alifanyika mlango halisi, wenye komeo na bawabu na kitasa? Wakati mwingine Yesu alisema Yeye ni mzabibu, na sisi ni matawi (Yohana 15:5). Je, Yesu alifanyika mzabibu halisi? Je, sisi tumefanyika matawi halisi ya mzabibu? Wakati mwingine Yesu akasema ni nuru ya ulimwengu na chakula kilichoshuka kutoka mbinguni (ona Yohana 9:5; 6:41). Je, Yesu ndiye mwangaza wa jua siku hizi na boflo ya mkate?
Basi – hizo zote ni lugha za mfano ambazo ni mlinganisho wa vitu viwili ambavyo ni tofauti kabisa, vyenye kufanana kwa kiasi fulani. Kwa namna fulani, Yesu ni kama mlango na mzabibu. Maneno ya Yesu wakati wa Chakula cha Mwisho ni mifano pia. Divai ilikuwa kama damu Yake (kwa kiasi fulani). Mkate ulikuwa kama mwili Wake (kwa kiasi fulani).
Mifano Ya Kristo
Mifano ya Kristo ni fungu lingine. Hiyo hufundisha masomo ya kiroho pia kwa kulinganisha vitu viwili visivyofanana. Ila, yenyewe ina neno umefanana na, au ni kama. Ni muhimu sana tukumbuke hilo tunapoifafanua, vinginevyo tutafanya kosa la kutafuta maana katika kila kitu kidogo kinachotajwa katika mfano. Mifano hufikia mwisho wa kufanana na tofauti zinaanza. Kwa mfano: Nikimwambia mke wangu hivi: “Macho yako ni kama vidimbwi vya maji” maana yake ni kwamba macho yake yanapendeza, yanavutia, na yana kina. Simaanishi kwamba kuna samaki ndani yake nao huogelea humo, wala kwamba ndege hutua hapo, wala kwamba wakati wa majira ya barafu yanaganda!Hebu tutazame mifano mitatu ya Yesu, tukianza na Mfano wa Juya.
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna. Hata lilipojaa, walilivuta pwani wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno (Mathayo 13:47-50).Sasa swali – Je, ufalme wa mbinguni na juya ni kitu kimoja? Hapana kamwe! Vitu hivyo viwili vinatofautiana sana, lakini vinafanana kidogo. Kama ambavyo samaki wanapimwa na kutenganishwa katika makundi mawili – wanaotakiwa na wasiotakiwa – wanapotoka kwenye juya, ndivyo itakavyokuwa katika ufalme wa Mungu. Siku moja, waovu na wenye haki – ambao kwa sasa wanaishi pamoja wote – watatenganishwa. Lakini hapo ndipo mwisho wa kufanana. Samaki huogelea; wanadamu wanatembea. Wavuvi wanatenganisha samaki. Malaika watawatenganisha waovu na wenye haki. Samaki wanapimwa utamu wao baada ya kupikwa. Watu watapimwa kumtii Mungu au kutokumtii. Samaki wazuri wanawekwa katika vyombo, na wale wabaya wanatupiliwa mbali. Wenye haki wataurithi ufalme wa Mungu na waovu watatupwa jehanamu.
Mfano huu ni mzuri wa kuonyesha jinsi ambavyo kila mlinganisho usivyofaa kabisa kueleza kitu kwa sababu hatimaye vitu vile vinavyolinganishwa hufikia mahali pa kutofautiana. Hatupaswi kwenda zaidi ya kusudi la msemaji, yaani kudhani kwamba tofauti zote ndiyo kufanana. Kwa mfano: Wote tunajua kwamba “samaki wazuri” huishia kupikwa kwa moto, na “samaki wabaya” hurudi majini. Yesu hakutaja hayo, maana yangekuwa kinyume cha kusudi Lake.
Mfano huu haufundishi mkakati wa “uinjilisti kwa juya” – kwamba tujaribu kumkokota kila mmoja kanisani – mwema na mbaya – akitaka asitake! Mfano huu haufundishi kwamba ufuoni mwa bahari ndipo mahali panapofaa kufanyia uinjilisti. Mfano huu hauthibitishi kwamba Unyakuo wa kanisa utatokea mwisho wa kipindi cha dhiki kuu. Wala mfano huu haufundishi kwamba wokovu wetu ni chaguo la Mungu kwa kuwa samaki waliochaguliwa katika mfano hawakuhusika kwa njia yoyote na kuchaguliwa kwao. Usilazimishe maana isiyostahili katika mifano ya Yesu!
Kuwa Tayari
Angalia mfano mwingine maarufu sana wa Yesu – Mfano wa Wanawali Kumi.Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, ‘Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki’. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, ‘Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.’ Lakini wale wenye busara wakawajibu wakisema, ‘Sivyo, hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie’. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine wakasema, ‘Bwana, Bwana, utufungulie’. Akajibu akasema, ‘Amin nawaambia, siwajui ninyi’. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa (Mathayo 25:1-13).Je, somo kuu la mfano huu ni nini? Linapatikana katika maneno ya mwisho: Kaeni katika hali ya kusubiri kurudi kwa Bwana, maana anaweza kuchelewa kuliko inavyotazamia.
Kama nilivyokwisha sema huko nyuma, Yesu aliwaambia wanafunzi Wake wa karibu sana mfano huu (ona Mathayo 24:3; Marko 13:3), waliokuwa wanamfuata kwa uaminifu sana wakati huo. Basi – kinachosemwa wazi kabisa katika mfano huu ni kwamba iliwezekana kwa Petro, Yakobo, Yohana na Andrea kutokuwa tayari wakati Yesu atakaporudi. Hii ndiyo sababu alikuwa anawaonya. Basi, mfano huu unafundisha kwamba upo uwezekano kwa wale walio tayari sasa kwa ajili ya kurudi kwa Kristo kutokuwa tayari wakati atakaporudi. Wanawali wote kumi walikuwa tayari kimsingi, lakini watano wakawa hawako tayari. Kama bwana arusi angefika mapema zaidi, wote kumi wangeingia katika karamu ya arusi.
Lakini, nini maana ya kuwepo kwa wanawali watano wapumbavu na watano wenye busara? Je, maana yake ni kwamba katika waamini wote, nusu tu ndiyo watakuwa tayari wakati Kristo atakaporudi? Hapana.
Nini maana ya mafuta? Je, ni mfano wa Roho Mtakatifu? Hapana. Je, ni udhihirisho kwetu kwamba wale tu waliobatizwa na Roho Mtakatifu ndiyo watakaoingia mbinguni? Hapana.
Je, kurudi kwa bwana arusi usiku wa manane kunaonyesha kwamba Yesu atarudi usiku wa manane? Hapana.
