RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO NKONE NA MADAM RUTI KUONYESHA MAVAZI SIKU YA TAMASHA LA VENERANDA BUGERAHA


Sipati picha siku hiyo pale Madam Ruti na Upendo Nkone kufanya Fashion Show katika tamasha la kubwa la mwimbaji wa nyimbo Injili Tanzania Veneranda Bugeranda. Tumezoea kuwaona waimbaji hawa wakiimba lakini siku hiyo ya Jumapili 30.10.2014 kutakuwa na vitu tofauti ambavyo hujawahi kuona. Waimbaji hawa wataonyesha mavazi ya kuvaa maofisini, beach, nyumbani, outing, madhabahuni, na sehemu mbalimbali.
http://tetemesha.com/tetemesha/images/art/347.jpg
Upendo Nkone
Tamasha hili litaambatana na kuwasaidia watoto yatima kutoka katika kituo cha watoto yatima cha SIFA FOUNDATION kilichopo hapa jijini Dar es Salaama. Watu wataweza kupata muda wa kukaa na kuongea na hawa watoto wanaohitaji faraja. Fikiria hawa ni watoto waliokosa wa wazazi pande moja au na wengine pande zote mbili yaani baba na mama. Watoto watajiisikia vizuri sana kuona wewe umetenga muda wako kukaaa na kufurahi nao. Siku hiyo Mungu atasema na wewe na hakika utapokea baraka za Mungu.

Madam Ruti
Mbali na kuwasaidia watoto hawa pia kutakuwa na waimbaji wengi sana watakashusha wingu la upako kwa njia ya uimbaji. Kwahiyo usikose siku hiyo ya kipekee kabisa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQok7b2r4rcPCql_UC2Vjbz4d1AJ7nAmGUpgSePlX2pi0jdieS_SNThTi-rOuY6oQNm7LTuBXexno7w6EFGOUQJJC5fi4qzikdQV_cul8YPXza3VC5EjHXtJ_haPnitFoQ4YbZUiJHDZdX/s1600/DSC_4183.JPG
Veneranda Bugeranda

Comments