Rumafrica ilibahatika tena kufika katika kanisa la Efatha Mwenge kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira na kuhudhuria ibada ya Jumapili 01.02.2014 ambapo Mch. Mercy aliweza kuhubiri Neno la Mungu ambalo liliwagusa watu wengi sana na kujikuta wanalia. Rumafrica ilitokwa na machozi sana kutokana na maombezi yaliyofanyika katika ibada hiyo. Mchungaji Mercy ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alikuwa na haya ya kusema katika ibada hii takatifu:
Nabii na Mtume Josephate Mwingira akiwa ibada. Picha ni ya ibada zilizopita na sio ya Jumapili ya mahubiri haya.
Tunaenda kufungua mlango wetu uwe wazi, na chochote kinachozuia ni lazima kitoke. Mwaka huu ni mwaka wa kutembea na Mungu, kuna mambo yanahitajika kufanyika ili uweze kutembea na Mungu. Wakorinto 1:16. Mlango uko wazi kwaajili yako lakini kuna vipingamizi vingi na katika hivyo vipingamizi unahitaji kupamba nanvyo kuvishinda.
Picha ya ibada za zilizopita
Katika dunia ya leo kuwa vingamizi vingi sana ambayo vinakufanya wewe usisonge mbele na baadhi ya vingamizi hivi ni:
(a) Tabia yako
Kuna mambo ambayo Mungu ameahidi lakini kuna vipingamizi na moja wapo ni tabia yako, jiulize tabia yako inafanana na tabia ya Mungu? Tabia yako lazima ifanane na Mungu ili kuepuka hicho kipingamizi. Tabia yako ikiwa mbaya inakusababishia kuwa mbali na baraka za Mungu. Uwepo wa Mungu unakuwa mbali sana na wewe na shetani anachukua nafasi kuhakikisha hufiki mbali na imani yako ya kumuamini Mungu.
(b) Mazingira ambayo tunaishi inawezekana ikawa nyumbani/ ofisini kwako, ibilisi anatumia mbinu kufunga ufahamu wako, kupinga malengo yako. Kila ukipanga jambo fulani halifanyiki.
Picha ya ibada za zilizopita
Leo tutakuwa na maombi makali sana katika ibada ya leo na Mungu anakwenda kufanya jambo ambalo hujawahi kuliona.
OMBI LA KWANZA: BWANA ATUPE MAVUNO MENGI ILI TUPATE WATENDA KAZI
Kuokoka kwetu akutoshi bali tunatakiwa neema ya wokovu kuwaleta watu wengine kuwa watenda kazi. Tuombe Mungu aweze kuleta watenda kazi, hao kondoo tutakao waleta lazima wakae zizini na sio kuondoka. Kutoka 10:1-3. Kipindi cha nyuma Bwana alituma watenda kazi.
OMBI LA PILI: MUNGU ATUPE KUTIMIZA AU KUFIKIA MALENGO, TUPE KUSUDIO LA KIUNGU
Joshua 1:7-8. Mungu wetu ni Mungu asiye na upendeleo, ni Mungu aliyejaa huruma na upendo. Tuombe Mungu atupe uhodari na ushujaa tusiwe na hofu kwani mlango upo wazi, ili Mungu atembee na wewe unatakiwa kutii yale ambayo watumishi wanakuagiza. Yashike na kuyafanyia kazi unayoagizwa, kutii ni bora kuliko dhabihu.
Tunatakiwa kutembea katika sayari hii kwa bidii ili kutimiza kusudi la Mungu. Jiulize nguvu ya Mungu iko ndani yako? Usisababishe moyo wako kuumia, maana moyo unavyoumia nguvu ya Mungu inapungua ndani yako. Linda sana moyo wako kwa kuwa huko zinatoka chemichemi za uzima
OMBI LA TATU: MUNGU AHUISHE UTENDAJI WETU NDANI YETU ILI ATIMIZE AHADI ZAKE
Warumi 8:28, Efeso 3:20. Ili tuweze kupokea mazuri si kwa kuomba sana bali ni kuwa na nguvu itakayokuwa ndani yetu. Nguvu ya Mungu itasababisha kupokea aliyoahidi kwetu, tunapokea nguvu kwa kupitia roho mtakatifu, nguvu ya Mungu inatakiwa kudumu ndani yetu.
OMBI LA NNE: MUNGU ATUPE AFYA NJEMA ILITUWEZE KUTIMIZA AHADI ZAKE
Matendo 4:7. Unatakiwa kufanya makubwa mpaka watu waulize ni kwa nguvu gani unafanya makubwa. Hakikisha unabeba jina la Yesu na nguvu ili kufanya mambo ya ajabu na makubwa, unafanya makubwa ndani ya biashara yako mpaka watu watashangaa. Isaya 53:4-5. Mungu anatamani kufanya makubwa katika maisha yetu na shetani analeta udhaifu katika miili yetu ili tushindwe kufanya kazi ya kumpendeza Mungu.
Shetani analeta magonjwa ili ushindwe kufika Kanisani kujifunza mbinu za kumpinga shetani. Sema kwa kupitia viungo vyangu utaenda kufanya makubwa na watu watafurahia ukuu wa Bwana.
Baada ya Mch. mercy kumaliza kuhubiri mke wa Nabii Josepahte Mwingira alikuwa na haya ya kusema kwa wahubiri wake.
Usikae nyumbani mwa Bwana kwa mazoea, tunza sana kile ulichonacho, wewe unayejua wokovu tunza wokovu wako. Uwe na adabu na kuwa na tabia nzuri na inashuhudia kwa wengine, jivunia wokovu wako, usipokaa na Yesu utaona aibu kusema umeokoka kwasababu huna ujasiri.
Kama utatembea na Mungu umaskini unakwisha kwasababu unatembea na Mungu, usipende kupokea laana bali tamani kupoka Baraka. Unatakiwa kuendelea na maombi hata kama upo nyumbani.
Comments