Mbona bwana arusi hakuwaita wale wanawali wenye busara ili wawatambue wenzao wapumbavu? Kama angefanya hivyo, ingeharibu hoja nzima ya mfano, maana wale wapumbavu hatimaye wangeingia arusini.
Labda tunaweza kusema kwamba, sawa na jinsi wale wanawali wapumbavu waliyvokosa taa na wakalala, ndivyo na waamini wapumbavu wanavyoanza kutembea katika giza la kiroho na kujikuta wamelala kiroho pia. Mwishowe, wanajifikisha mahali pa kuhukumiwa. Pengine arusi katika mfano huu inaweza kufananishwa na karamu ya arusi ya Mwanakondoo hapo baadaye – ila, hapo ndipo tunapoweza kufika bila ya kuanza kulazimisha maana nyingine katika mfano huu.
Kuzaa Matunda
Tafsiri mbovu kuliko zote niliyowahi kusikia ya mfano mmoja wa Kristo ni ile iliyotolewa na mhubiri mmoja, kuhusu Mfano wa Ngano na Magugu. Hebu kwanza tusome mfano wenyewe.Akawatolea mfano mwingie akisema, “Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, ‘Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?’ Akawaambia, ‘Adui ndiye aliyetenda hivi’. Watumwa wakamwambia, ‘Basi, wataka twende tukayakusanye?’ Akasema, ‘La, msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu’.” (Mathayo 13:24-30).Sasa, yule mhubiri akafafanua hivi:
Ni kweli kwamba ngano na magugu vinapochipua vinafanana. Hakuna awezaye kueleza kwamba hii ni ngano au haya ni magugu. Ndivyo ilivyo katika dunia na katika kanisa. Hakuna awezaye kueleza Wakristo wa kweli ni akina nani, na wasioamini n akina nani. Hawatambulikani kwa maisha yao, kwa sababu Wakristo wengi si watii kwa Kristo, sawa tu na wasioamini. Mungu tu ndiye ajuaye mioyo yao, Naye atawachambua wakati wa mwisho.Shida ni kwamba – wazo la Mfano wa Ngano na Magugu si hilo! Ukitazama kwa makini utaona kwamba mfano unafundisha kwamba waamini ni rahisi kuwatofautisha na wasioamini. Angalia – watumwa walitambua kwamba magugu yamepandwa wakati ngano ilipoanza kuzaa (angalia ms. 26). Magugu hayazai matunda yoyote, na hiyo ndiyo njia rahisi ya kuyatambua. Mimi naona kuna fundisho kubwa kwa Yesu kuamua kwamba magugu yasiyozaa yawe mfano wa waovu watakaousanywa mwisho wa wakati na kutupwa jehanamu.
Hoja kuu za mfano huu ni dhahiri kabisa: Waliookoka kweli huzaa matunda; wasiookoka hawazai matunda. Japo Mungu hawahukumu waovu sasa hivi wanapoishi miongoni mwa waliookoka, siku moja atawatenganisha kutoka kwa wenye haki na kuwatupa jehanamu.
Halafu – Yesu Mwenyewe alitoa maana ya mfano huu, hivyo hakuna haja ya mtu kutafuta maana nyingine kuliko aliyotoa.
Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie (Mathayo 13:36-43).
Kuzidisha Maana
Lugha nyingine inayotumiwa sana katika Biblia ni ile ya kuzidisha maana. Haya ni maneno yenye kuzidisha maana kwa makusudi ili kutilia mkazo kitu. Kwa mfano: Wakati mama anapomwambia mtoto wake hivi: “Nimekuita mara mia uje kula”, hapo maneno ya kuzidisha maana yametumiwa. Si kwamba ameitwa mara mia moja. Hebu tuone maneno ya Yesu katika Biblia yenye kuonyesha jambo hili.Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanamu (Mathayo 5:30).Kama Yesu alimaanisha kwamba kila mmoja wetu anayetenda dhambi kwa njia fulani akitumia mkono wa kuume aukate, basi wote tungekuwa hatuna mikono ya kuume! Ila ni hivi: Tatizo la dhambi halimo katika mikono yetu. Basi, maana hasa ya Yesu ilikuwa kutufundisha kwamba dhambi inaweza kutupeleka jehanamu, na njia ya kuepuka dhambi ni kuondoa majaribu na vitu vile vinavyoweza kutufanya tujikwae na kuanguka.
Kumfananisha Mungu na Mwanadamu
Aina ya tatu ya lugha inayopatikana katika Maandiko ni kumfananisha Mungu na mwanadamu. Yaani, Mungu anapewa tabia au sifa za kibinadamu ili kutusaidia kumwelewa zaidi. Kwa mfano: Tunasoma hivi katika Mwanzo 11:5 –BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.Hiyo ni lugha ya mfano kwa sababu, haiwezekani kwamba Mungu mwenye kujua yote alifanya safari kutoka mbinguni kwenda Babeli ili kuchunguza walichokuwa wanajenga wanadamu!
Wataalamu wengi wa Biblia wanahesabu kila tamko lenye kueleza viungo vya mwili wa Mungu kama vile mikono Yake, pua, macho na nywele kuwa ni lugha ya mfano. Wanasema haiwezekani Mungu Mwenyezi kuwa na viungo kama wanadamu.
Mimi sikubaliani nao kwa sababu kadhaa. Kwanza: Kwa sababu Maandiko yanasema wazi kabisa kwamba sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na sura Yake.
Mungu akasema, ‘Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu’ (Mwanzo 1:26. Maneno mepesi kukazia).Kuna wanaosema kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na sura Yake kwa sababu tunajitambua, tunawajibika kiadili, tuna uwezo wa kufikiri na kadhalika. Sawa, lakini tusome maneno yanayofanana sana na Mwanzo 1:26. Haya yanapatikana sura kadhaa baadaye.
Adamu alipoishi miaka mia na thelathini, alizaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Seti (Mwanzo 5:3. Maneno mepesi kukazia).Bila shaka maana yake ilikuwa hii: Seti alifanana kabisa na baba yake, kimwili. Kama hivyo ndivyo katika Mwanzo 5:3, bila shaka usemi huo unamaanisha hivyo hivyo katika Mwanzo 1:26. Tafsiri sahihi ya Maandiko na akili timamu zinasema hivyo.
Tena, tuna maelezo fulani kuhusu Mungu yatolewayo na waandishi wa Biblia waliomwona. Kwa mfano: Musa na wazee sabini na tatu wa Israeli walimwona Mungu!
Ndipo akakwea juu, Musa na Haruni na Nadabu na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli; wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake. Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa (Kutoka 24:9-11).Je, ungemwuliza Musa kama Mungu ana mikono na miguu, angesemaje?[2]
Nabii Danieli pia alipata maono ya Mungu Baba pamoja na Mungu Mwana.
