RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE: JAMBO LOLOTE UTAKALOLIAZIMIA MWAKA HUU WA MTEMBEO WA MUNGU NA LITOKEE KWAKO

Rumafrica Jumapili hii iliweza kufika katika kanisa la Efatha Mwenge kwa Mtume na Nabii Josephate Mwingira. Mchungaji wa eneo la Sayuni  Mch. Aimana Dominick ndiye aliyetoa neno la Mungu Jumapili hii na alianza kwa kusema, huu ni mwaka wa mtembeo, mtindo wa Bwana kutembea ni tofauti na ule wa  mwanadamu, tunatakiwa kuweka bidii kwa yale yanayompa Bwana utukufu. Tujitahidi mwaka unapoisha tuone matokeo ya mtembeo.
Picha ya Mch. Aimana Dominick katika ibada zilizopita.
Ayubu 22:28, Nawe utakalokusudia Neno nalo litatokea kwako, na mwanga utaangaza njia zako. Ukileta bidii kwa hilo ulilokusudia, litatimia na kuthibitika.Fikiria ni mabo yapi unakusudia mwaka huu yatokee kwako?

Picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira katika ibada zilizopita.

Unapokutana na changamoto katika wokovu wako, wewe fanya bidii kumtafuta Bwana na kuulinda wokovu wako.Watu wengi wanapokutana na magumu wanamsahau Mungu na kukimbilia kwa waganga au kufanya vitu kinyume na taratibu za Mungu.
Hakuna linaloshindikana kwa huyu Mungu tunayemwabudu, tunatakiwa kutii na kufuata yale anayotuagiza. Mungu wetu ameweka taratibu zake katika Biblia na tunatakiwa kuisoma hii Biblia ili iweze kutuongoza kufuata yale Mungu anataka tuyafanye.

Weka bidii katika kazi ya Mungu ili hilo ulilowekeza liweze kutimia.Hutakiwi kukamata sana udini bali mkamate sana Mungu wako kwa bidii,  unatakiwa kujenga uhusiano madhubuti na Yesu kuliko huyo unayeamini kuwa ni wamuhimu sana hapa duniani.Watu wengi sana wamewaweka watu kuwa miungu yao, eti kwasababu ana mali nyingi na kutokana na mali zake anayeheshimika kuliko Mungu. Kama akiambiwa leo usiende kanisani twende kutafuta pese naye anakubali.
Jambo gani ulisikia na ukafanyia bidii au kulifanyia kazi, na kama ulifanyia ni  kwa kiasi gani? Unapoona changamoto fanya bidii kama ulivyoweka makubaliano na Bwana wetu Yesu Kristo kuwa nikipata fursa fulani nitafanya kwa bidii. Watu wamekuwa wakiomba kupata kazi na wakipata kazi wanaanza uzembe kazini na kufanya kwa ulegevu. Hii sio tabia nzuri na unapofukuzwa kazi unaanza kusema kuna mkono wa Mungu. Fanya kazi yako kwa bidii.
.
Mungu wetu yupo juu ya changamoto tunazopitia, ahadi za Mungu ni za kweli , kwa hiyo fanya bidii katika hizo ahadi alizokuahidia. Unapopata changamoto usikate tamaa na kurudi nyuma.

Hakuna jambo lolote litakalo zuia wewe kupata hilo ulilopanga mwaka huu, kwa hiyo fanya bidii kwa hilo jambo unalotaka litokee. Kama unataka kupata mtoto mwaka huu basi fanya bidii mwezi huu wa kwanza (Januari), ukifanya uzembe  basi hutazaa mwaka huu, bali utazaa mwakani. Tunatakiwa kuwa wajanja sana katika maswala ya kiimani. Weka malengo yako uliyopanga na fanyia kazi, kwani huo ni waraka wako, uking’ang’ania hilo ulilopanga lazima litokee.
Bwana anasema ni sikukuu siku ile ya kumkiri Bwana, unatakiwa kukiri kwa hilo unalotaka litokee, unapokiri tofauti na neno basi hutapata kile unachotaka kutokea. Kwa mfano unaomba Bwana akupe mtoto, unaenda hospitalini madaktari wanasema hutapata mtoto, wewe amini lile la Mungu.
Unapopewa malengo basi yafanyie kazi ili malengo hayo yatimie kwa wakati wake, neema ya Bwana ipo kwani ipo Mungu wetu siku ataosha ujinga wa kutofanya jambo kwa bidii.

Ili tuweze kwenda vizuri katika ahadi lazima:-
a.      
(a) Kuwekeza katika muda.
Ukidhamiria kweli kuwekeza katika muda, muda utakukumbusha, kama ulipanga kufanya jambo kwa muda muafaka jaribu kuwa na kitu kitakacho kukumbusha.

Mungu wetu aliwekeza kwenye muda kwani alisema kuwe na mchana na giza, kila jambo linalotakiwa kufanyika mchana lifanyike na yale ya usiku yafanyike.

Mungu wetu ameweka kitu fulani kwetu sisi, ndio maana kama umepanga kufanya jambo fulani katika muda uliopanga utaona ukifika ule muda uliopanga utasikia sauti inakukumbusha kufanya lile jambo ulilokusudia kulifanya, ukienda kinyume basi utakuwa umepoteza ule muda wako wa kulifanya hilo jambo..

Waefeso 5:15-16, Angalieni sana jinsi mnavyoenenda, sio kama wasio na hekima, maana uovu waweza kukutokea. Unapotaka kuwekeza kitu Fulani usikurupuke bali  angalia kwa makini kabla ya kuwekeza. Unaweza kuwekeza mahali ambapo hutapata faida kama haukuwa makini.

Kwa nini tunataka kuwekeza kwenye muda? Hekima inahitajika sana kuwekeza kwenye muda, hekima ya Mungu inakupa akili ya kutunza muda. Kila iitwapo leo muda hauongezeki kwako, bali muda unapungua ila umri wako unaongezeka kwako.

Unaposikia sauti ndani mwako inasema ufanye jambo kwa kipindi hicho basi fanya kwa wakati huo, ukichelewa lile jambo linabadilika na kuongezeka thamani. Kwa mfano unasikia sauti inasema nunua lile shamba, ukapuuzia, ukija siku nyingine thamani ya shamba inaongezeka.

Mara nyingi tumekuwa hatuwekezi kwenye muda, tumekuwa watu wa kushindwa na kufeli katika swala la maendeleo.Tukubaliane kuwekeza katika muda ili yale mazao mema yaweze kupelekwa sokoni kuuzwa. Makanisa yapo mengi na huduma zipo nyingi lakini yote yatakwenda mbinguni.

Ukikosea kuwekeza kwenye muda piga magoti na muombe Mungu akusaidie ili uvune lile tunda ulilokusudia kuvuna. Tamani kuwekeza kwenye muda na fanya bidii kuwekeza kwenye muda, ukifanya hivyo utaona mambo yako yanakwenda sawa sawa.

Unapoenda ibadani weka kusudio lako kwamba kitu gani Mungu akutendee, usije Kanisani kama mazoea kwani utakuwa unapoteza muda wako na hakuna utakachopata baada ya ibada kuisha.

Ukiona muda unakwenda na kusudio lako halijatokea basi muulize Mungu mbona hili jambo halijatokea?

Jitahidi katika mtembeo huu wa Mungu usiwe msindikizaji, weka makusudio yako mwaka huu kuwa haya nataka yatokee mwaka huu, na yafanyie bidii.


Comments