RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE : MANENO YA HEKIMA

Mafanikio ya kila mmoja aliyeko hapa Duniani, chanzo chake ni KUSIKIA. Uharibifu wowote unaouona huku Duniani, Chanzo chake ni nini, Ni KUSIKIA.

Hata wale wezi hawaendi kuiba mpaka wasikie wanaenda kuiba nini, hakuna mwizi atakayeenda kuiba.

Hata yule anayefanya uasherati hawezi kufanya uasherati mpaka kwanza asikie, anaambiwa "nakupenda sana, wewe ni mzuri sana,".. basi akiwa anashangaa anashangaa, anashangaa, anashangaa, anasikiliza yale anayoyasikia, yanamvuta, yanamvuta, yanamvuta mpaka anafanya hicho anachofanya; Chanzo chake ni nini?, ni KUSIKIA.

Nabii na Mtume Josephate Mwingira

Uharibifu wowote unaouona huku Duniani chanzo chake ni Kusikia.USTAWI wowote unaouona huku Duniani, chanzo chake ni KUSIKIA.

Sasa ili wewe uwe wa tofauti kuanzia sasa, ili uwe wa tofauti na vile ulivyokuwa hapo nyuma; Lazima pia USIKIE ili uwe wa Tofauti. Ni lazima USIKIE, Usikie nini, Usikie TOFAUTI na ulivyokuwa unasikia hapo nyuma, maana ili UWEZE KUWA WA TOFAUTI, ni lazima USIKIE Tofauti, maana yale uliyoyasikia mwanzo yamekuharibu ukaharibikiwa.

Comments