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku [Mungu Baba] ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa … Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu [Mungu Mwana] akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote na taifa zote na lugha zote wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa (Danieli 7:9-10, 13-14).Kama ungemwuliza Danieli ikiwa Mungu ana nywele nyeupe na umbo la kumwezesha kuketi kwenye kiti cha enzi, angejibuje?
Basi, mimi ninaamini kwamba Mungu Baba ana umbo lenye utukufu sana linalofanana na umbo la mwanadamu, japo Yeye hana mwili wa nyama na damu – ni roho (ona Yohana 4:24).
Sasa – Utajuaje mafungu ya Maandiko yanayotakiwa kufasiriwa kama yalivyo, na yapi yafasiriwe kwamba ni mifano? Hilo ni rahisi tu kwa yeyote anayeweza kufikiri vizuri. Wewe tafsiri kila kitu kama kilivyo, isipokuwa kama kinaeleweka vingine. Kwa mfano: Vitabu vya manabii katika Agano la Kale pamoja na kitabu cha Ufunuo cha Agano Jipya vimejaa lugha ya mifano. Kuna ambayo imefafanuliwa, na mingine haijafafanuliwa. Lakini lugha za mifano zinazohusika si ngumu kutambua.
Kanuni ya pili: Soma ukizingatia mantiki. Kila fungu lazima litafsiriwe kulingana na yatokanayo katika mafungu jirani, na Biblia nzima. Mantiki ya kihistoria na kitamaduni lazima pia izingatiwe kila inapowezekana.
Huenda ikawa kusoma Maandiko bila ya kujali mantiki yake na kwamba Biblia nzima inasema nini juu ya hicho, ndiyo sababu kubwa ya Maandiko kutafsiriwa vibaya.Inawezekana kuifanya Biblia iseme chochote unachotaka iseme kwa kutenganisha maandiko na mantiki yake. Kwa mfano: Una habari kwamba Biblia inasema Mungu hayupo? Tunasoma hivi katika Zaburi ya 14, “Hakuna Mungu” (ms. 1). Lakini sasa, tukitaka kutafsiri maneno hayo kwa usahihi, lazima tuyasome katika mantiki yake. Ni hivi: “Mpumbavu amesema moyoni mwake, ‘Hakuna Mungu’.” (Zaburi 14:1. Maneno mepesi kukazia). Unaona? Mstari umekuwa na maana tofauti kabisa!
Mfano mwingine: Nilisikia mhubiri mmoja akihubiri juu ya Hitaji la Wakristo kubatizwa ‘katika moto’. Alianza ujumbe wake kwa kusoma maneno ya Yohana Mbatizaji katika Mathayo 3:11, kama ifuatavyo: “Kweli, mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba, lakini yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi. Sistahili hata kuvua viatu vyake. Huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (TLR).
Kutokana na mstari huo mmoja tu, alitengeneza ujumbe. Ninakumbuka akisema hivi: “Haitoshi kwamba umebatizwa na Roho Mtakatifu! Yesu anataka akubatize kwa moto pia, sawa na jinsi Yohana Mbatizaji alivyotamka!” Basi akaendela kueleza kwamba tukiisha “kubatizwa kwa moto” tutajaa shauku na ari ya kumtumikia Mungu. Hatimaye akaita watu wafike mbele, wale waliotaka “kubatizwa kwa moto”.
Kibaya ni hiki: Mhubiri huyo alifanya kosa la kawaida kabisa – la kuondoa mstari katika mantiki yake.
Kwani Yohana Mbatizaji alimaanisha nini aliposema Yesu angewabatiza watu kwa moto? Ili tupate jibu, tunachohitaji ni kusoma mistari miwili kabla ya mstari huo, na mstari mmoja baada ya mstari huo. Hebu tuanze na mistari miwili kabla. Yohana alisema hivi:
Msije mkadhani kwamba mtajiambia wenyewe, ‘Sisi ni wa uzao wa Ibrahimu’ kwa sababu nawaambia hivi: Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe haya. Tena, shoka limekwisha wekwa kwenye mashina ya miti. Basi, kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni (Mathayo 3:9-10, TLR. Maneno mepesi kukazia).Kwanza: Tunajifunza kwamba idadi fulani ya wasikilizaji wa Yohana siku hiyo
walikuwa Wayahudi, waliodhani kwamba wokovu wao ulitokana na ukoo wao. Hivyo, mahubiri ya Yohana yalikuwa uinjilisti.
Pili: Tunajifunza kwamba Yohana alikuwa anaonya kwamba watu wasio-okoka wako katika hatari ya kutupwa katika moto. Ni sahihi kufikiri kwamba “moto” anaosema Yohana katika mstari wa 10 ndiyo huo huo aliosema habari zake katika mstari wa 11.
Hayo yanakuwa wazi zaidi tukisoma mstari wa 12.
“Na pepeto Lake liko mkononi Mwake, naye atausafisha vizuri uwanda Wake wa kupuria nafaka. Ataikusanya ngano Yake ghalani, lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika” (Mathayo 3:12, TLR. Maneno mepesi kukazia).Katika mstari wa 10 na 12, moto unaotajwa na Yohana ni ule wa jehanamu. Katika mstari wa 12 anataja kwa lugha ya mfano kwamba Yesu atagawanya watu katika makundi mawili – ngano, ambayo ataikusanya “ghalani”, na makapi, ambayo atayachoma “kwa moto usiozimika”.
Kutokana na mistari inayotangulia, bila shaka Yohana katika mstari wa 11 alimaanisha kwamba Yesu angewabatiza watu na Roho Mtakatifu kama ni waamini, au kwa moto, kama si waamini. Kwa kuwa ni hivyo, haipaswi mtu awahubirie Wakristo kwamba wanahitaji kubatizwa kwa moto!
Tukiachana na mantiki hiyo ya mistari husika, tutazame pia Agano Jipya lote. Je, kuna mfano wowote katika Matendo ya Mitume, mahali ambapo Wakristo wanatajwa kwamba walibatizwa “kwa moto”? Hapana. Kinachokaribia ni maelezo ya Luka kuhusu siku ya Pentekoste, wakati wanafunzi walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu na ndimi za moto zikaonekana kwa muda juu ya vichwa vyao. Lakini Luka hakusema kwamba huo ulikuwa ni “ubatizo kwa moto”. Zaidi ya hayo – je, tunaweza kupata fundisho au ushauri wowote katika nyaraka za mitume kwamba Wakristo wabatizwe “kwa moto”? Hapana. Basi, ni salama kabisa kusema kwamba hakuna Mkristo anayetakiwa kutafuta ubatizo wa moto.
