RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MALEBO ALIYEIMBWA NA MUNISH KUSHIRIKI TAMASHA LA MAXIMILLIANI MACHUMU MWANAMAPINDUZI

Watu wengi tumekuwa tukidhani Mch. Munishi alimwimba Malebo kama mtu wa kufikirika ili aupambe wimbo wake, la hasha..Malebo ni mtu wa kweli na sio wa kufikirika kama tulivyokuwa tukidhani, na yele aliyoimbwa ni kweli yalikuwa maisha yake. Tunamshukuru Mungu Malebo kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya kidunia, anamtumikia Mungu wetu wa mbinguni.
Katika Tamasha la uzimduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Mch. Maximilian Machumu (Mwanamapinduzi) au Majeshi Majeshi inayoenda kwAKUFA, Malebo na Munishi watakuwepo na watamwimbia Mungu siku hiyo na kushuhudia maisha yao kabla na baada ya wokovu.
Malebo aliyesimama akisalimia waumini baada ya kusalenda kwa Yesu Kristo.

Tamasha hili litaanza saa 7:00 mchana na kuelekea pale Kawe katika viwanja vya Tanganyika Pekers kwa Mch. Josephate Gwajima siku ya Jumapili 7.12.2014, na hakutakuwa na kiingilio chovhote. Waimbaji wakongwe wa zamani watakuwepo kuleta uwepo wa Mungu ambao utakubadilisha kimasha siku hiyo. Usikose kuja na jamaa yako au ndugu yako ili awe shahidi siku unapokea baraka za Mungu kupitia uimbaji.

Wa pili kutoka kushoto ni Malebo akifuatiwa Mch. Munishi.

Yaani siku hiyo sipati picha kwani kutakuwa na waimbaji wakongwe kama vile david Robert. Mch, Jangalason, Mtume Komanaya, Mzee Makassy, Mch. Bupe Kingu, na wengine wengi kama utakavyowaona katika tangazo hapo chini.
Kutoka kushoto ni Malebo, Mch. Maximilian Machumu (Mawanamapinduzi) mdada wa Yesu, David Robert, Munishi


SIKILIZA WIMBO WA MAXIMILIAN MACHUMU


SIKILIZA WIMBO WA MALEBO KUTOKA KWA MUNISHI