RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI SIKU YA KWANZA KIKIWASILI KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA K.K.K.T USHORA KIBAYA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA KWA KUFANYA UMISHENI

Mwandishi na Picha: Rumafrica
Ikiwa ni siku ya kwanza kwa waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania kukanyaga katika viwanja vya kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida, wanakijiji waliwapokea waimbaji hawa kwa nderemo na vifijo wakiongozwana Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh. Martha Mlata. Waimbaji na wachungaji walioalikwa walionekana wenye kushangazwa na maandalizi waliyoyakuta katika viwanja hivyo ikiwa ni pamoja na jukwaa kubwa lenye viwango vya kimataifa likiwa limefungwa kijijini hapo.
Mh. Martha Mlata kwa mara ya kwanza wakicheza katika viwanja vya kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya.

Mh. Martha Mlata alionekana akiwa na furaha kubwa sana kuona waimbaji wenzake wameweza kukanyaga katika viwanja vya Ushora kwa kazi ya Mungu. Mh. Martha Mlata ni mmoja wa walezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania na pia ni mwimbaji maarufu sana wa nyimbo za Injili, alweza kumshukuru sana Mungu kwa wema wake na kuwalinda waimbaji na wageni wote walioalikwa katika shughuli ya umisheni.
Mh. Martha Mlata wa tatu kutoka kulia

Lengo kubwa la waimbaji kufika katika kijiji hiki cha Ushora Kibaya ni kufanya umisheni, kufundisha Neno la Mungu, kuwaombea wenye uhitaji na kuwafungua waliofungwa na vifungo vya shetani, kupanda miti kama moja ya utunzaji mazingira, kuonyesha filamu za maisha ya Yesu  kwa wanakijiji hao, kuwaelimisha wanakijiji na kuwaburudisha kwa njia ya uimbaji.

Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) Stella Joel akifuatia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh. Martha Mlata na ni Mlezi wa CHAMUITA,

Katika ziara hii kulikuwa na wachungaji, wainjilisti, walimu na viongozi mbalimbali wa dini walioweza kuhudhuria mkutano huu mkubwa.
Kwaya ya kanisa la KKKT Ushora Kibaya ikiwakaribisha wageni kwa nyimbo za nguvu.

Sasa ngoja tuone baadhi ya picha zinazoonyesha jinsi wanakijiji walivyowapokea wageni wao tarehe 14.11.2014.




 Mh. Martha Mlata (kushoto) na Stella Joel
 wa tatu kutoka kushoto ni mwimbaji Paffii
 Wa tatu kutoka kulia ni mwimbaji Ann Annie kutoka Arusha
Kutoka kulia ni MC kutoka Ushora, Jane Misso, Stella Joel, Mh. Martha Mlata, Askofu mkoa wa Singida



Gari lililokuwa limebeba generator kwaajili ya umeme.


Comments