Injili Ya Uongo Iliyotoka Katika Maandiko
Mara nyingi, Injili yenyewe inatafsiriwa vibaya na wahubiri na waalimu ambao, kwa sababu wanashindwa kujali mantiki, wanatafsiri vibaya Maandiko. Mafundisho ya uongo kuhusu neema ya Mungu ni mengi sana kwa sababu hiyo.Kwa mfano: Maneno ya Paulo kuhusu wokovu kupatikana kwa neema na si matendo, yapatikanayo katika Waefeso 2:8 yametumiwa vibaya kukuza injili ya uongo, na ni kwa sababu mantiki imepuuzwa. Paulo aliandika hivi:
Mmeokolea kwa neema kwa njia ya imani. Wala hiyo haitokani na ninyi wenyewe – ni zawadi ya Mungu. Si kwa sababu ya matendo, mtu yeyote asije akajisifu (Waefeso 2:8-9, TLR).Wengi hutilia mkazo zaidi maneno ya Paulo kuhusu wokovu kuwa wa neema, kuwa zawadi, na si kwa ajili ya matendo. Kutokana na hilo, wanatoa fundisho kwamba wokovu na utakatifu havina uhusiano, kitu ambacho ni kinyume na ushahidi wa maandiko chungu nzima. Wengine hufikia hata mahali pa kusema kwamba hata toba si kitu cha lazima kwa wokovu kupatikana. Huo ni mfano mmoja mkubwa jinsi Maandiko yanavyotafsiriwa isivyo, kwa kupuuza mantiki.
Kwanza: Hebu tufikiri fungu lenyewe zima linasema nini. Paulo hasemi kwamba tumeokolewa kwa neema. Anasema tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani. Imani ni sehemu muhimu sana ya wokovu kama neema. Maandiko yanasema kwamba imani pasipo matendo haifai – imekufa – na haiwezi kuokoa (angalia Yakobo 2:14-26). Kwa hiyo, Paulo hafundishi kwamba utakatifu hauna maana kwa wokovu. Anachosema ni kwamba, juhudi zetu hazituokoi – msingi wa wokovu wetu ni neema ya Mungu. Yaani – tusingeweza kuokoka bila neema ya Mungu, lakini pia, ni wakati tunapoitikia neema ya Mungu kwa imani ndipo wokovu unapotokea katika maisha yetu. Matokeo ya wokovu kila mara ni utii, ambalo ni tunda la imani halisi. Tukitazama mantiki – mstari unaofuata tu – jambo hilo linathibitishwa. Paulo anasema hivi:
Kwa maana sisi tu kazi ya mikono Yake. Tumeumbwa katika Kristo Yesu tufanye matendo mema, ambayo Mungu aliyeandaa kabla, kwamba tuenende katika hayo (Waefeso 2:10, TLR).Sababu ya kuzaliwa upya kwa njia ya Roho Mtakatifu, ya kuwa viumbe vipya ndani ya Kristo, ni ili tuweze kuenenda katika matendo mema ya utii. Kwa hiyo, ‘mchoro’ wa wokovu anaoeleza Paulo ungefanana hivi:
Neema + Imani = Wokovu + Utii
Yaani – neema ukijumlisha na imani matokeo ni wokovu pamoja na utii. Neema ya Mungu inapoitikiwa kwa imani, matokeo kila wakati ni wokovu na matendo mema.Lakini, wale waliopasua maneno ya Paulo kutoka mantiki yake, wameunda kitu chao, kinachofanana hivi:
Neema + Imani – Utii = Wokovu
Yaani – neema ukijumlisha na imani bila utii husababisha wokovu. Kulingana na Biblia, huo ni uzushi – mafundisho potofu.Tukisoma kidogo tu mantiki ya maneno ya Paulo, tutagundua pia kwamba hali halisi huko Efeso ilikuwa sawa na sehemu zingine alizohubiri Paulo. Yaani: Wayahudi walikuwa wanawafundisha waongofu wapya wa Paulo wasiokuwa Wayahudi kwamba iliwabidi kutahiriwa na kushika baadhi ya sheria za kidini za Torati ya Musa kama walitaka kuokoka. Basi, kutokana na mantiki hiyo ya tohara na matendo ya kidini, Paulo aliandika juu ya “matendo” yasiyotuokoa (ona Waefeso 2:11-22).
Tukisoma zaidi kidogo na kupata mantiki ya barua ya Paulo nzima kwa Waefeso, tutaona waziwazi kabisa kwamba Paulo aliamini utakatifu ni lazima kwa wokovu.
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi. Bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadangaye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi (Waefeso 5:3-6. Maneno mepesi kukazia).Kama Paulo aliamini kwamba neema ya Mungu mwishowe ingemwokoa mtu ambaye ni mchafu na asiyetubu, au mwenye tamaa, asingeandika maneno hayo. Maana aliyokusudia Paulo kwa maneno yake katika Waefeso 2:8-9 inaweza kueleweka vizuri tu katika mantiki yabarua yake nzima kwa Waefeso.
Vurugu Ya Galatia
Maneno ya Paulo katika barua yake kwa Wagalatia nayo yametafsiriwa hivyo – nje ya mantiki yake. Matokeo ni kupotoka kwa Injili, jambo ambalo Paulo alitarajia kulisahihisha kwa barua yake kwa Wagalatia.Kiini cha barua nzima ya Paulo kwa Wagalatia ni: “Wokovu kwa imani, si kwa matendo ya Torati”. Lakini je, Paulo alikusudia kwamba wasomaji wake wafikie uamuzi kuwa utakatifu si kitu cha lazima ili mtu aingie katika ufalme wa Mungu? Hapana kamwe!
Kwanza: Tunaona kwamba kwa mara nyingine tena Paulo alikuwa anapambana na Wayahudi walikuja Galatia na kuwafundisha waongofu wapya kwamba wasingewokoka kama wasingetahiriwa na kuishika Torati ya Musa. Paulo anataja swala la tohara mara kadha katika barua yake, maana hilo linaonekana kuwa ndiyo mkazo mkuu kwa Wayahudi washika sheria (tazama 2:3, 7-9, 12; 5:2-3, 6, 11; 6:12-13, 15). Paulo hakusumbuliwa na waamini Wagalatia kuwa watii mno kwa amri za Kristo. Yeye alisumbuliwa na ukweli kwamba walikuwa hawamwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wao, badala yake, wanaweka imani yao kwenye tohara na juhudi zao dhaifu sana za kuishika Sheria ya Musa.
Tunapotafakari mantiki nzima ya barua ya Paulo kwa Wagalatia, tunaona akiandika hivi katika sura ya 5:
Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya: uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo. Katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:18-21. Maneno mepesi kukazia).Kama Paulo alitaka Wagalatia wajue kwamba wanaweza kupuuza utakatifu na bado waingie mbinguni, asingeandika maneno aliyoandika. Ujumbe wake si kwamba wasiokuwa watakatifu wanaweza kwenda mbinguni. Ujumbe wake ni kwamba wale wanaopuuza neema ya Mungu na kafara ya Kristo kwa kujaribu kujipatia wokovu wao kwa tohara na kushika Torati ya Musa hawawezi kuokolewa. Tohara haileti wokovu. Ni imani katika Yesu inayosababisha wokovu wenye kuwabadilisha waamini na kuwa viumbe vipya, vitakatifu.
