Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye atakuwa mgeni rasmi katika
tamasha hili kubwa la mtumishi wa Mungu Victor mwana wa Aron katika
kanisa la DCT Tabata Shule Dar es Salaam. Tuna kila sababu ya kumshukuru
Mh. Fredrick Sumaye kwa kutenga muda wake kwajili ya kushiriki tamasha
hili la kuzindua albamu ya Victor Aron inayoenda kwa jina la Kanuni au
2x2. Tunatambua kuwa ana majukumu mengi kwaajili ya ujenzi wa Taifa
letu, lakini ameweza kukubali kuungana na kijana wake. Mungu azidi
kumpigania Mh. Fredrick Sumaye kwa kazi zake na mipango yake
aliyoipanga.
Mh. Fredrick Sumaye
Tamasha hili litaambatana na uimbaji kutoka kwa waimbaji mbalimbali kama vile Christina Shusho, Madam Ruti, Christopher na wengine wengi. Uzinduzi utafanyika siku ya Jumapili 02/11/2014 kuanzia saa 8 mchana, kwahiyo unaombwa kuwahi mapema ili ujipatie nafasi nzuri ya kukaa. Mbali na uzinduzi tamasha hili limeandaliwa kwaajili yako wewe kuja kumsifu Mungu, na hakuna kiingilio kabisa.
Victor Aron
Victor Aron ataimba LIVE nyimbo zaidi ya tano kwa utukufu wa Mungu.Akiongea na Rumafrica, alisema yeye na crew yake wamejiandaa vya kutosha na hawana wasiwasi kabisa siku hiyo, kwahiyo anaomba sana watu wafike na ikiwezeka kila mmoja aje na marafiki zake kupokea baraka zao kwa njia ya sifa.
ANGALI TANGAZO UTAJIFUNZA JAMBO

Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523
Comments