RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ROSE MUHANDO, BONNY MWAITEGE NA GASTON SAPULA WATINGA OFISI ZA RADIO KASIBANTE



Msanii wa muziki wa Injili, Bonny Mwaitege (kulia) akisalimia na Mtangazaji wa Radio Kasibante Mwl. Joyce Ruboz mapema leo katika kipindi cha Gospal Flava cha Kasibante FM 88.5.

Mtumishi wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando akiwa kwenye studio za radio Kasibante FM 88.5 akionekana mwingi wa furaha wakati akihojiwa na mtangazaji (hayupo pichani) wa kipindi cha Gospal Flava leo Bukoba mjini.

Mtangazaji wa kipindi cha Gospal Flava Mwl. Joyce Ruboz akifurahia jambo baada ya kuwaona waimbaji wa Injili wakiporomosha sauti zao tamu wakati wa kipindi chake leo asubuhi.

Mwalimu Joyce Ruboz pia ni mmoja wa waratibu wa fainali za Biblia mjini Bukoba katika suala zima la kutanua na kuendeleza jamii kupitia vipindi vya dini. Wasanii Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula walitinga ndani ya Radio Kasibante FM tayari kupamba fainali za mashindano hayo leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 8 mchana.
Boniface Mwaitege (kulia) akiwa na msanii mwenzake wa Nyimbo za Njili, Gaston Sapula kwenye Studio za Radio Kasibante FM Bukoba leo.

...Rose Muhando akiwa na Gastona Sapula studio.
...Rose Muhando akiwa Katika Ukumbi wa Radio Kasibante FM
Mtangazaji wa Radio Kasibante FM 88.5, Abera naye alikuwepo katika Ofisi zao, anapokea wageni kwa tabasamu (hawapo pichani).

Picha ya pamoja Mwalimu Joyce Ruboz na Wasanii wa Injili wanaotarajia kupamba fainali za Biblia leo katika Uwanja wa Kaitaba.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe (wa tatu toka kulia) naye alipata picha ya pamoja na wasanii hao.
(PICHA: FAUSTINE RUTA/BUKOBA)

Comments