Kwa sababu kutahiriwa si kitu wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya (Wagalatia 6:15).Yote hayo tena huonyesha jinsi ilivyo muhimu kujali mantiki wakati unapofasiri Maandiko. Njia ya pekee ya Injili kupotoshwa kwa kutumia Neno la Mungu ni kupuuza mantiki. Kinachotushangaza tu ni mioyo ya hao “watumishi” ambao wanafanya hivyo kwa ujasiri kabisa huku wakijua – yaani, makusudi.
Kwa mfano: Niliwahi kumsikia mhubiri mmoja akitangaza kwamba hatupaswi kutaja ghadhabu ya Mungu tunapohubiri Injili kwa sababu Biblia inasema hivi: “…wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu” (Warumi 2:4b). Basi, kulingana na huyo ndugu, njia inayofaa ya kutangaza Injili ni kusema habari za upendo na wema wa Mungu tu. Hayo yangewavuta watu watubu.
Lakini, unaposoma mantiki ya mstari huo ambao mhubiri aliutaja – yaani sura ya pili ya kitabu cha Warumi – tunagundua kwamba unazungukwa na Maandiko kuhusu hukumu ya Mungu na hasira Yake takatifu! Mantiki yake inaonyesha kwamba hakuna uwezekano kuwa Paulo alikusudia kusema hayo aliyosema huyo mhubiri. Hebu ona.
Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia (Warumi 2:2-9. Maneno mepesi kukazia).Paulo anapotaja wema wa Mungu anasema juu ya wema ambao Mungu anaonyesha kwa kuchelewesha ghadhabu Yake! Sasa, inashangaza jinsi mtumishi anavyoweza kusema kitu cha kijinga namna hiyo, huku akijua Biblia nzima inavyosema juu ya hilo, na kwamba imejaa mifano tele ya wahubiri waliowaonya hadharani kabisa wenye dhambi kwamba watubu.
Jinsi Maandiko Yanavyokubaliana
Kwa kuwa Biblia imevuviwa na Mtu mmoja, ujumbe wake unakubaliana tangu mwanzo hadi mwisho. Hii ndiyo sababu tunaweza kuamini mantiki kutusaidia kutafsiri maana aliyokusudia Mungu katika fungu lolote. Mungu hawezi kusema kitu katika mstari mmoja kinachopingana na mstari mwingine, na ikionekana amefanya hivyo, hatuna budi kuendelea kujifunza mpaka tafsiri ya mistari hiyo miwili ikubaliane. Kwa mfano: Katika sehemu kadha za Mahubiri ya Yesu Mlimani, inaonekana kana kwamba anapinga na hata kurekebisha sheria ya kiadili ya Agano la Kale. Hebu tazama hii:Mlisikia kwamba walisema hivi: ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino’. Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu, bali mtu akikupiga kofi shavu la kuume, mgeuzie upande wa pili pia (Mathayo 5:38-39, TLR).Yesu anatamka maneno ya Torati ya Musa, kisha anasema kitu kinacho-onekana kupinga sheria ile aliyoitamka. Tutafsiri alichosema namna gani? Je, Mungu amebadilisha mawazo kuhusu swala la maadili? Je, kulipiza kisasi kulikubalika katika agano la kale lakini hakukubaliki katika agano jipya? Kitakachotusaidia ni mantiki tu.
Yesu alikuwa anazungumza na wanafunzi Wake (ona Mathayo 5:1-2), watu ambao walichojua kuhusu Neno la Mungu ni mambo waliyofundishwa na waandishi na Mafarisayo katika masinagogi yao. Huko walisikia sheria ya Mungu ikitajw akwamba, “Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.” Maana ya amri hiyo ilikuwa imegeuzwa sana na waandishi na Mafarisayo kwa sababu ya kupuuzia mantiki yake. Mungu hakutaka amri hiyo itafsiriwe kwamba ni sharti watu wajaribu kulipiza kisasi kila mara kwa makosa madogo. Katika Torati ya Musa Yeye alisema kisasi ni chake (ona Kumbu. 32:35), na kwamba watu Wake wawatendee mema adui zao (tazama Kutoka 23:4-5). Lakini waandishi na Mafarisayo walipuuza amri hizo na kutengeneza tafsiri yao wenyewe ya maneno ya Mungu ya “jicho kwa jicho”, iliyowapa wao haki inayofaa ya kujilipiza kisasi kibinafsi.[3] Walipuuza mantiki.
Agizo la Mungu kuhusu “jicho kwa jicho, na jino kwa jino” linapatikana katika mantiki ya amri Zake zenye kutoa haki inayostahili katika mahakama za Israeli (tazama Kutoka 21:22-24; Kumbu. 19:15-21). Kuwa na utaratibu wa mahakama ni ufunuo tosha wa jinsi Mungu asivyounga mkono kisasi cha mtu binafsi. Mahakimu wasio na upendeleo wanaotazama ushahidi husika wana uwezo zaidi wa kutoa haki kuliko watu binafsi ambao wamekosewa na wenye mtazamo wa kibinafsi. Mungua natazamia kwamba mahakama na mahakimu watatoa adhabu zinazostahili hatia, bila upendeleo. Ndiyo sababu ni “jicho kwa jicho, jino kwa jino”.
Basi, tunaweza kulinganisha maneno hayo ambayo mwanzoni yalionekana yanapingana. Yesu alikuwa anawasaidia wasikilizaji Wake waliokuwa wamefundishwa uongo maisha yao yote waelewe mapenzi ya Mungu ya kweli kwa ajili yao kuhusu kisasi cha binafsi. Hayo yalikuwa yamefunuliwa tayari katika Torati ya Musa, lakini yalipotoshwa na Mafairsayo. Hakuwa anakwenda kinyume na Torati alyompa Musa. Alikuwa anadhihirisha maana yake halisi – ile iliyokusudiwa.
Sasa hilo linatusaidia na sisi kuelewa vizuri kile ambacho Yesu anatazamia kutoka kwetu kuhusu kutokuelewana kunakoweza kusababisha twende mahakamani. Mungu hakuwatazamia Waisraeli kupuuzia kila kosa walilotendewa na Waisraeli wenzao. Ingekuwa hivyo asingeweka utaratibu wa mahakama. Vivyo hivyo, Mungu hatazamii Wakristo kupuuzia kila kosa wanalotendewa na waamini wanzao (au wasioamini basi). Agano Jipya linapendekeza kwamba Wakristo wasioweza kuelewana wapate msaada wa kupatanishwa na waamini wenzao (ona 1Wakorintho 6:1-6). Wala hakuna kosa kwa Mkristo kumpeleka asiyeamini mahakamani, kwa habari ya kutokuelewana kwa hali ya juu. Mfano ni kama kutolewa jicho au jino! Makosa madogo ni kama vile kupigwa kofi shavuni, au kunyang’anywa kitu kidogo (kama vile shati lako), au kulazimishwa kwenda maili moja. Mungu anataka watu Wake wamwige Yeye na kuonyesha neema isiyo ya kawaida kwa wenye dhambi na waovu wasiofikiri.
Wamekuwepo waamini wenye nia njema tu ambao, kwa kudhani kwamba wanamtii Yesu, wanakataa kuwashtaki wale ambao wameshikwa wakiwaibia. Walifikiri kwamba wanageuza “shavu la pili – kumbe wanamwezesha mwizi kuiba tena, wakimfundisha kwamba hakuna adhabu kwa kosa kama hilo. Wakristo wa namna hiyo hawaenendi kwa kuwapenda wengine ambao wataibiwa mali na mwizi huyo huyo! Mungu anataka wezi wapate haki na kutubu. Lakini, mtu anapokukosea kwa njia ndogo kama kukupiga kofi, usimpeleke mahakamani au kumpiga kofi na wewe. Mwonyeshe rehema na upendo.
Kutafsiri Ya Kale Kwa Kutumia Mpya
Hatupaswi kutafsiri maandiko ya Agano Jipya kwa mwanga wa Agano la Kale tu, bali kila wakati tutafsiri maandiko ya Agano la Kale kwa mwanga wa Agano Jipya. Kwa mfano: Waamini wazuri tu wamesoma zile sheria za chakula za Musa, na wakafikia uamuzi kwamba Wakristo wanatakiwa kula chakula kulingana na sheria hizo. Kama wangesoma mistari miwili tu katika Agano Jipya wangegundua kwamba sheria za Musa kuhusu vyakula haziwahusu walioko chini ya Agano Jipya.[Yesu] Akawaambia, ‘Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi kwa sababu hakimwingii moyoni ila tumboni tu, kisha chatoka kwenda chooni?’ (Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote) (Marko 7:18-19).Chini ya agano jipya, hatutawaliwi na Torati ya Musa bali Torati ya Kristo (tazama 1Wakorintho 9:20-21). Ingawa Yesu aliunga mkono maadili ya Torati ya Musa (na kuyaingiza katika Torati ya Kristo), hakufundisha kwamba Wakristo ni lazima washike sheria za Musa kwa habari ya vyakula. Hata mitume hawakufundisha hivyo.
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe, wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba (1Timo. 4:1-5).
Ni wazi lakini kwamba Wakristo wa kwanza – ambao wote walikuwa Wayahudi walio-ongoka – waliendelea kufuata sheria za vyakula za agano la kale kwa sababu ya desturi zao (ona Matendo 10:9-14). Na watu wa Mataifa walipoanza kumwamini Yesu, wale Wayahudi Wakristo wa mwanzo waliwaambia wafuate sheria za vyakula za Musa kwa kiasi fulani kwa sababu tu ya kuwajali Wayahudi jirani ambao wangekwazwa (ona Matendo 15:1-21). Kwa hiyo, hakuna kosa lolote kwa Wakristo kufuata sheria za vyakula za Musa mradi tu wasizitumaini kwamba zitawaokoa au kuwapa haki fulani.
Baadhi ya Wakristo wa kwanza walishawishika pia kwamba ni kosa kula nyama au vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Paulo aliwashauri waamini waliokuwa na mawazo tofauti (kama yeye) wafuate kanuni ya upendo kwa ndugu zao wenye “imani dhaifu (tazama Warumi 14:1). Alishauri wasifanye chochote kitakachowakwaza dhamiri zao. Kama mtu ataacha kula vyakula kwa sababu ya kumwamini Mungu (hata kama imani yake haina msingi), anatakiwa kupongezwa kwa msimamo wake badala ya kulaumiwa kwa kutokuelewa kwake. Vivyo hivyo – wale wanaojiepusha na vyakula fulani kwa sababu ya imani zao binafsi wasiwahukumu wale wasiojiepusha. Wote wawili waenende kwa upendo, maana hilo linaagizwa na Mungu (tazama Warumi 14:1-23).
Vyovyote vile – Kwa sababu Biblia ni ufunuo unaoendelea, tunapaswa kutafsiri ufunuo wa zamani (yaani, Agano la Kale) kwa mwanga wa ufunuo mpya zaidi (yaani, Agano Jipya). Hakuna ufunuo wowote wa Mungu ambao unapingana – siku zote unasaidiana na kukubaliana.
Mantiki Ya Kitamaduni na Kihistoria
Kila inapowezekana, tunatakiwa kujali mantiki ya kitamaduni na kihistoria ya maandiko tunayojifunza. Kujua kitu juu ya mila, jiografia na historia ya fungu husika mara nyingi husaidia kupata mtazamo ambao tungeukosa. Hapo tunahitaji msaada kutoka vitabu vingine. Biblia nzuri ya kujifunzia (siku hizi zipo!) itakuwa na msaada katika eneo hili.Ifuatayo ni mfano michache kuhusu jinsi habari za kihistoria au utamaduni zinavyoweza kutusaidia tusichanganyikiwe tunaposoma Biblia.
1) Wakati mwingine katika Maandiko tunasoma kuhusu watu kupanda darini (au orofani) – tazama Matendo 10:9 – au kutoboa dari (tazama Marko 2:4). Itasaidia tukijua kwamba kwa kawaida huko Israeli nyumba zilikuwa na mapaa yaliyonyooka, na kwamba pembeni mwa kila nyumba kulikuwa na ngazi za kupandia huko darini. Tusipojua hilo tutafikiri juu ya mtu katika Biblia akihangaika kuparamia bati la msonge huku akipata shida mahali pa kujishikilia!
2) Tunasoma katika Marko 11:12-14 kwamba Yesu aliulaani mtini kwa sababu haukuwa na tini, japo “hakikuwa kipindi cha tini”. Inasaidia tukijua kwamba kwa kawaida miti ya mtini huwa na tini chache hata kama si wakati wake. Basi, Yesu hakukosea kuwa na matazamio aliyokuwa nayo.
3) Tunasoma katika Luka 7:37-48 kuhusu mwanamke aliyeingia nyumbani mwa Farisayo, mahali Yesu alipokuwa akila chakula. Maandiko yanasema alisimama nyuma ya Yesu akilia, kisha akaanza kulowesha miguu ya Yesu kwa machozi yake, kuipangusa na nywele zake, na kuibusu na kuipaka marhamu. Itatushangaza kwamba iliwezekanaje hayo yote kufanikiwa huku Yesu ameketi mezani anakula chakula. Je, aliingia chini ya meza? Alifanikiwaje kuiepuka miguu ya wale walaji wengine wote?
Jibu ni kwamba katika siku zile, kawaida ilikuwa kula chakula ukiwa umejilaza chini kwa ubavu mmoja karibu na meza fupi. Mkono mmoja ulitumiwa kujitegemeza na mwingine kujilisha. Yesu akiwa hivyo, aliweza kuabudiwa na kutendewa yote hayo na yule mwanamke.
Hii pia inatusaidia kuelewa jinsi Yohana alivyoweza kuegama kifuani pa Yesu wakati wa Chakula cha Mwisho, na kumwuliza swali. Yohana alikuwa amejilaza kwa ubavu, mgongo wake ukimkabili Yesu. Basi ilikuwa rahisi tu kwake kuegama kifuani pa Yesu na kumwuliza swali bila kumsumbua mtu mwingine (ona Yohana 13:23-25). Ile picha maarufu ya Chakula cha Mwisho iliyochorwa na Da Vinci, ambapo Yesu na wanafunzi wake wameketi mezani – sita upande huu na sita upande huu – inaonyesha kutoelewa Biblia kwa mchoraji huyo. Hapo alihitaji kuelezwa kidogo mantiki ya kihistoria!
Swali La Kawaida Kuhusu Mavazi
Swali moja ninaloulizwa na wachungaji duniani kote mara nyingi ni hili: “Je, ni sawa kwa wanawake Wakristo kuvaa suruali, na huku Biblia inakataza wanawake kuvaa mavazi ya wanaume?”Hili ni swali zuri tunaloweza kujibu tukitumia kanuni nzuri tu za kutafsiri, pamoja na kutazama mantiki ya kitamaduni.
Hebu kwanza tutazame zuio la Biblia juu ya wanawake kuvaa mavazi ya wanaume (na kinyume chake pia).
Mwanamke asivae mavazi ya mwanamume, na mwanamume asivae mavazi ya mwanamke, maana yeyote afanyaye mambo hayo ni chukizo kwa BWANA Mungu wako (Kumbu. 22:5, TLR).Tunapaswa kuanza kwa kuuliza hivi: “Kusudi la Mungu kutoa amri hii lilikuwa nini?” Je, lengo Lake lilikuwa kuwazuia wanawake kuvaa suruali?
Hapana – hilo haliwezi kuwa kusudi Lake kwa sababu wakati huo wanaume wa Israeli hawakuwa wanavaa suruali. Suruali hazikuhesabiwa kuwa mavazi ya kiume au ya kike, wala ya mtu yeyote. Ukweli ni kwamba, mavazi yaliyovaliwa siku za Biblia yalifanana sana na mavazi ya kike ya siku hizi! Hiyo ni habari kidogo tu ya kihistoria na kitamaduni, inayotusaidia kutafsiri vizuri kile ambacho Mungu anasema.
Sasa – kusudi la Mungu lilikuwa nini?
Tunasoma kwamba yeyote aliyevaa mavazi yasiyo ya jinsia yake alikuwa chukizo kwa BWANA. Hilo ni jambo zito. Je, kama mwanamume akichukua kitambaa cha mwanamke akakivaa kichwani kwa nukta tatu anakuwa chukizo kwa Mungu? Hapana, si hivyo.
Inaonekana kwamba, kitu alichokuwa anapinga Mungu ni watu kuvaa makusudi ili waonekane kuwa ni wa jinsia nyingine na huku si hivyo. Mbona mtu atake kufanya hivyo? Pengine ni kwa sababu alitazamia kumshawishi mwingine wa jinsia ile kimapenzi – ufuska. Kama ni hivyo, bila shaka tunaanza kuelewa jinsi tendo hilo linavyoweza kuwa chukizo kwa Mungu.
Basi, haiwezekani mtu kuamua kwamba ni makosa kwa wanawake kuvaa suruali kutokana na maneno ya Kumbukumbu 22:5, isipokuwa kama atavaa ili kujifanya mwanamume, kwa lengo la kuwashawishi wanaume kimapenzi. Akivaa na aendelee kuonekana kama mwnaamke, hafanyi dhambi kwa kuvaa suruali.
Ila, Maandiko yanafundisha kwamba wanawake wavae mavazi ya staha (ona 1Timo. 2:9). Basi, suruali zenye kubana sana kiasi cha kuonyesha umbo hazifai. Hata magauni na sketi na blauzi za namna hiyo hazifai, kwa sababu zinaweza kusababisha wanaume kutamani. Mavazi mengi yanayovaliwa na wanawake hadharani katika nchi za Magharibi (na hata Afrika!) hayafai kabisa, na ni yale yanayovaliwa na makahaba katika nchi zingine. Hakuna mwanamke Mkristo anayetakiwa kuvaa mavazi hadharani yenye kuonyesha mwili, au kwa lengo la “kuvutia”.
Mawazo Mengine Machache
Inanishangaza kwamba sijawahi kuulizwa swali la wanawake kuvaa suruali na wachungaji huko Uchina. Pengine ni kwa sababu wanawake wengi wa Uchina wamekuwa wakivaa suruali kwa muda mrefu. Nimeulizwa swali hili na wachungaji katika nchi ambazo wanawake wengi hawavai suruali. Hapo tunaona mwingiliano wa utamaduni.Pia inanishangaza kwamba sijawahi kuulizwa swali kama hilo na watumishi wanawake katika nchi ya Myanmar, ambako kimila wanaume huvaa vazi linalofanana na sketi liitwalo longgi. Ni kwamba mavazi ya kike na ya kiume hutofautiana kutoka mila hadi nyingine, hivyo tunapaswa kuwa waangalifu tusilazimishe utamaduni wetu kuingia katika Biblia.
Mwisho: Nashangaa ni kwa nini wanaume wengi wasiotaka wanawake wavae suruali kwa sababu ya Kumbukumbu 22:5 hawaoni sababu ya kujipima wenyewe na Walawi 19:27. Tunasoma hivi:
Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.Inawezekanaje wanaume – kinyume kabisa cha Walawi 19:27 – wanyoe kabisa ndevu walizopewa na Mungu, zenye kuwatofautisha na wanawake, kisha wawahukumu wanawake wanaovaa suruali kwamba wanajaribu kufanana na wanaume? Hapo kuna unafiki kiasi fulani!
Labda maelezo kidogo ya kihistoria yatasaidia kuelewa kusudi la Mungu katika Walawi 19:27. Kuharibu pembe za ndevu ulikuwa utaratibu wa kidini wa kipagani katika kuabudu sanamu. Mungu hakutaka watu wake waonekane kuwa wamejitoa kwa miungu ya kipagani.
Nani Anayezungumza?
Kila mara tutazame nani anazungumza katika maandiko, maana hilo litatusaidia kutafsiri fungu hilo vizuri. Japo kila kilichomo katika Biblia kimevuviwa kuwemo, si kila kitu kilichomo katika Biblia ni Neno la Mungu lililovuviwa. Nini maana yangu?Katika mafungu mengi ya Maandiko, maneno ya watu ambayo hayajavuviwa yameandikwa. Kwa hiyo, hatupaswi kufikiri kwamba kila kitu kilichosemwa na watu kilichoandikwa katika Biblia kimevuviwa na Mungu.
Kwa mfano: Watu wengi hukosea kwa kutumia maneno ya Ayubu na rafiki zake kana kwamba ni maneno yaliyovuviwa ya Mungu. Kuna sababu mbili kubwa zenye kuonyesha kwamba ni kosa. Kwanza: Ayubu na rafiki zake walibishana kwa sura thelathini na nne. Hawakukubaliana. Basi, si kila walichosema kinachoweza kuhesabiwa kuwa Neno la Mungu lililovuviwa kwa sababu Mungu hajipingi Mwenyewe.
Pili: Mwishoni mwa kitabu cha Ayubu, Mungu mwenyewe anazungumza, naye anamkemea Ayubu na rafiki zake kwa kusema mambo ambayo hayakuwa sahihi (ona Ayubu 38 hadi 42).
Tunapaswa kuwa makini tunaposoma Agano Jipya pia. Mara kadhaa Paulo anasema wazi kwamba baadhi ya mafungu aliyoandika ni mawazo yake au maoni yake binafsi (ona 1Wakorintho 7:12, 25-26, 40).
Nani Anasemeshwa?
Hatupaswi tu kuuliza nani anayezungumza katika fungu lolote la Biblia. Tunapaswa pia kuona nani anaambiwa kinachosemwa. Tusipofanya hivyo, tutatafsiri vibaya kitu – kwamba kinatuhusu – kumbe si hivyo. Au tunaweza kutafsiri kwamba kitu hakituhusu, kinachotuhusu.Mfano: Wengi hudai hii ahadi ipatikanayo katika Zaburi mojawapo, wakiamini ni yao.
Atakupa haja za moyo wako (Zaburi 37:4).Lakini je, ahadi hiyo ni kwa kila aisomaye au ajuaye habari zake? Hapana! Tukisoma mantiki, tutaona kwamba inawahusu watu fulani tu, watakaotimiza masharti matano.
Umtumaini BWANA, ukatende mema, ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Jifurahishe katika BWANA, naye atakupa haja za moyo wako (Zaburi 37:3-4, TLR).Ni muhimu sana tujue nani anaambiwa maneno husika. Ona mfano mwingine.
Petro akaanza kumwambia [Yesu], ‘Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe’. Yesu akasema, ‘Amin nawaambieni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume au ndugu wake, au mama au baba au watoto, au mashamba kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume na ndugu wake na mama na watoto na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele’ (Marko 10:28-30).Ni kawaida sana mahali pengine kudai hiyo “mara mia” wakati mtu anapotoa kumsaidia mtu anayehubiri Injili. Lakini, hiyo ahadi ni kwa watu wa namna hiyo? Hapana. Imetolewa kwa watu wanaoacha familia zao, mashamba yao au hata nyumba zao ili kuhubiri Injili, kama alivyofanya Petro aliyemwuliza Yesu swali hilo. Alitaka kujua thawabu yake na wanafunzi wengine ingekuwa nini.
Cha kushangaza ni kwamba, wale wenye kuhubiri juu ya kurudishiwa mara mia hukazia sana nyumba na mashamba. Hawataji sana kuhusu watoto na udhia, ambavyo pia vimetajwa! Yesu hakumaanisha kwamba watakaoacha nyumba zao watapata nyumba mia moja badala yake. Aliahidi tu kwamba watu wakiacha familia zao na nyumba zao, wanafamilia wao wapya kiroho watawakaribisha majumbani mwao kukaa. Wanafunzi wa kweli hawajali sana kuhusu kumiliki vitu maana hawana chochote chao – wao ni mawakili tu wa vitu vya Mungu.
Mfano Wa Mwisho
Watu wanaposoma mahubiri ya Yesu ya pale “Mlima wa Mizeituni” katika Mathayo 24 na 25, kuna wanaodhani kwamba alikuwa anazungumza na wasiookoka, na kwamba hayo aliyosema hapo hayawahusu. Hayo ni makosa. Wanasoma Mfano wa Mtumishi Asiyekuwa Mwaminifu na Wanawali Kumi kana kwamba ni mambo wanayoambiwa wasioamini. Lakini kama nilivyokwisha sema huko nyuma, waliokuwa wanaambiwa ni wanafunzi waliokuwa karibu sana na Yesu (tazama Mathayo 24:3; Marko 13:3). Basi, kama Petro, Yakobo, Yohana na Andrea walihitaji kuonywa juu ya uwezekano wa kutokuwa tayari Yesu akirudi, sisi pia tunahitaji kuonywa juu ya hilo. Maonyo ya Yesu katika mafundisho Yake pale Mlima wa Mizeituni yanamhusu kila mwamini – hata wale wasiodhani yanawahusu kwa sababu ya kushindwa kujua waliokuwa wanaambiwa.Kanuni ya tatu: Soma na moyo ulio wazi. Usilazimishe imani na mafundisho yako kwenye fungu la Maandiko. Ukisoma kitu kinachopingana na imani yako, usijaribu kuibadili Biblia. Badilisha unachoamini.
Kila mmoja wetu husoma Maandiko akiwa na mtazamo au msimamo fulani tayari. Kwa sababu hiyo, mara nyingi ni vigumu sana kwetu kusoma Biblia kwa moyo ulio wazi na wa dhati. Tunaishia kulazimisha imani zetu kwenye Maandiko, badala ya kuruhusu Biblia iumbe imani au itikadi au mafundisho yetu. Mara nyingine hata tunatafuta Maandiko yatakayounga mkono itikadi zetu, na kupuuza yale yenye kupingana nazo.Angalia mfano huu niliokutana nao hivi karibuni, wenye kuonyesha jinsi unavyoweza kulazimisha itikadi yako iingie kwenye mstari. Mwalimu mmoja alianza kwa kusoma maneno maarufu sana ya Yesu – Mathayo 11:28-29.
Njooni kwangu ninyi nyote mliochoka, na wenye kulemewa, nami nitawapumzisha. Ivaeni nira yangu mjifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu (TLR).Kisha mwalimu akaendelea kwa kufafanua kwamba Yesu alikuwa anatoa mapumziko aina mbili. Pumziko la kwanza (kwa maoni yake) ni la wokovu, katika 11:28, na la pili ni la uanafunzi katika 11:29. Pumziko la kwanza linapatikana kwa kumjia Yesu, na la pili linapatikana kwa kujitoa Kwake awe Bwana, au, kujitia nira Yake.

Comments